Ni lini ubunge umeanza kuwa dili?

Rockefeller

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,196
2,151
Habari za jioni wakuu,

Nilikua nasikiliza hotuba moja ya Wasira akielezea wasifu wake hasa katika utumishi wa uma. Katika hotuba hio Wasira anaelezea mwaka 1970 alivyochaguliwa kuwa mbunge akiwa kijana wa miaka 25 tu, anaeleza alivyoacha ubunge na kuchaguliwa kuwa mkuu wa mkoa na baadae kwenda kufanya kazi ubalozini Washington.

Kiukweli nilishangazwa kwanza sikuwahi kujua kama ameshawai kushika nafasi hio akiwa na umri mdogo hivyo wa miaka 25. Pili nikawa najiuliza mtu anaachaje ubunge kwenda kuwa mkuu wa mkoa au mfanyakazi wa ubalozi??

Nikamuuliza mzee mmoja jirani, akanambia kwamba zamani ubunge haukuwa dili kama ilivyo saivi kwamba zamani ubunge ulikua ni kazi ya wapiga domo tu na wasiosoma. Mbunge hakuwa na reputation kama waliyonayo wa sasa hivi.

Nikasema nije kwa wazee wa jamvi mtueleze, Je ni kweli miaka hiyo ubunge haukuwa dili kama ilivyo sasa na ni lini ubunge ulianza kupata heshima kama unayopata sasa hivi.

Asanteni.
 
Mpaka leo hii ubunge ni kwa ajili ya wapumbavu ambao hawajasoma na wanataka kupata pesa za kisomi kiurahisi, hatma yake ni hii mikataba ya Bandari.

Mtu kama Babu Tale nae ni mbunge halafu unauliza kama ubunge ni dili.

Kuna baadhi ya wabunge ni malimbukeni na watupu kichwani kiasi cha kushindwa hoja na mtoto wa darasa la nne.
 
Kwani wabunge wa mwaka 70 walipatikanaje kwanza?

Katiba ya mwaka 77 ilipatikanaje?

Hata wa sasa hawana credibility...ni chawaz
 
Back
Top Bottom