Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,594
- 1,683
Inakuwaje kwamba Kenya, kuanzia kati ya mwaka uliopita, ilishuhudia kuanguka vibaya kwa sarafu yake, Kenya Shilling, hadi kufikia mwisho wa 2023, ilipoteza asilimia 20% ya thamani yake.
Shilingi ya Kenya iliwahi kubadilishwa Sh.167 kwa dola moja, kutoka shilling 135 kabla rais Ruto kushika madaraka.
Lakini katika wiki mbili zilizopita, wataalamu wa uchumi Kenya, wakiongozwa na Waziri wa Fedha, walifanya juhudi za ziada kuinua kima cha Shilingi, na hii leo shlingi inabadilishwa kwa sh. 137 kwa dola moja. Wataalamu hao wameapa kuirusha shillingi hadi kufikia sh.100 kwa dola 1 hadi Juni.
Baadhi ya faida za kupanda thamani ya sarafu ya nchi ni kupunguza mzigo wa deni, hivi kwamba serikali italipa kiasi hafifu. Pia bidhaa zinazotoka nje zinakuwa na bei hafifu, na la muhimu zaidi kuna uwezekano wa kupungua bei za bidhaa zinazoingizwa. Kama vile Kenya hivi sasa bei ya mafuta imeshuka kwa zaidi ya shilingi 27 kwa lita.
Ukitazama Tanzania, hali inazidi kuwa mbaya katika exchange rate na kana kwamba hakuna juhudi zozote zinazofanyika ili kuinua kima cha shilingi ya Tanzania. Twasikia maneno tu ya kejeli na ya kihuni yasiyoonesha taaluma, kwamba 'tunakopa kwa vile tuna uwezo wa kulipa' kana kwamba kukopa ni ibada ya faradhi!
Nashuku kwamba kuna uhaba wa elimu na uelewa wa masuala ya fedha katika ngazi za juu za wanaoongoza sera za fedha nchini humu. Kama ungekuwepo, suala la thamani ya fedha yetu lingekuwa lajadiliwa kila siku, kama ilivyo Kenya. Hili ni suala kubwa kabisa linaloathiri maisha ya watu, lakini halipewi umuhimu huo.
Swali langu kwa Dk Waziri: lini ataanza kuweka mikakati ya kupandisha thamani ya pesa yetu? Aanze kwa kufanya dola moja iwe tu = 2,000 kutoka Tshs. 2,549.60 hivi sasa. Watanzania wangeona mabadiliko makubwa sana ya maisha yao.