Ni lini serikali italipa salary arrears wanazodaiwa na vyuo vikuu?

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Hii serikali yetu tukufu wamekuwa wepesi sana kuhimiza wafanyakazi kutimiza wajibu wao ili kuleta tija kazini lakini serikali hiyo hiyo haitimizi wajibu wake kwa wafanyakazi.

Mosi. Imegoma kupandisha madaraja, vyeo na mishahara kwa mujibu wa sheria sasa inakaribia miaka miwili kwa visingizio vya uhakiki usio na mwisho wala tija.

Pili, Imegoma kulipa madai ya wafanyakazi ambayo ni pamoja a malimbikizo ya mishahara kwa muda mrefu kiasi kwamba deni limezidi kuwa kubwa.

Kwa mfano waalimu wa shule za msingi na sekondari wanadai sasa zaidi ya trillioni 1 na dalili za kulipa deni hilo wala
hazionekani.

Cha kusitisha zaidi waadhiri wa vyuo vikuu wanadai mslimbikizo yao ya mishahara i (salary arrears) tangu July 2015 mpaka leo hawajalipwa. Ikumbukwe hii ni sehemu ya mshahsra wa mtu ambao alilipwa pungufu ya alichostahili. Mwaka wa fedha 2015/2016 umekwisha... Kimya mwaka wa fedha 2016/2017 nao unaisha kimya! Maana yake nini?

Cha ajabu sasa, serikali inapandisha makato ya mkopo wa elimu ya juu kwa asilimia 15 na kuhimiza watu walipe huku wao setikali hawalipi madeni wanayodaiwa na wafanyakazi.

Mbaya zaidi tunaona pesa zinatumika katika mambo ambayo sio vipaumbele kwa sasa. Kwa mfano kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato, kununua ndege sita kwa pesa taslimu, kutoa pesa nyingi kwenye maeneo fulani huku maeneo mengine yakiwa hoi. Kuhamia Dodoma ghafla bila maandalizi yoyote nako kunasababisha yote haya

Mfano unatoa bilioni 12 kwa mkupuo kwa mahakama, na sehemu nyingine bils kuzingstia pia kuna sehemu nyingine nazo zinahitaji. Hspa zilipaswa zilitolewe kidogokidogo ili kupunguza makali katika maeneo muhimu pia mfano kwenye mafao ya wafanyakazi.

By the way, pesa zilizotokana nacwafanya kazi hewa, kubana ufujaji wa pesa za umma na kubana matumizi zimeenda wapi? Mbona hali inatoka from "worse to worst"? Mbona hatuoni faida za kuwabana mafisadi? Au mafisadi wenyewe walikuwa fake, propaganda za kisiasa?

Mbona hstuoni mabadiliko katika maisha yetu? Mbona hali sasa imekuwa mbaya kuliko kipindi cha "mafisadi" na "wapiga dili"?

Iweje serikali izibe mianya yote hiyo (ikimaanisha kwamba sasa serikali ina pesa za kutosha) lakini insdhindwa kulipa stahiki za wafanya kazi wake_? Kinyume chake inazidi kuwanyonga kwa kukata makato makubwa kwenye mishahara yao midogo?

Au tuseme kwamba serikali imeamua tu kuwatesa na kuwafanyia ubabe watumishi wake? Sasa kumbe tusemeje?
Saa Huu ni uungwana?

Watumishi wa umma tumeikosea nini serikali hii tukufu ya Ndugu JP Magufuli? Utafanikishaje kuifikisha nchi katika uchumi wa kati kama wale unaowategemea kulitekeleza hilo wana manung'uniko na masononeko moyoni?

Nilikuwa nawaza hivi. Ni kwa nini kwa mfano kwa sababu serikali inadai baadhi ya watumishi wake kupitia bodi ya mikopo na watumishi hao nao wanaidai serikali stahiki zao mbalimbali kwa nini hayo madeni serikali inadaiwa yssipelekwe kwenye bodi ya mikopo kupunguza madeni ili kelele za kuidai serikali zipungue na kuondoa hii kero ya kudaiana? Yaani kwa mtindo wa "punguza deni lako kwenye deni ninalokudai". Undava undava!

Anyway, ninachosema hapa ni kwamba kila upande utimize wajibu wake. Usitegemee tija kutoka kwa wafanyskazi wako huku ukiwanyanyasa kwa kuwanyima stahiki zao! Mwenye masikio na akili huko serikalini na asikie na kuelewa na kuyafanyia kazi haya!

La sivyo, mjue uvumilivu una mwisho!
 
Back
Top Bottom