Ni lini Rais atawaalika jopo la maskini

mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,434
5,535
Nimekuwa nikisikia viongozi wa juu haswa Rais JPM akijipambanua kila siku yuko kwa ajili ya watu masikini na wanyonge

Hili la wanyonge silisemei coz ni dhahiri huwezi kuwa mbabe then uwe mtetezi wa wanyonge

Tatizo lipo kwenye masikini coz naona wafadhili wanaoalikwa wanakuja na jopo la matajiri ili wabadilishane mawazo na matajiri wenzao

Kwanini hao wafadhili wasiongozane na jopo la maskini waje tujadiliane na sisi maskini tuone ni namna gani tunaweza kuuboresha umaskini wetu uwe wa kisasa uendane na sayansi na technology

Wito kama kweli JPM anayaishi maneno yako siku moja tuletee wafadhili waongozane na jopo la masikini tubadilishane umasikini wetu

Tumeona matajiri wakipendelewa sasa iwe zamu ya masikini

Kwaniaba ya maskini nawasilisha
 
Maskini umekosa kiungo gani cha mwili?? Pambana tofauti na hapo utakufa na umaskini wako!
 
Maskini umekosa kiungo gani cha mwili?? Pambana tofauti na hapo utakufa na umaskini wako!
Sijakosa kiungo ila nimekosa kiunganishi kama Bashite yeye kapata kiunganishi

Swali sisi masikini tunahitaji tupate fursa ya kukutana na masikini wenzetu mfano masikini wa USA au Morocco wanakuja tunajadili umasikini wetu

Wewe mbona jopo la matajiri wanakuja ila hujawai itwa au kuhudhuria then unatuzarau masikini
 
Kweli aiseee umesema wazo la sekondari sana, rais wa masikini wanyonge ila hajawahi hata siku moja kualika wanyonge na masikini wajumuike pamoja!
 
Kweli aiseee umesema wazo la sekondari sana, rais wa masikini wanyonge ila hajawahi hata siku moja kualika wanyonge na masikini wajumuike pamoja!
Ni masikitiko kaja mfalme wa Morocco na jopo la matajiri sijui wa china kaja na jopo la matajiri wa Ethiopia hivyo hivyo

Hata sisi masikini tunataka kujadiliana na masikini wenzetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom