Ni lini Magufuli ataacha kumsifia Kikwete?

Ni lini Magufuli ataacha kumsifia Kikwete?

mululu

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2014
Posts
756
Reaction score
408
Wandugu,

Nimekuwa namfuatilia sana huyu mgombea urais wa CCM, ndg Pombe Magufuli, anapokuwa jukwaani anatumia muda mwingi sana kumsifu Kikwete kuliko yeye mwenyewe kujipambanua atafanya nini.Sio siri mimi huyu jamaa sijawahi kusikia hotuba yake isiyo na jina Kikwete.

Magufuli mpaka sasa hajajua huyo anayemsifu ndiye katufikisha hapa pabovu tulipo? Wewe tumia muda wako kumsifu huyo boss wako utakuja kustuka imekula kwako, utakuwa loyal kwa jamaa mpaka lini?

Mwanzo mimi nilijua unamfurahisha ili akuteue kuwa mgombea, sasa si tayari umeshateuliwa mbona bado unazidi kummwagia jamaa masifa? Ina Maana kweli wewe huna cha kusema chako?

Ushauri wangu usimsifie sana maana yake mwisho wa siku asije akaona unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa...
 
Amezidi sana... Hadi kero utafikiri anamwombea kura.!
 
Huyu mtu alikuwa hakujipanga hata kidogo, maneno yake tangu achaguliwe ni SITAWAANGUSHA! Sijui kama kwa dhati anajua matatizo makuu yanayowasumbua watz kwa sasa, wananchi wanahitaji kiongozi wa ngazi yoyote, udiwani, ubunge na uraisi aeleze in details matatizo ya nchi na ni kwa namna gani kwa kushirikiana na viongozi wenzake na sisi watz tutayatatua na kujiletea maendeleo kwa kutumia raslimali lukuki zilizopo nchini, huyu ndio kiongozi tunayemtaka, sio kuishia kusema SITAWAANGUSHA! Nilishawahi kusema kuwa msimamizi mzuri wa barabara haimpi uhalali mtu kuwa raisi na kiongozi mzuri, kwa mtazamo wangu watu wengine wanaweza kufanya vizuri kama wako chini ya kiongozi fulani, na hili linaweza kuwa kosa KUBWA kufanywa na sisiem mwaka huu.
 
Awe makini sana Dr.Magufuli,asijiamini kupita kiasi.Ngoja kipenga cha kampeni kipulizwe.Tunataka wagombea watwambie nitafanya hiki na kile siyo kushambuliana tu
 
Wenda vile bado ni shughuli za ndani ya chama na za kiserikali, so inabidi amsifie m/kiti wake na mkuu wake wa kazi respectively.
 
sasa hivi wanachofafanya ni mchezo wa kusifiana wakifika sehemu jk anamsifia alcohol na alcohol anamsifia jk yana wanajitekenya na kucheka wenyewe!

Kama taasisi na hapo ndio wanapowafanya wale waliopita awamu zingine kama vile hawajafanya kazi wakati kama chama ambacho ni taasisi kisionyeshe mbele ya kadamnasi kwamba awamu zingine wajenga vivuko 13 alafu JK peke yake kajenga vivuko 13, kama kila mtu angekuwa na timu yake ya ufundi anaorodhesha vitu alivyovifanya kwenye awamu yake lazima tungepata sehemu zingine ambazo na yeye wangemlinganisha.

Washukuru tu kwamba kwenye chama chao hakuna migogoro mikubwa ya wazi ya kitendaji na kisiasa baina ya wakongwe ndani serikali na chama na kizazi kiya otherwise yangezuka makundi ndani ya serikali yao sikivu nadhani yangeitwa timu COMPARE AND CONTRAST.
 
Leo asubuhi wakati wa mapitio ya magazeti ilibidi nicheke, vichwa vya habari vimejaa, Magufuli amsifu Kikwete' linalofuata 'Kikwete ampongeza Magufuli', yaani wamebaki kupongezana wao kwa wao.

Mkuu mululu Magufuli hakutegemea kupata hiyo nafasi hivyo anafanya kila njia kumsifia anayedhani kamfikisha hapo.
 
Last edited by a moderator:
Bwana mmoja mwenye shamba alipanda viaziii akachimbachimba akaona alimasiii looo looo bahahatii looo looo bahaaahaatii ya mtu nwenye shamba.....
 
Pombe hajajua kama yeye ndio mwenyekiti wa ccm.Anategemea Kikwete amtume kazi za kufanya.

Tatizo la magufuli ni kuwa hupenda sana kujikomba kwa yule aliyemteua, hata kipindi cha Mkapa alikuwa akimsifia sana Mr Clean iwe ni bungeni au sehemu yoyote atakayotoa hotuba. Na ukumbuke Magufuli ndio chaguo la Mkapa katika kinyang'anyiro cha Urais.
 
Hawezi kuacha kumisifia kwasababu anamtegea sana amsaidiki katika mipango ya kuiba kura. kwa sasa Pombe anamtegemea sana baba na mama salma kuliko mungu
 
Huyu jamaa kugombea urais alikuwa anashtua tu,Mara tiiiiiii,yumo!Naona hajajiandaa na hajui asimamie nini!Hafai kuwa rais
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom