Ni lini Magufuli ataacha kumsifia Kikwete?

Ni lini Magufuli ataacha kumsifia Kikwete?

Tatizo la Makufuli ni "Kukariri"

Jamaa amekariri mambo ya miaka ya 2005 kuwa JK anapendwa sana na Watanzania. Kumbe kwa sasa ukichukua watu 3 maarufu wanaochukiwa na Watanzania JK ni mmoja wapo.

Kukariri kubaya.
 
Huyo CCM wamemuonea kumpa hiyo nafasi ya kupeperusha bendera kwenye uchaguzi. Alistahili kufanywa mkuu wa kitengo cha takwimu. Ili hata kama umeme hakuna na mtu huwezi pata data za haraka unamtwangia simu tuu,
Mpiga simu; Bwana Pombe hivi ni umbali gani kutoka Mtwara hadi Bukoba kupitia Nzega?
Pombe; Hapo ni kilometa elfu moja mia nane ishirini na tatu nukta sita tisa point saba moja, ila kupitia Arusha utapunguza umabali huo kwa kilometa mia moja ishirini na sita nukta tatu nne point moja nane. Ila hapo kuna mchanganyiko wa kiwango cha lami na kiwango cha changarawe kwa tofauti ya kilometa ....................
Hapo bwana Pombe ndio angetumika kwa faida.
 
mululu

Yaani ndugu mululu umeelezea barabara kabisa.Oyee nyingiii na kumsifia Kikwete Magufuli anashindwa hata kujipambanua mwenyewe kutwa kumsifia Jk.Wananchi hawana imani ,wamechoka,wameumia na Kikwete na akiligundua hilo ataacha mara moja hizi sofa uchwara.Sijui anamdanganya nani??sijui sifa hizi zitamsaidia nini hata akishinda huu uchaguzi.Huu ni Uhuni tu wakutekenyana na kucheka wote.Na kwa taarifa yao oktoba tunamchagua Lowassa.
Kwisha habari.
 
Last edited by a moderator:
Muda Mrefu Magufuli Amekuwa Akimsifu Kikwete Na CCM Kwa Kusema Hajui Kama Rais Anayekuja Atafikia Viwango Vya Kikwete.Anakera Sana.Kila Neno Kibwagizo Ni Kikwete!
 
....ndio uje uone aina ya viongozi wetu TZ..alafu huyu magufuli ndio wanataka aje awe rais??...kwamba kwa kuwa anapewa cheo na mkuu wake basi lazima amfagilie!!kwamba cheo kinatolewa kama pande..ama msaada kwa mtu...ndio maana anamsifia boss wake kila mara...huu unafiki hauna kipimo..na hivi amepitiswa kuwa mgombea urais wa ccm ndio kabisaa anaona amepewa uhai wa pili...utashangaa povu linavyomtoka kwa sifa kwa boss wake..

...ni pale tu mwenye njaa na shida apewapo msaada kujaza tumbo lake ndipo ni kawaida kumwaga misifa kwa amlishae ....inashangaza basi kumwona anaejiita msomi (dr)kumwaga sifa kedekede kwa boss wake ahata pale pasipodhaniwa...je anawezaje kutufanya tuamini kuwa hasemi asante kwa kupewa ulaji??....inasikitisha sana...
..nchi hii hakika inahitaji mageuzi makubwa....aina ya viongozi kama magufuli wanaofannya kazi kuwaridhisha wanaowapa vyeo hawaitajiki TZ ya leo...maana ndio waliotufikisha tulipo kama taifa lenye mkwamo...yani magufuli amekua kama kipofu alieona nyota...
 
Umoja na Mshikamano ndani ya CCM unatokana na kila mtu kumjua mwenzake vilivyo. Huyo kaiba hiki na yule kapora hiki. Ufisadi huu ni wa fulani n.k. Hali hiyo inawafanya wabaki wakisifiana na kupongezana. Hii ndiyo thinking ya JK kwamba hata akiwakata apendavyo mambo yatapoa tu kumbe hakufikiria nje ya Box. Kwa uhakika EL ataidhalilisha CCM sana katika uchaguzi unaokuja

Magofuli hawezi kushindana na El hata kwa haiba ya kawaida, Mvuto na utendaji kazi, EL anamzidi sana JPM
 
Kaka swali lako zuri sana siku magufuli akijitambua ataacha, niseme kuwa Magufuli ni kama wale watoto ambao hawataki kuondoka kwa baba na Mama kwenda kujitegemea siku zote wao hulia lia tu home.
 
watwambie ktk kipindi cha JK deni la taifa limefika kiasi gan? na litalipwaje? sio porojo...Watz tumechoka na kutufanya wajinga mda mrf..
 
kuna jamaa mmoja kasema huyu jamaa wakimuaja peke yake bila wana saikolojia unaweza ukasikia kesho naye kahamia UKAWA,ndio mgombea wakwanza duniani asiye na vipaumbele,maanake yeye hawezi kujiongoza anasubiri kuongozwa
 
Wakulima Sitawaangusha!Wafanyakazi Sitawaangusha!Bodaboda Sutawaangusha!Wafugaji Sitawaangusha! Wasanii Sitawaangusha!Wafanyabiashara Sitawaangusha! Wanafunzi Sitawaangusha!Wanawake Sitawaangusha!Vijana Sitawaangusha! Mh. Kikwete Sitamwangusha!Ukawa Sitawaangusha!
Nichagueni Sitawaangusha!
Asanteni kwa kunisikiliza hamjaniangusha!
Ccm Oyee! Kikwete Oyee!
 
Jamani, wewe ungefanyaje kuonyesha shukrani kwa mtu aliyelala na jina lako mfukoni kukupeleka NEC na hata kugeuza namba za kina mama kuwa kiduchu kwa ajili yako wewe? Acha aendelee kumsifia bwana wake wala msimunee wivu. Akiangukia pua ndio ataacha
 
Wakulima Sitawaangusha!Wafanyakazi Sitawaangusha!Bodaboda Sutawaangusha!Wafugaji Sitawaangusha! Wasanii Sitawaangusha!Wafanyabiashara Sitawaangusha! Wanafunzi Sitawaangusha!Wanawake Sitawaangusha!Vijana Sitawaangusha! Mh. Kikwete Sitamwangusha!Ukawa Sitawaangusha!
Nichagueni Sitawaangusha!
Asanteni kwa kunisikiliza hamjaniangusha!
Ccm Oyee! Kikwete Oyee!

teh teh teh, magufuliii... aliulizwa nn kipaumbele chako? akajibu nasubiri ilani ya chama changu, daaah hatufai hata kdogo
 
Awe makini sana Dr.Magufuli,asijiamini kupita kiasi.Ngoja kipenga cha kampeni kipulizwe.Tunataka wagombea watwambie nitafanya hiki na kile siyo kushambuliana tu

Wewe umenena kweli kwani kampeni hazijaanza. Kinachoendelea sasa ni kujenga imani ya wananchi kwa kuwakumbusha ni nini utawala chini ya Kikwete umeweza kufanya. Na UKAWA nao wana mnadi Lowasa kama mkombozi na upambe mkubwa.
 
Bado anaimba "Hadi mselema, hadijaa. Kikwete selema..."?
 
Hana cha kuongea au kutuahidi wananchi zaidi ya kumsifia jk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom