Ni lini Magufuli ataacha kumsifia Kikwete?

Ni lini Magufuli ataacha kumsifia Kikwete?

hadi anakera, kauli zake ni tatu tu kila anapofanya mkutano.



1. ....hivi watanzania nimeshawahi kuwaangusha kweli........ (anataka watu wamwonee huruma)
2. ....yani kwa kweli mimi mkinichagua nitatekeleza ilani ya chama chetu kuwaletea maendeleo ya kweli......
3......namshukuru sana mweshimiwa Rais Jakaya kuifikisha nchi hapa ilipo, namshukurus sana tena sana, nafikisha pongezi zangu za dhati kwake, tena na yeye yupo hapa ananisikia.......

Atakapokuwa rais ataacha tu
 
Atakapokuwa rais ataacha tu

Ni kweli hajawahi kutuangusha watanzania katika majukumu aliyokabidhiwa na marais waliopita. Sio kama Lowassa aliyetuangusha katika uwaziri mkuu katika miaka miwili tu akaanza kufakamia rushwa na kutumia mamlaka yake vibaya. Magufuli ni jembe la ukweli. Linapiga mzigo na kuz....ka mar....hemu.
 
25 October 2015 UKAWA tukiwa pale magogoni.
Hatamsifia sababu 1 atakuwa Chato na mwingine atakuwa Msoga analima Mananasi.
 
Magufuli akipata URAIS ni dhahiri atakuwa ni muendelezo wa JK na sera mbovu za chama tawala.
 
Magufuli akipata URAIS ni dhahiri atakuwa ni muendelezo wa JK na sera mbovu za chama tawala.

Lowassa ndio hana jipya kabisa

Alipokuwa kampeni meneja wa JK alituambia maisha bora kwa kila mtz ss anatuhadaa anataka tuwe matajiri kama bakhresa . Asaeme kwanza wamasai mbona bado wanajifunga mashuka machafu kiashiri a cha kwamba umaskini umekithiri kiasi cha kukosa sabuni ya kufulia. Sishangai kwa sababu its vety well known kuwa Lowassa ni tapeli la kitaifa la kisiasa
Potelea mbali FISADI
 
25 October 2015 UKAWA tukiwa pale magogoni.
Hatamsifia sababu 1 atakuwa Chato na mwingine atakuwa Msoga analima Mananasi.

Magogoni polini mnachoma mkaa. Watanzania hawawezi kuwapa wahuni Ikulu
 
akiwa waziri alikuwa anapewa statistics za Tanroads, kazi yake ilikuwa kujaza kichwani mwake na kumwaga hizo figures bungeni. sasa hakuna hizo data za kujaza kichwani kabakia na sitawaangusha
 
Mkuu umesema kweli Magufuli anajipendekeza sana kwa Kikwete yaani hadi kero.
 
nafikili ataacha pale tu atakapohamia ukawa, maana ata lowasa alikua akimsifia kikwete lakini aliacha alipohamia ukawa
 
2005 US$=Tshs:420/=,2015 US$1=2300/= Haya ndo maendeleo aloleta jk na jpm anayasifia na kutoyaangusha.
Watanzania kuweni makini kupita wakati mwingine wowote wa uhai wa Taifa letu,tusirudie ya 2005 kamwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom