Ni lazima wote watoe sababu

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
NI LAZIMA WASEME NA WATOE SABABU

Niwape mfano wa Simba na Yanga wakiwa na mchezo wa mpira, kuna majibu ya ya aina tatu yanaweza kutokea kwa timu yoyote kati ya hizo. Kushinda, kushindwa au kutoka suluhu.

Ikatokea Simba wameshinda, watu wanakuwa na sababu za kutosha ni kwanini wameshinda, na zitakuwa sababu nzuri sana. Na hata ikatokea simba wameshindwa, watu watakuwa na sababu kwa nini wameshindwa, na zitakuwa sababu za ukweli sana. Timu ile ile kwenye mchezo ule ule lakini kushinda au kushindwa kote watu wanakuwa na sababu.

Hivyo ndivyo ilivyo kwenye maisha yako pia.

Unapochagua kufanya jambo kubwa, jambo ambalo wengine hawajawahi kufanya, utakaposhinda kuna wengi watakuwa na sababu nzuri kwa nini umeshindwa. Tulijua, hiki kilimsaidia na mengine mengi.

Lakini pia kwenye jambo hilo hilo ikatokea umeshindwa, watu watakuwa na sababu kwanini umeshindwa.

Tulimwambia, asingeweza hili na mengine mengi.

Ufanye nini?

Fanya kile unachotaka kufanya, pigania kile unachoamini, na ikitokea umeshindwa na watu wanakusema, jua hata ungeshinda bado wangesema.

Pia ikitokea umeshinda na watu wanakupongeza, jua kama ungeshindwa wangekusema.

Chochote unachofanya, fanya kwasababu ndio unachoamini na ndio hasa unachotaka, usifanye kwa kuangalia watu wanasema nini.

Watakupotosha na utashindwa kuwa na maisha bora kwako.
 
Back
Top Bottom