Ni laana kwa utamaduni wa makabila mengi hapa TANZANIA kula rambirambi...

mndorwe

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
2,472
1,027
Leo nilikuwepo sokoni sadala nauza nyanya jamaa mmoja akaniambia ukiona mtu anakula rambirambi ujue kuna kitu anataka na atakipata.

Kwa utamaduni wa watu wa hapa Hai mkoani kilimanjaro, watu wengi wanaogopa kula rambirambi. Hata chakula cha msibani huruhusiwi kubeba nyumbani kwako tunaamini kuwa ukibeba chakula cha rambirambi hadi nyumbani kwako unataka na wewe upate msiba kwako.

Hivi hii ikoje kwa makabila mengine hapa Tanzania. Je wanaruhusiwa kula rambirambi?
 
Kama watu wanaweza kuua, wataogopa rambi rambi ? Kama hawaogopi hukumu unafikiri wataogopa laana?
Sikio la kufa.
 
Kuna mtu alitumia rambirambi kulipia ada ya mwanawe , hakika nakuambia , pamoja na akili nyingi za yule dogo lakini alifeli vibaya sana !

Kutafuna rambirambi ni laana isiyo na msamaha .
 
Unaongea kama umetokea Mars bana,siku hizi rambirambi zinapigwa,chakula kinabebwa,na mfiwa anadai rambirambi tena kwa kukumbusha kabisa eti msiba wa fulani nilitoa kadhaa,mbona mie sijapewa?
 
Kuna mtu alitumia rambirambi kulipia ada ya mwanawe , hakika nakuambia , pamoja na akili nyingi za yule dogo lakini alifeli vibaya sana !

Kutafuna rambirambi ni laana isiyo na msamaha .

Huyo jamaa alitia fora aisee

Badala ya dogo kufau
Anaenda kufeli mpaka anaptiliza

Ndo maana,walisema choz la
Mfiwa halitadondoka bure
 
Si shangai rambi rambi kuliwa
Ila maana ishazoeleka

Ila nashangaa
Mtu kubeba chakula

Cha msiban kupeleka
Kwenu huyo atakua
Alishalaaniwa kitambo
Na,shetan
 
Serikali imegoma kupokea misaada kutoka kutoka nchi wahisani na pato la ndani halitoshelezi mahitaji
Na alieshika mpini ndo mchangisha rambirambi unategemea nini hapo?
 
Kuna kaukweli fulani. Tangu Simba Sports Club watafune rambirambi ya Mafisango ubingwa ligi kuu imekuwa ndoto kwao!
 
Leo nilikuwepo sokoni sadala nauza nyanya jamaa mmoja akaniambia ukiona mtu anakula rambirambi ujue kuna kitu anataka na takipata.Kwa utamaduni wa watu wahapa Hai mkoani kilimanjaro, watu wengi wanaogopa kula rambirambi....hata chakula cha msibani huruhusiwi kubeba nyumbani kwako tunaamini kuwa ukibeba chakula cha rambirambi hadi nyumbani kwako unataka na wewe upate msiba kwako.....Hiv hii ikoje kwa makabila mengine hapa Tanzania je wanaruhusiwa kula rambirambi?
Hukuwaeleza vixuri. Kuna chakula cha msiba, kila mwanakijiji analeta (ugali, waki, makande, mihogo) wanakula waombolezaju wote wala hakibaki; kwa hiyo swali la kula rambirambi si kweli, kilichopo ni chakula kinacholetwa na kila mwanakijiji.

Pia kuna rambirambi, michango ya mtu na mtu kuwasaidia wafiwa. Hii kamwe huwa si chakula, ni hela, anapewa mwanafamilia. Kuna zingine huingizwa kwenye daftari, zingine hupewa mhusika kadiri mtoaji anavyoguswa. Hutangazwa na mtemi au na Mzee wa Kijiji, wala haitangazwi na diwani. Matanga yakishafungwa yamefungwa; hayarudiwi tena na Meya, kwanza kwenye msiba hatuna siasa.

Hiyo ndiyo makabila mengine tangu Meru hadi Nzega. Unaonaje?
Kama watu wanaweza kuua, wataogopa rambi rambi ? Kama hawaogopi hukumu unafikiri wataogopa laana?
Sikio la kufa.
 
Serikali imegoma kupokea misaada kutoka kutoka nchi wahisani na pato la ndani halitoshelezi mahitaji
Na alieshika mpini ndo mchangisha rambirambi unategemea nini hapo?
Masahihisho - Nchi kapuku kama ilivyo Tanzania haijawahi kugoma kupokea msaada ( rejea kauli ya kuomba Zuma ajenge reli ), Bali ni ukweli ulio wazi kwamba Tanzania IMENYIMWA MISAADA NA KUTIMULIWA KWENYE MCC KWA KUMPORA USHINDI MAALIM SEIF HUKU IKITUMIA SILAHA ZA KIVITA VIKIWEMO VIFARU .
 
Kula rambirambi ni laana, laana, laana! Kuna jamaa yetu mmoja alitumwa pesa za rambirambi akazila. Hakumaliza miaka mitatu akafa.
 
Huwa nasikia huko hawaogopi kuua ili kupora duka akatajirike, sasa iweje waogope kubeba ubwabwa au kula rambirambi?
 
Back
Top Bottom