Ni kweli yametokea..!!

SALOK

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
3,308
1,924
Amini usiamini ndugu mtanzania haya yametokea leo tarehe 09 april 2012 ktk hospitali ya wilaya tandahimba, kuna ndugu yangu alimpeleka mwanae, kwa kudra zake manani alipata huduma, mwanae alipatiwa vipimo akagundulika na malaria akaandikiwa dawa 'mseto' alipoenda dirishani kuchukua dawa akaambiwa akanunue dukani, alipofika duka lilokaribu na hospitali akaambiwa amsubiri mwenye duka kaenda hospitali kuchukua dawa. Baada ya muda kidogo akatokea akiwa na box lenye dawa. Hizi ndio hospital zetu. Je tutafika?
 
Hivi hali hii mpaka lini? yaani madaktari wanathubutu kuuza dawa tena wazi wazi namna hii, unaambiwa hospitali hamna dawa kanunue dukani, unafika dukani unauziwa dawa zile zile za hospitali tena bila kificho..!! inauma sana! Hii Nchi hii..??
 
Sijui ni nani wa kumfunga paka kengele, wala hata simjui paka mwenyewe ni yupi!!
 
tutafika tu.....ila wangapi watafika ndo issue....
Ila kosa ni lao hao wanaoteseka kwa kuwa wao ndo wanakataa kuleta mabadiliko ya nchi hii....so wacha jamaa wajisevie na wajilimbikizie maendeleo na sisi wanonge tunaowatukuza wacha tuendelee kula joto ya jiwe
 
ila kosa ni lao hao wanaoteseka kwa kuwa wao ndo wanakataa kuleta mabadiliko ya nchi hii....so wacha jamaa wajisevie na wajilimbikizie maendeleo na sisi wanonge tunaowatukuza wacha tuendelee kula joto ya jiwe

erick laiti ungelijua hali ya kisiasa ya t/mba usingesema hayo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom