Ninajua kuwa wananchi hao NY wengi walitumiwa E-mails za kualikwa na kuambiwa kuwa watoe maswali yao in advance na kuyapeleka ubalozini mapema, at least a week before,
sasa kama kawaida yetu wabongo, kuna waliorukia kimbele mbele na kutuma maswali, sasa kilichofanyika ni watu wa JK, kuyakusanya na kuchambua yaliyorudiwa kwa wingi na kuyaita kuwa ndiyo kero ya wananchi wa NY, kwa hiyo hotuba nzima ya rais ilitenngenezwa kwa kutumia maswali hayo, na hii ikampa advantage rais ya kugusa issue muhimu kwa juu juu, halafu yalipokuja maswali kugusa hizo issue akasema kuwa hawezi kurudia tena aliyokwisha yasema,
wananchi wa NY, walipaswa kujibu na kuujibu ubalozi kuwa watauliza maswali pale pale uwanjani sio kutuma kabla kama bungeni, maana hata bungeni kuna maswali ya nyongeza, but psychologically, kuwaambia wananchi watume maswali mapema ilikuwa ni mbinu ya kuwatisha pia na wote mliokuwepo mmeona results,
Yes, kuna kijana aliyeuliza swali la mwisho ambaye aliitwa ndani nakuonana na JK, usoi uso kwani pamoja na mengine kile kitendo cha kumuita Bwana Rais, hakikukubalika, anyway sijui kama kuna waliotishwa as kutishwa kabla ya mkutano!