Ni kweli tumefikia hapa..??

Ni kweli tumefikia hapa..??

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2010
Posts
7,991
Reaction score
5,234
Jana nilimtembelea dada yangu,katika kuongea na binti yake wa miaka 8 aliye darasa la tatu nikamuuliza ili kumpima uelewa wake katika somo la maarifa ya jamii.Nitajie maadui watatu wa Taifa,nilitegemea jibu liwe umaskini ujinga na maradhi.Cha kushangaza katika kujibu mtoto huyo alianza kwa kusema adui wa kwanza niiii Kikweteeee,wa pili niiii,ikanibidi nimuwahi asiendelee na kumrekebisha.Sasa najiuliza kama mtoto wa miaka minane anaweza kukujibu hivyo hali ikoje kwa vijana..?? Hebu nisaidieni jamani nanyi katika jamii zenu ili kuwajua maadui wa Taifa kwa sasa...
 
Mtakavitu... ndio hivyo ujue tumefika hapo sasa, lakujiuliza tutatokaje hapo na kuendelea mbeleni....? au sio St. Paka Mweusi?
 
Last edited by a moderator:
kipindi hichi, watoto na vijana wa dogo wanajua mengi ambayo pengine watu wazima hawayajui... sasa la kushangaza watawala wanatuona mapoyoyo kabisa....!
Uko sahihi kabisa ila kilichonishtua ni kuona watoto wamefikia kumuona mkuu wa nchi ndio adui,mawazo hayo wanayatoa wapi,ni nani anayewafundisha,na je vijana wanaoingia rika la kupiga kura nao watakuwa na mawazo ya aina gani..?? Au ndio ile hadithi ya mchimba kaburi kaingia mwenyewe inataka kuleta uhalisia..??
 
St. Paka Mweusi awali nikupe heri ya mwaka mpya.

Tuje kwa huyo mtoto wenu, hapa unaona inavyokuwa mbaya
kupanda chuki kwa vizazi vijavyo.

Ungeenda mbele kidogo umuulize kama anamjua aliyemtaja ni nani,
pia ungedokoa kidogo kilichomfanya aseme hivyo.

( n.o.o .......... Ingekuwa hivyo kweli mbona upo una maisha mazuri tu huko uliko;
kwani original yako si ni hapo hapo alipo huyo mtoto wenu)
 
Nashukuru mama heri na wewe,ila ndio watoto wetu hawa hata sijui tuwafanyeje....Nilishindwa kuendelea sababu ya kuogopa kusikia makubwa zaidi mama.....
 
Back
Top Bottom