Ni kweli taifa letu limepata upendeleo wa kipekee kutoka kwa Mungu tofauti na mataifa mengine Afrika au ni fikra potofu?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,597
46,244
Wabongo tuache kujipumbaza kwamba sisi ni taifa special sana linalotazamwa na Mungu kipekee ndio maana tumekuwa na rasilimali nyingi, maziwa, mito, bahari, hali ya hewa nzuri n.k. Mataifa yote unayoyaona Afrika leo ni zao la mkutano wa Berlin wa mwaka 1884/1885 wakoloni wenye nguvu(mabeberu) walipojisevia ardhi zetu kama mlo wa mchana na sisi tukaendelea na urithi huo baada ya uhuru. Ni mataifa machache sana Kama Sudan ya kusini, Somalia na Ethiopia ambayo hayakupitia utaratibu huo.

Hutajapendelewa na Mungu kuwa na utulivu wa muda mrefu kupitia chama kimoja tawala tofauti na mataifa mengi ya Afrika. Chama tawala kimekuwa kuanzia TANU mpaka CCM ya sasa kimekuwa na weledi mkubwa sana katika kuyaleta makundi mbalimbali ya kijamii chini ya himaya yake kwa ushawishi wa kimaslahi zaidi kuliko kutumia dola ndio maana kipo imara madarakani kwa miongo yote hiyo, hakuna muujiza wa kiMungu katika hilo.

Wengine wanafika mbali katika kujifariji huku na kudai hata kuna mabadiliko makubwa yametokea ili Mungu kulisaidia taifa hili! Kama hilo ni kweli kwa nini mabadiliko hayo yasitokee huko kwingine dunia ambapo wanayahitaji zaidi kuliko sisi tena kwa miongo mingi?
 
Na huko kwingine yanatokea Kwa namna tofaut , na huwez kujua ...... We tambua Tu mwenendo wa Taifa lako basi..... kuna wakati Yesu alimwambia Petro mambo yake ya mbele na atakufaje , pembeni yake alikuwepo kijana mdogo Yohana, Petro akataka kujua ya Yohana naye itakuwaje , Yesu akamwambia hayo ya huyo hayakuhusu wewe jali ya kwako na nifate Mimi......
 
Na huko kwingine yanatokea Kwa namna tofaut , na huwez kujua ...... We tambua Tu mwenendo wa Taifa lako basi..... kuna wakati Yesu alimwambia Petro mambo yake ya mbele na atakufaje , pembeni yake alikuwepo kijana mdogo Yohana, Petro akataka kujua ya Yohana naye itakuwaje , Yesu akamwambia hayo ya huyo hayakuhusu wewe jali ya kwako na nifate Mimi......
....Utakapokuwa mzee watakufunga na kukupeleka usipopataka.
....Ikiwa nataka huyu aishi milele yakupasani wewe?
 
Wabongo tuache kujipumbaza kwamba sisi ni taifa special sana linalotazamwa na Mungu kipekee ndio maana tumekuwa na rasilimali nyingi, maziwa, mito, bahari, hali ya hewa nzuri n.k...
Mungu anawapenda watu wote Sawa,ilimradi ufate taratibu zake,kusema Mungu anatupenda sana bongo kuriko anavyoipenda UK,USA,ni ujinga kabisa, umaskini wote huu, mbona hajatupa utajiri kama wao?
 
Israel tuu, wao ndiyo wameruhusiwa kuwakalia kimabavu waarabu kuwauwa na kuwanyanganya ardhi zao....,,,,,
 
Wahindu wekundu kule USA walilaaniwa?
Babu zetu waliopelekwa utumwani?
 
Back
Top Bottom