Huko vituko vya kichawi, vipi sana, ni katikati ya mwaka jana tu, afisa mtendaji, alilala ndani kwake, asbuhi, akajikuta amelala nje ya nyumba yeye na familia yake.
Mbaya zaidi, wote wamelala uchi wa mnyama.
Uchawi sio kama majani polini, eti ukienda tu huko, basi uone wazi wazi, vitendo vya kichawi, kwanza wachawi, katika mazingira ya kawaida, ni watu wema huwezi dhani. Ila ndugu yangu hata ukisikia samaki baharini, sio ukienda tu baharini, basi utawaona wanaogelea tu, la hasha, ila ni kweli samaki wapo baharini na ndipo makazi yao.