Ni kweli Sumbawanga kuna uchawi?

Ni kweli Sumbawanga kuna uchawi?

nipo sumbawanga mitaa ya sumbawanga imepangika kuliko Mbeya karibu huku mkuu kizwite, Bible, chanji, majengo, kristo mfalme, sumbawanga asilia, bomani, katuma, mkoani,katandala, majumba sita. Welcome sumbawanga hukumambo ya uchawi hayapo ila zamani yalikuwepo
 
Salam kwenu wanaJF
Sumbawanga ni wilaya ya mkoa wa Rukwa nilianza kuisikia kwa sifa nyingi zisizo nzuri na zilikuwa za uchawi tangu nikiwa mtoto nakumbuka nilipokuwa primary shule moja mkoani dodoma kulikuwa na mwalimu wetu alikuwa wa sumbawanga na alikuwa akilima anapata sana tofauti na wenyeji na wale wezi wa mazao walikuwa wakiiba tu wanabeba wanajikuta wamepeleka kwake..
Nilizidi kuamini kuwa sumbawanga ni wachawi sana sanaa.. Na mikoa mingi ukitembea unakutana na matangazo ya waganga wa jadi kutoka sumbawanga hii ni kuonesha ni kwa namna gani watu wa kule ni kiboko kwa mambo hayo..

Leo ni siku ya sita nipo sumbawanga na nilipoambiwa nije huku kwa shughuli za kikazi kwa muda wa siku 14 niliogopa kidogo lakini kiukweli kabisa sijaona la kutisha maisha yanaenda na naona kunaendelea pia sioni matangazo ya waganga ila nimekutana na matangazo kadhaa kwenye miti na nguzo yameandikwa FREEMANSONS UKITAKA KUJIUNGA PIGA NAMBA .. sasa nikajiuliza inamaana zile story za uchawi ni kweli au sio kweli?? Wenyeji wamesema wachawi wamehamia vijijini hapa mjini wengi ni wageni na wamestaarabika kidogo lakini nimepewa onyo kwamba usitembee na mzawa wa huku unaweza usirudi kwenu na ukitembea nao usiwaahidi ambacho huwez kumtimizia..

Mazingira yako poah barabara ni nzuri kutoka mbeya kwa private car kukutumia masaa matano..
Pia naona kama wamejenga vizuri tofauti na mbeya huku mitaa imetenganishwa na barabara na panaonekana vizuri tofauti na ukisimuliwa au vile unavuta picha ukitajiwa jina sumbawanga.
Wasiwasi wangu umeniisha.. Waungwana msiogope kwenda ikibidi nimeambiwa fursa nzuri ni kilimo zaidi ..
1.Kimsingi concept ya freemanson kwa Tanzania inachukuliwa kama ni wachawi au watu wenye uwezo wa kupata fedha kimiujiza

2. Jambo hili limekuwa likienezwa na baadhi ya vijarida vya kizushi pamoja na baadhi ya dini wasiojua ukweli juu ya hili ikitumika kama ngao ya kutisha watu

3. Ukweli ni kwamba freemanson kilikuwa ni chama cha wajenzi walalahoi waliokuwa wanateseka kwenye kazi zao na wakaunganisha nguvu pamoja wakaja kuwa na uwezo mkubwa kiuchumi na kiushawishi

3. Baadhi ya waganga matapeli na hao wenye vijarida wametengeneza illusssion hasa kwa watu wa vijijini ukipata maendeleo ya gafla wanakuita freemason, ukiwa serious na mambo yako wanakuita freemason

4. Huu ujinga umeenea miji mingi kwa matapeli hayo kubandika mabango na kuweka namba zao za simu ili kutapeli watu.

5.Ninasihi mamlaka za miji kutumia sheria zao ndogondogo (by laws) kuwakamata kwa kuweka mabango ambayo kwanza yanachafua miji na hayajathibitishwa na mamlaka husika
 
nipo sumbawanga mitaa ya sumbawanga imepangika kuliko Mbeya karibu huku mkuu kizwite, Bible, chanji, majengo, kristo mfalme, sumbawanga asilia, bomani, katuma, mkoani,katandala, majumba sita. Welcome sumbawanga hukumambo ya uchawi hayapo ila zamani yalikuwepo
Shukrani sana mkuu
 
Mamlaka ya miji wamekusikia
 
nipo sumbawanga mitaa ya sumbawanga imepangika kuliko Mbeya karibu huku mkuu kizwite, Bible, chanji, majengo, kristo mfalme, sumbawanga asilia, bomani, katuma, mkoani,katandala, majumba sita. Welcome sumbawanga hukumambo ya uchawi hayapo ila zamani yalikuwepo
Karbu majengo special Apa me Npo rafiki karibu na kanisa LA nazareti
 
Uchawi watu wameupa kiki ili kutufanya tuishi kwa uoga..
Lkn uchawi uliopo ni kama ule wa nazingaombwe tu hakuna uchawi mkali wa kumfanya mtu apotee au abadilike kuwa kuku..

Mengine ni utapeli na kutishana tu..

NB:anaebisha namuomba aniroge huko alipo kesho nijikute nimelala mitaloni ndo ntaamini uchawi upo kweli
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hadithi tu ilikua,

Mkuu karibu Chanji tupige zetu kilaji kufukuza baridi hii.
 
Wachawi wapo Tena wengi.tongoza mdada mfipa halafu uone chale toka kifuani mpaka kunako habari. Maofisini ndo usiseme, Tena waliosoma kidogo kutwa kwa waganga
 
nipo sumbawanga mitaa ya sumbawanga imepangika kuliko Mbeya karibu huku mkuu kizwite, Bible, chanji, majengo, kristo mfalme, sumbawanga asilia, bomani, katuma, mkoani,katandala, majumba sita. Welcome sumbawanga hukumambo ya uchawi hayapo ila zamani yalikuwepo
Usidanganye watu.mi niko mawenzusi.hivi kuna mfipa Hana chale kwenye makalio na kifuani?
 
Back
Top Bottom