Ni kweli Sumbawanga kuna uchawi?

Ni kweli Sumbawanga kuna uchawi?

Mbabe hunter

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2016
Posts
327
Reaction score
480
Salam kwenu wanaJF,

Sumbawanga ni wilaya ya mkoa wa Rukwa nilianza kuisikia kwa sifa nyingi zisizo nzuri na zilikuwa za uchawi tangu nikiwa mtoto nakumbuka nilipokuwa primary shule moja mkoani Dodoma kulikuwa na mwalimu wetu alikuwa wa Sumbawanga na alikuwa akilima anapata sana tofauti na wenyeji na wale wezi wa mazao walikuwa wakiiba tu wanabeba wanajikuta wampelekea kwake.

Nilizidi kuamini kuwa Sumbawanga ni wachawi sana sana na mikoa mingi ukitembea unakutana na matangazo ya waganga wa jadi kutoka Sumbawanga hii ni kuonesha ni kwa namna gani watu wa kule ni kiboko kwa mambo hayo.

Leo ni siku ya sita nipo Sumbawanga na nilipoambiwa nije huku kwa shughuli za kikazi kwa muda wa siku 14 niliogopa kidogo lakini kiukweli kabisa sijaona la kutisha maisha yanaenda na naona kunaendelea pia sioni matangazo ya waganga ila nimekutana na matangazo kadhaa kwenye miti na nguzo yameandikwa Freemansons ukitaka kujiunga piga namba.

Sasa nikajiuliza inamaana zile story za uchawi ni kweli au sio kweli? Wenyeji wamesema wachawi wamehamia vijijini hapa mjini wengi ni wageni na wamestaarabika kidogo lakini nimepewa onyo kwamba usitembee na mzawa wa huku unaweza usirudi kwenu na ukitembea nao usiwaahidi ambacho huwezi kumtimizia. Mazingira yako poa barabara ni nzuri kutoka Mbeya kwa private car kukutumia masaa matano.

Pia naona kama wamejenga vizuri tofauti na mbeya huku mitaa imetenganishwa na barabara na panaonekana vizuri tofauti na ukisimuliwa au vile unavuta picha ukitajiwa jina Sumbawanga. Wasiwasi wangu umeniisha.

Waungwana msiogope kwenda ikibidi nimeambiwa fursa nzuri ni kilimo zaidi.
 
Ni kama vile zile story za tanga ukikuta kifuu usikipige teke kitakwambia umenipigia nini au uchume embe likwambie nirudishe uliko nitoa nilikua naogopa kuja kwa kweli lakini toka nimefika haya mambo sjayaona
 
Back
Top Bottom