Ni kweli nyoka huwa wanajiunga baada ya kuuawa?

Aelknes

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
231
551
Habari za muda huu wana JF?

Leo katika pitapita zangu kuna sehemu nimekuta kuna nyoka ameuliwa.
Lakini kilichonifikirisha ni baada ya kuuliwa walimkata kichwa alafu wakakifukia na kiwili wili wakaenda kukitupa barabarani

Sababu kuu ni kufanya asijiunge
Sasa kwa wenye uelewa naomba kuuliza ni kweli nyoka huwa wanajiunga au ni imani za watu??
images%20(19).jpg
 
Nilivyokuwa kijana mdogo nilishawahi kuua nyoka nikamuacha hapo hapo nyumbani nikisubiri ajiunge nilishinda kuanzia asubuhi Hadi jioni ili tu nione nyoka atakavyojiunga ila weee wapi!,Hadi nyoka akaanza kuoza na kuliwa na wadudu,

Na siyo Mara moja kufanya hivyo...mwishowe nikaona huu ni upuuzi mkubwa ni Kama hadithi za alfu Lela ulela tu...
 
Nyoka huwa hawajoungi ila wanatabia ya kutembea wawili jike na dume na moja akipotea mwingine anafuata alimopita wamwanzo kwahiyo Kama usipokuwa makini unaweza ukamuona wapili ukahisi ndo wamwanzo.

Wengine huwa wanachukua maiti ya mwenzake au viumbe wanaokula nyoka na kwenda kuificha au kula so unaweza ukahisi labda amejiunga na kusepa kumbe amechukuliwa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
ni stori tu hakuna ushahidi wowote.Alafu sio vyema kuwaua nyoka hovyo.
 
Hapana mkuu ni story za zaman kma ile ukirukwa utakua mfupi mbona walikuruka ila sasa hv hasheem thabiti unamwona kma kigoda
 
Ni stori za kuzusha ni kama ukisimama huku wengine wamekaa unawanyonya damu,ukikutana na paka mweusi asubuhi ni mkosi,ukimwona zeruzeru unatema mate kifuani na kumuomba Mwenyezi Mungu apishe mbali na mwisho eti bundi akilia basi kuna mtu atakufa.
 
Ni stori za wazee wetu kama tunavyoambiwa leo hi eti mungu yupo na watu wanakubali!

Miaka ya mbeleni huko vitukuu wetu watakuwa wanatuona sisi wazee wao watu wa ajabu kwa kuamini eti mungu yupo.
 
Me nachokijua walikifukia kichwa sababu bado kingekuwa na uwezo wa kuuma. Hii nimethibitisha baada ya kuona samaki aina ya kamongo kutenganishwa kichwa na kiwiliwili lakini kichwa kilikuwa kinauma kisu kiasi cha kuogepesha. Swala la nyoka kujunga ni story za wahenga
 
Nyoka huwa hawajoungi ila wanatabia ya kutembea wawili jike na dume na moja akipotea mwingine anafuata alimopita wamwanzo kwahiyo Kama usipokuwa makini unaweza ukamuona wapili ukahisi ndo wamwanzo.

Wengine huwa wanachukua maiti ya mwenzake au viumbe wanaokula nyoka na kwenda kuificha au kula so unaweza ukahisi labda amejiunga na kusepa kumbe amechukuliwa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kuhusu jike na dume kufuatana ni ukweli mtupu japo sina hakika kama ni jamii zote.
 
Habari za muda huu wana JF?

Leo katika pitapita zangu kuna sehemu nimekuta kuna nyoka ameuliwa...
Walipokuwa wakisema nyoka akikatwa anajiunga, hawakuwa wanamaanisha nyoka huyu (snake). Tafsiri halisi ilikua inareflect kitendo Cha mwanaume kutahiriwa.

Sasa weka fikra katika mtazamo huo, then rudia ile kauli kuwa nyoka akikatwa kichwani, hujiunga. Utaona inaleta maana.
 
Back
Top Bottom