Ni kweli Michael Jackson aliwahi kuja Tanzania akaishia Airport akisema TZ inanuka?

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Tangu nikiwa mdogo, stori hii naiskia. Mliokuwepo au mlioshuhudia...Ni kweli Michael Jackson aliwahi kuja Tanzania akaishia Airport akisema Tanzania inanuka?
 
Alikuja na kupokelewa na rais mwinyi na ilikuwa inatangazwa laiv redio ya taifa. Katika hali ambayo haikueleweka muda mwingi michael alionekana kubana pua yake. Alikuwa kwa siku kadhaa na sio kweli kuwa aliishia eapoti.
Maceleb wengne maaruf kwa kipind hicho waliopokewa na rais mwiny ni pope john na kandabongoman wa dr congo (kipindi hicho ikiitwa zaire)
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1992 au 1993. Alikaa siku kadhaa ila alippshuka alionekana kushika pua. Unaijua mapandikizi aliyoyafanya kwenye pua yake labda yalisababisha kushika pua. Ila hakutamka kuwa pananuka. Ni ishara tu. Kumbe we ni mtoto sana
 
Ni kweli mdogo wangu, mflume huyu wa pop duninia aliwai kutembelea mji mkubwa wa tanzania uliokuwa unaitwa kwa wkt huo kama jiji la makamba, na alipumzika hapo cku kadhaa, lkn kitu cha ajabu kilichotokea wakati huo Michael alionekana kushika pua yake angali anajitokeza kusalimia watu, nafikiri hali hiyo ilisababishwa either na athari ya urekebishwaji wa sura yake ya mwanzo na kuwa sura iliyofanana na dada yake Janet jackson, au inawezekana ilikuwa ni tabia yake tu ya kuzaliwa nayo,
Sasa kibongobongo watu wakatafisiri kuwa anashika pua kwa vile anasikia harufu mbaya ya bongo,
Inawezekana kuwa kuna ukweli kwamba alikuwa anahisi harufu mbaya ya jiji letu hilo lkn hakutamka hadharani
 
12509628_1406068526074228_593145621895158471_n.png
 
129ce6c1fb7d2babc53bea38d7506a8b_full.jpg

Alipokelewa na Mh. Waziri wakati huo Hassan Diria naye ni marehemu kama Michael Jackson
 
Ni kweli mfalme huyo wa pop duniani alifika nchini hapa mwaka 1992 na kufikia hoteli ya Kilimanjaro, ambapo wakati huo hiyo ndiyo ilikuwa hoteli no. 1 nchini.
Ni kweli pia huyo jamaa alipofika hapa nchini alikuwa muda mwingi akiishika shika pua yake, lakini sidhani kuwa hiyo ilikuwa ni ishara ya kuwa alikuwa akisikia harufu mbaya ya Jiji la Dar, ila inasemekana ilikuwa inatokana na pua yake kufanyiwa plastic surgery na kuifanya kuwa ndefu tofauti na ilivyokuwa awali ilivyoumbwa na Mungu ambapo ilikuwa fupi.
 
Back
Top Bottom