Ni kweli Michael Jackson aliwahi kuja Tanzania akaishia Airport akisema TZ inanuka?

Alikuja na kupokelewa na rais mwinyi na ilikuwa inatangazwa laiv redio ya taifa. Katika hali ambayo haikueleweka muda mwingi michael alionekana kubana pua yake. Alikuwa kwa siku kadhaa na sio kweli kuwa aliishia eapoti.
Maceleb wengne maaruf kwa kipind hicho waliopokewa na rais mwiny ni pope john na kandabongoman wa dr congo (kipindi hicho ikiitwa zaire)

kubanaje pua mkuu, katika kuongea au kama vile kuna kitu kinanuka?
 
12509628_1406068526074228_593145621895158471_n.png
Hapa kashika pua ipi. Au pua yake iko mdomoni.

Mengi yanasemwa ila ni kama hearsay wachache walomwona live au kwa tv coz kipindi kicho tv zilikua zinahesabika nchini
 
naikumbuka hyo siku na mm nilienda kumshangaa michael nkashake nae akapagawa akaniachia hela nying ambazo zilinpa heshma mtaana pia akaambia tutaenda wote marekan dah had anakufa hakuwah kuntafuta nadhan laana zangu zinemponza
 
Alijjifunga kitambaa cheupe mdomoni alafu nakumbuka alitumia gari aina ya kombi rangi ya njanooo open Roof ....
 
Ila twende mbele turudi nyuma......sidhano dunia mzima kama kuna mtu maarufu kumshinda michael Jackson.......
Jamaa anashikilia taji karne hii ya 21.......

Maana watu wanamapenzi naye na mahaba yasiyo na kifani......sijawahi kuona........jamaa anapendwa utadhani mdogo wake yesu......khaaaaaa......

Mtu anaweza msema vibaya mdomoni ila moyoni anamkubali kupita maelezo.....

Jamaa kweli ni legendary ......i wish angekuwa hai hadi leo na asingekiwa na misala.......tungekuwa tunapata ngoma zenye ubunifu wa hali ya juu.......

Nakumbuka kipindi nipo katoto ka miaka 4 .....mshua alienda state.....akarudi na santuri......na sahani mbili za michael......moja ilikuwa na track ya thriller.....na nyingine ilikuwa na liberian girl.........basi nilikuwa kila siku lazima niweke track ya Liberian girl.....nilikuwa napenda kale kasauti ka yule dada anayesema " Nakukependa pia.....nakutaka pia....mpenzi weee"........nikawa naimba pia.....

Nikaiona video ya thriller kwa mara ya kwanza pale drive in ( sasa hivi pame bomolewa ni ubalozi wa marekani ) aiseee......sikulala ule usiku.......lile werewolf nilikuwa naliona kwenye giza hadi nikaona isiwe inshu naenda kulala na washua room kwao hadi nitakaposahau........

Aiseee ........acha tu huyu jamaa nimetoka naye mbali hadi machozi ya mahaba ya kazi zake yana nilenga lenga hapa.......
 
Alikuja bongo akafikia Kilimanjaro hotel akaonana na mwinyi then akaenda sinza kuwasilimia watoto wenye mtindio wa ubongo
 
Attachments

  • 1470352691242.jpg
    1470352691242.jpg
    11.9 KB · Views: 94
Pia MJ alishikana mkono na mwanadada kipindi hicho Shyrose Bhanji. Na Shyrose alikaa wiki mbili bila kunawa mkono wake kama kumbukumbu yake ya kuonana uso kwa uso na kushikana mkono na MJ.
 
Ni kweli mdogo wangu, mflume huyu wa pop duninia aliwai kutembelea mji mkubwa wa tanzania uliokuwa unaitwa kwa wkt huo kama jiji la makamba, na alipumzika hapo cku kadhaa, lkn kitu cha ajabu kilichotokea wakati huo Michael alionekana kushika pua yake angali anajitokeza kusalimia watu, nafikiri hali hiyo ilisababishwa either na athari ya urekebishwaji wa sura yake ya mwanzo na kuwa sura iliyofanana na dada yake Janet jackson, au inawezekana ilikuwa ni tabia yake tu ya kuzaliwa nayo,
Sasa kibongobongo watu wakatafisiri kuwa anashika pua kwa vile anasikia harufu mbaya ya bongo,
Inawezekana kuwa kuna ukweli kwamba alikuwa anahisi harufu mbaya ya jiji letu hilo lkn hakutamka hadharani
Jiji la Makamba?no,kama sikosei RC wa wakati huo alikuwa Mustapha Nyang'anyi
 
Pia MJ alishikana mkono na mwanadada kipindi hicho Shyrose Bhanji. Na Shyrose alikaa wiki mbili bila kunawa mkono wake kama kumbukumbu yake ya kuonana uso kwa uso na kushikana mkono na MJ.
Lol!
 
Ni kweli mdogo wangu, mflume huyu wa pop duninia aliwai kutembelea mji mkubwa wa tanzania uliokuwa unaitwa kwa wkt huo kama jiji la makamba, na alipumzika hapo cku kadhaa, lkn kitu cha ajabu kilichotokea wakati huo Michael alionekana kushika pua yake angali anajitokeza kusalimia watu, nafikiri hali hiyo ilisababishwa either na athari ya urekebishwaji wa sura yake ya mwanzo na kuwa sura iliyofanana na dada yake Janet jackson, au inawezekana ilikuwa ni tabia yake tu ya kuzaliwa nayo,
Sasa kibongobongo watu wakatafisiri kuwa anashika pua kwa vile anasikia harufu mbaya ya bongo,
Inawezekana kuwa kuna ukweli kwamba alikuwa anahisi harufu mbaya ya jiji letu hilo lkn hakutamka hadharani

Wewe nawe muongo. Wakati anakuja Michel mkuu wa mkoa alikua ni Mary Chipungahelo.
 
Back
Top Bottom