Loading
JF-Expert Member
- Feb 10, 2012
- 594
- 101
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania One Theatre TOT na pia Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi (CCM), Hayati John Komba alitoa kali ya mwaka baada ya kuanika sifa za kaburi ambalo angependa azikwe siku akifa.
Akizungumza na Amani Mei 2, mwaka huu katika Makaburi ya Mwananyamala Kwakopa jijini Dar es Salaam kulikokuwa na mazishi ya msanii wa kundi lake, Fatma Ally Fatuma Dogodogo, Komba alisema hatafurahi endapo atazikwa kwenye kaburi lisilo na hadhi.
Alidai kuwa, anaamini kaburi lake likijengwa katika muonekano mzuri itakuwa rahisi hata kwa watu watakaokuwa wanakwenda kumuombea kuvutiwa kuliko kumfukia kikawaida.
Siku nikifa naomba kaburi langu lijengwe kwa marumaru na juu liwekewe kioo cha kuslaidi ili hata mtu akitaka kuja kufanya ibada ya kuniombea, awe anavuta tu kioo kisha anashuka ngazi hadi kwenye jeneza langu, sio kama hivi wanavyozikwa wengine, alisema Komba.
Hivyo tunaimani wana familia watatekeleza matakwa haya.
Source GPL