Ni kweli Mh. Komba alitabiri kifo chake?

Ni kweli Mh. Komba alitabiri kifo chake?

Wananchi tumieni hospitali ya muhimbili kwa ugonjwa wa kisukari na moyo la sivyo mtakufa ni magonjwa yanayohitaji wataalwmu madactari na manesi wenye ujuzi wakuto dawa za magonjwa hayo.
 
leo watu wanakimbizana na marehemu utadhani bado yupo hai
ukinda fb wamo twitter wamo ig wamo jf ndio kabisaaa kweli kapteni kumtusi mzee warioba sasa naamini imemkosti

ingekua kweli binadamu akimtusi binadamu mwenzake Mwenyezi Mungu huchukua roho yake papohapo - wengi kwenye jf wangekua marehemu miaka kadhaa - kifo cha binadamu kilishapangwa kabla hajazaliwa, kila mtu anakumbuka siku ya kuzaliwa lakini hakuna anayeijua siku, saa, mahali wala sababu ya kifo chake
 
ingekua kweli binadamu akimtusi binadamu mwenzake Mwenyezi Mungu huchukua roho yake papohapo - wengi kwenye jf wangekua marehemu miaka kadhaa - kifo cha binadamu kilishapangwa kabla hajazaliwa, kila mtu anakumbuka siku ya kuzaliwa lakini hakuna anayeijua siku, saa, mahali wala sababu ya kifo chake

kuna watu wanajua siku zao za kufa dogo acha kukariri.
 
Khaa!! Kwani babu wa babu yako naye alikosa nini naye hadi akafa? Hivi akili zenu zikoje?mnamshambulia mtu asiye na uwezo wa kujibu mapigo hawezi kugombea wala kujibu hoja zenu wakati wapo wengi wazima mnawagwaya. Hii ndiyo dalili kuu ya mtu dhaifu huwa anapigana na maiti. Kumbe ndiyo maana sisi ni masikini angalau sasa JK atakuwa na majibu kwa nini sisi ni masikini

kweli kabisa mkuu!
 
Hata mimi hayo magazeti msiyalete humu huo utabiri uko wapi msitake sifa za bure eti alitabiri kioi sasa acheni ujinga wa kupost ujinga rip komba JOHN
 
Mafarao wamezikwa kwenye mapiramidi, lakini hilo halibadili ukweli kwamba wamekufa.

Ni ujivuni wa kibinadamu tu.
 
Mnaposema R.I.P(Rest In Peace),huwa mnamwambia nani haswa!,Mungu au marehemu!,acheni kuiga mambo yasiyokuwa na maana yoyote,wengi nimeona wanasema rest in peace!,haiwezi kubadili sehemu marehemu alipokwenda,kifo kimewekwa mara moja na ukishakufa unakwenda moja kwa moja hukumuni,unapoiambia maiti ipumzike kwa amani haisikii,haifahamu tena mambo ya duniani,muda tunapokuwa hai hapa duniani,ni wakati wa kutenda mema na kutengeneza maisha ya baadae baada ya kifo,sisi tulio wakristo tunaambiwa kwamba pasipo kuwa na utakatifu kamwe hatutaweza kumwona Mungu,sasa haya maneno ya R.I.P,mimi binafsi naona tu kuwa ni faraja za kujitaabisha wala hayawezi kubadili chochote,(mtu asipozaliwa mara ya pili,kwa maji na kwa roho hawezi kuurithi ufalme wa mbinguni),tutafute kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna atakayemwona Mungu asipokuwa nao.Kupumzika kwa amani(R.I.P) kwa Mkristo anatengeneza mwenyewe akiwa hai,akishakufa huwezi kumuombea tena.Mbarikiwe.
 
Kifo ni kilele cha matokeo ya the second law of thermodynamics kwa vyoye vyenye uhai.

Hujanipa jibu bado.
Andika kwa kiswahili hakuna mtu amekuwekea Swali Kiingereza.

Kifo Ni Nini. Na Huo uhai Uliotaja hapo juu Ni NINI?
 
Kwa nini nikujibu na kwa nini nikujibu kwa Kiswahili?

Teh teh teh teh!

Usilete ujanja wa kitoto wewe.
Sema Sina jibu.
We si unawaimbia nyimbo watu kila siku hapa Jukwaanj kuwa kila unachokikubali Una ushahidi Nacho?

Sasa nipe ushahidi hapa wa Kifo ulichosema hapo juu pamoja na huo Uhai.

Kifo ni nini?
Na UHAI ni Nini?
 
Back
Top Bottom