Ni kweli Mh. Komba alitabiri kifo chake?

Ni kweli Mh. Komba alitabiri kifo chake?

Khaa!! Sasa kitu gani kimelipwa? Hivi huna hata akili kidogo tu za kuweza kujua kifo ni nini?

Kifo ni kukata roho,kupotea kwenye uso wa dunia tunakuzika kama tunakuwepo,hujamwelewa kuhusu "malipo ni hapa duniani",komba alikuwa na mpango mchafu na watanzania,kutoa kauli ya tutakwenda msituni haikuwa lugha sahihi ili kutetea udhalimu wa katiba ya ccm.
 
Kuomba alikuwa bogus..
Lakini rest in peace
 
Kifo ni kukata roho,kupotea kwenye uso wa dunia tunakuzika kama tunakuwepo,hujamwelewa kuhusu "malipo ni hapa duniani",komba alikuwa na mpango mchafu na watanzania,kutoa kauli ya tutakwenda msituni haikuwa lugha sahihi ili kutetea udhalimu wa katiba ya ccm.

Sawa sawa
 
mwenywe niliona labda nasoma vibaya ila sijaona utabiri ila aliacha will yake ya jinsi ya kuzikwa

Na wosia ni kitu cha kawaida kabisa maana hakuna mwanadamu ataishi milele katika damu na nyama...
 
Badala akumbuke namna ya kulipa madeni crdb bank na kwengineko au kuwapa wanae ujanja wa kuepuka hayo madeni akiwa hayupo yeye anang'ang'ania makaburi ya tiles,sasa ngoja mali zitaifishwe aone kama hela za kuweka marumaru zitapatikana.
 
Kifo ni kukata roho,kupotea kwenye uso wa dunia tunakuzika kama tunakuwepo,hujamwelewa kuhusu "malipo ni hapa duniani",komba alikuwa na mpango mchafu na watanzania,kutoa kauli ya tutakwenda msituni haikuwa lugha sahihi ili kutetea udhalimu wa katiba ya ccm.
Khaa!! Kwani babu wa babu yako naye alikosa nini naye hadi akafa? Hivi akili zenu zikoje?mnamshambulia mtu asiye na uwezo wa kujibu mapigo hawezi kugombea wala kujibu hoja zenu wakati wapo wengi wazima mnawagwaya. Hii ndiyo dalili kuu ya mtu dhaifu huwa anapigana na maiti. Kumbe ndiyo maana sisi ni masikini angalau sasa JK atakuwa na majibu kwa nini sisi ni masikini
 
Ccm wanajiona wataishi milele
CCM ni nani wewe? Ni mtu m jinga tu anaweza kujitapa kama yeye ni ccm au cdm au chama chochote kama si mvivu mpenda kula vya bure ( mwanasiasa). Kuna tofauti kubwa kati ya vyama vya siasa na klabu za yanga na simba
 
lakini msisahau plan yake kwenda msituni haikuwa kwenda kucheza ngoma ilikuwa ni kuja kuua watu sasa sijui mnalimlilia nini?
 
Na wosia ni kitu cha kawaida kabisa maana hakuna mwanadamu ataishi milele katika damu na nyama...

tatizo letu sisi wa bongo ukiacha wosia tunadanganyana yakua unajichuria kufa lakini kiuhalisia hakuna kitu kama hiko, na kuna ubora wa kuacha wosia kwan utakua umejitendea haki yako muhim ya mwisho
 
Nadhani uongozi ni utashi.binafsi sidhani kama walio ccm wote ni wadhambi na walio cdm ni wasafi,kila binadam anatamaaa ya kula hasa anapotengewa na kuona ufree upo,tumeshuhudia Libya na kwingineko.kikubwa ni kupata kiongozi mwenye uchungu na nchi na wananchi wake.hatuwezi kukaa na kusubiri sijui ccm aingie au cdm aingie atuleteee mahitaji home hapana,lazima ujishughulishe,akiingia hujali familia rafiki wapambe,jiulize wewe Nani kwake.hivyo ni vyema kufikiri sana. Kila nafsi itaonja mauti na hakuna kipimo cha matendo yetu.maana tunaambiwa hakuna ajuaye kama ni mwema hadi siku ya hukumu.Asamehewe kwa mabaya tuyaonayo ss na apumzike kwa amani John Komba
 
Hizo hela za kujengea kaburi la gharama ni vizuri zikaelekezwa kwny kulipa madeni aliyokuwa akidaiwa na bank. Kwa sasa familia inalia kwa Mambo mawili, kufiwa na mzazi/mme, kupigwa mnada mali nyingi alizokuwa amechuma na hivyo familia kubaki haina kitu!
 
Hivi chenge yeye bado hajatabiri atakufa lini? Maana ndo mzigo uliobaki
 
View attachment 230657

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania One Theatre ‘TOT’ na pia Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi (CCM), Hayati John Komba alitoa kali ya mwaka baada ya kuanika sifa za kaburi ambalo angependa azikwe siku akifa.

Akizungumza na Amani Mei 2, mwaka huu katika Makaburi ya Mwananyamala Kwakopa jijini Dar es Salaam kulikokuwa na mazishi ya msanii wa kundi lake, Fatma Ally ‘Fatuma Dogodogo’, Komba alisema hatafurahi endapo atazikwa kwenye kaburi lisilo na hadhi.

Alidai kuwa, anaamini kaburi lake likijengwa katika muonekano mzuri itakuwa rahisi hata kwa watu watakaokuwa wanakwenda kumuombea kuvutiwa kuliko kumfukia kikawaida.

“Siku nikifa naomba kaburi langu lijengwe kwa marumaru na juu liwekewe kioo cha ‘kuslaidi’ ili hata mtu akitaka kuja kufanya ibada ya kuniombea, awe anavuta tu kioo kisha anashuka ngazi hadi kwenye jeneza langu, sio kama hivi wanavyozikwa wengine,” alisema Komba.

Hivyo tunaimani wana familia watatekeleza matakwa haya.

Source GPL

Sijaona mahali alipojibashiria namna atakavyokufa (ambako ningekubali kuwa alijitabiria kifo chake) bali alieleza namna anavyotaka azikwe.
 
Maandiko matakatifu yanasema. WAHESHIMU BABA NA MAMA YAKO SIKU ZAKO ZIPATE KUWA NYINGI DUNIANI. Marehemu JK alimtukana mzee Warioba ambaye ni sawa na mzazi wake. MUNGU anajua sababu ya kumtanguliza mbele ya haki.
 
Jahannamu ndio makazi ya kuffar. Hivi sasa anajuta huko aliko.
 
Back
Top Bottom