Ni kweli mapenzi ya siri yana ukomo wake.

Ni kweli mapenzi ya siri yana ukomo wake.

saudari

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
2,655
Reaction score
2,783
Habari zenu wana MMU!!!
Mimi kama mimi kwa mtazamo wangu naona mapenzi ya siri yana ukomo wake.
Unapokuwa unapenda mapenzi ya siri sana, unampa wakati mgumu mwenzako.
Ni rahisi kufikiria kwamba, unafanya hivyo kwa kuwa ama hujiamini au una mtu mwingine. Weka mambo hadharani. Mtambulishe mwenzi wako kwa marafiki zako.

Jiamini, unapokutana na mtu uliyesoma naye zamani au kuishi naye sehemu moja, mwambie kwamba uliyenaye ni mwenzako na unatarajia kuingia naye kwenye ndoa. Kufichaficha kunaondoa utamu wa mapenzi. Kunazidisha maswali ambayo hayana majibu. Kama yapo ni huyo mwenzako kujijibu mwenyewe. Kwa kawaida, hatajipa majibu mazuri. Yatakuwa ya kinyume – yenye tafsiri mbaya. Kwamba yawezekana hutaki kumtambulisha kwa kuwa una mtu mwingine.

Je, ni kweli? Kama ndivyo huna sababu ya kumpotezea muda mwenzako. Kama si kweli, basi amka. Gundua kwamba ulikuwa unafanya makosa na uanze ukurasa mpya.


Ni mtazamo tuu,hata wewe waweza kuwa na mtazamo wako.





 
Hussein wa watu alijiimbia''Siri ya nini?''nini maana yakee siri ya nini nini hasara yake?wewe ni wangu mimi ni wako' siri ohhh siri ya mapenzi siri ooooh wenzangu mapenzi ya siri nalialia''Siri hazifai kwenye mapenzi ya kweli.Siri zinaleta maumivu kwenye mapenzi.
 
Sasa nimtambulishe wakati nna uhakika sina future naye?

Au unaongelea wapenzi wa aina gani?

Yaani nimtambulishe kimada wangu kwa mke?[/QUOTE Kongosho bana we point zako zinaniachaga hoi kwa vicheko,ujue mi nitakushtaki oohooooo sijui we point zako unazitoleaga wapi?sa hivi nitakuwa nikiona comment yako nakuwa naziba macho maanake mmmmhhhh zis is too much.sasa hivi unaweza kumtambulisha kimada kwa mke kweli?au unatafuta timbwili na wife?
Sasa upo naye wa nini kam huna feature naye?
 
Last edited by a moderator:
Hussein wa watu alijiimbia''Siri ya nini?''nini maana yakee siri ya nini nini hasara yake?wewe ni wangu mimi ni wako' siri ohhh siri ya mapenzi siri ooooh wenzangu mapenzi ya siri nalialia''Siri hazifai kwenye mapenzi ya kweli.Siri zinaleta maumivu kwenye mapenzi.

Looh! wish ungeniona baada ya kupata hii ridhimu faster nimeufuata huu wimbo naburudisha nafsi
 
::
saudari
Siku hizi ni wako ukiwa nae !!
Tungejua wanavyotupanga tungejinyongea uzi wa buibui !!
Unampenda mtu,akisikia unamtambulisha anajua we kakushika.
Anacheka kwako ukitoka anawalilia wengine,tena chozi la chumvi eti anawapenda.
FEW ARE LUCKY TO HAVE THEIR MATCHES
=
 
Last edited by a moderator:
Niaminicho mimi katika mahusiano hasa nizungumzie upande wetu wanaume hasa wale wapenda totoz wengi kwa wakati mmoja, mara nyingi anakuwepo mmoja anaetambulishwa kwa marafiki hata ndugu na huyu amefikia level ya juu ya kupewa daraja la mke. Sasa kama wakitambulisha wote na wengine wana timu ya mpira si wataonekana sio riski kwa marafiki na ndugu?????????????????????. "Mwisho wa yote Ukimwi unaua na kama kondomu zinakinga mbona maambukizi yanaongezeka?"
 
Kimada huwa yupo tu

Utamu wa main course kuwe na starter na dessert pia

Kongosho bana we point zako zinaniachaga hoi kwa vicheko,ujue mi nitakushtaki oohooooo sijui we point zako unazitoleaga wapi?sa hivi nitakuwa nikiona comment yako nakuwa naziba macho maanake mmmmhhhh zis is too much.sasa hivi unaweza kumtambulisha kimada kwa mke kweli?au unatafuta timbwili na wife?
Sasa upo naye wa nini kam huna feature naye?
 
mi sijaelewa .... labda saudari atoe ufafanuzi zaidi lolz

unataka wenzio watokwe na manunduuu eee..

na wengine wawe na event za utambulisho consecutively kwi kwiiiiii
 
Last edited by a moderator:
Kuna wakati inakuwa ngumu kutambulishana hata kama mnapendana.Yaache Mapenzi yatajitambulisha yenyewe tu wakati ukifika.
 
Niaminicho mimi katika mahusiano hasa nizungumzie upande wetu wanaume hasa wale wapenda totoz wengi kwa wakati mmoja, mara nyingi anakuwepo mmoja anaetambulishwa kwa marafiki hata ndugu na huyu amefikia level ya juu ya kupewa daraja la mke. Sasa kama wakitambulisha wote na wengine wana timu ya mpira si wataonekana sio riski kwa marafiki na ndugu?????????????????????. "Mwisho wa yote Ukimwi unaua na kama kondomu zinakinga mbona maambukizi yanaongezeka?"

Kama umaona mkeo amewazidi wote mpaka ukampa "golden chance" kwanini utangetange nje?? Huku unajua kabisa "Ukimwi unaua na kama condom zinakinga mbona maambukizi yanaongezeka". TAFAKARI NA UCHUKUE HATUA.
 
Looh! wish ungeniona baada ya kupata hii ridhimu faster nimeufuata huu wimbo naburudisha nafsi
Basi mwenzio sio misifa hiyo sa hivi ungeuona mkichwa wangu hata usingeamini umekuwa huooo,si unajua tena ndugu yangu kumkumbushia mtu mbali raha wewe!!
 
mi sijaelewa .... labda saudari atoe ufafanuzi zaidi lolz

unataka wenzio watokwe na manunduuu eee..

na wengine wawe na event za utambulisho consecutively kwi kwiiiiii

Ninachotaka mimi ni kuwa na msimamo kwa maamuzi uliyoyachukua kabla haujamkabidhi mtu mwingine moyo wako/ fall in love kwa mtu, it means kama umeamua kuwa na mtu kwanini usichukue uamuzi wa kumtambulisha kwa rafikizo???
Kama umeona mkeo hakutoshelezi kwa namna moja au nyingine kwanini usimweleze ukweli ili ajue ni wapi pakujirekebisha???
 
ni kweli uwazi ni mzuri kwenye mahusiano, hakuna haja ya kuwa msiri, anayefanya hivyo bado hajafanya chaguo sahihi, bado anapepesa macho huku na huko akiwa na vidumu kibaao, huwez kutambulisha wote ndiyo, lakini mazingira ya kufanya hivyo yanapotokea basi ni vyema ukafanya hivyo kwa kujiamini ili kuendelea kumjengea uaminifu mpenzi wako....
 
Back
Top Bottom