Ni kweli Majaji wetu wamefikia kuitana Majina Haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli Majaji wetu wamefikia kuitana Majina Haya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kimbunga, Apr 12, 2012.

 1. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Wanabodi nilikuwa nasoma makala kwenye Gazeti la Raiamwema ambayo imeandikwa na Msomaji Raia yenye kichwa cha Habari Majaji wana chanjo ya kutotumiwa kisiasa? nikakutana na sntensi zifuatazo:  Mpaka hapa ni sahihi pia kuhoji ikiwa majaji wetu wako salama na michezo ya kisiasa. Hawa ni watu muhimu katika wajibu wa kutoa haki, je, wanayo chanjo ya kuwazuia kupata ugonjwa unaoitwa siasa?  Kama wanayo mbona hawa wao wenyewe wanatuhumiana na kuitana majina ya bandia. Wako majaji wanaoitwa “M-serikali”, “Wa system”, wa “Voda Fasta”, “Wa Ikulu” na “wa awamu ya nne”.


  Raia Mwema | Majaji wana chanjo ya kutotumiwa kisiasa?

  Hivi kweli wakuu Majaji wetu ambao tunawategemea kutoa haki wamefikia hatua ya kuitana majina hayo? Kwa maana nyingine ni kwamba judiciary yetu imegawanyika kiasi cha mgawanyiko huo kuwa reflected na hayo majina ambayo Msomaji anasema wanaitana? Je ukiwa na kesi yako kwa Voda fasta utatapata haki sawa na kesi hiyo hiyo kama ingepelekwa kwa M-serikali, nk?
   
 2. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Kwa tz hamna haja ya kuwa na majaji, kwani wapowapo tu kupindisha haki kutokana na maslahi yao(fake and foolish judges)
   
 3. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Na hii ni kwa sababu ya kuwaweka incompetent lawyers kuwa majaji... Embu fikiria mfano mtu kama mwanasheria mkuu anvyochemkaga mbele ya kina TL na Mbowe utasema ni jaji yule au Upe tu.
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kimbunga, umeshawahi kuhusika (kwa namna moja ama nyingine) na kesi yoyote iliyosikilizwa na jaji au hata hakimu? Kuna rushwa, visasi, wivu, kulipa fadhila nk na mara nyingine hata udini!

  Sina hakina wewe upo katika fani gani au unajishugulisha na nini lakini kwa ujumla matatizo na changamoto unazoziona katika jamii zinakuwa reflected karibu kwenye fani zote...sheria (mawakili, majaji, mahakimu, wazee wa baraza etc), walimu, madaktari, wahasibu nk nk. Majaji ni binaadamu kama mimi na wewe...ni kweli wana taaluma, uzoefu na weledi katika sheria lakini aspect ya kibinaadamu haiwezi kuondoka....kama ni mpenda rushwa atakula rushwa, kama ni mwizi ataiba tu, kama sio mtu wa kutunza siri ndio hivyo atavujisha siri nk nk. Na hata hizo taaluma, uzoefu na weledi katika sheria zinatofautiana sana kutoka jaji mmoja mpaka mwengine...na kwa kweli wao wenyewe watu wa sheria wanajuana sana....vodafasta wanajulikana, 'waliopewa' tu ujaji kwa maslahi ya watu au makundi fulani pia wanajulikana!
   
 5. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mahakama ni sehemu ya haki ambayo sio lazima itoe haki, Ukihoji mwenendo wa mahakama unaleta virugu lakini Je, haki kupotelea mikononi mwa mahakama ni sahihi??? au nako pia ni kuleta vurugu???

  Napendekeza mtu akikataa rufaa ikaonekana jaji aliboronga, jaji huyu apewe kalipio kali na akirudia mara kosa hilo ndani ya miaka mitano afukuzwe na akifanya kosa hilo mara tatu afukuzwe pia.
   
 6. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Majaji vilaza nchi hii, Mwanasheria mkuu ndo kilaza kabisa, Viongozi vilaza usisema, sijui tutaponea wapi
   
 7. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kimbunga,

  This is one of many patriotic bombs set to destroy this beloved country the soonest.. and it includes,

  (1) Mawaziri wa awamu ya 4 ambao ni mabomu ya kuua nchi ni pamoja na
  • Kawambwa (Elimu)
  • Ngereja (Maliasili)
  • Mponda (Afya)
  • Malima (Ujenzi)
  • ..
  (2) Majaji

  • Huyo aliyehukumu kesi ya Lema
  • Huyo anayeendesha kesi ya Lisu, T.
  • ...
  (3) Universities' Management

  • Prof Mkandara (UDSM)
  • ................. (UDOM)
  • ...
  (4) RCs & DCs

  • RC wa Arucia
  • DC wa Igunga TABORA
  • ...
  Kwa hali hiyo nchi itazama
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu kinachonitisha ni haya majina wanayoitana. Unajua kama waalimu wanaoitwa Vodafasta tunajua kuwa wamepelekwa wakasoma fasta fasta na matokeo yake tunayaona. Sasa kama watoa haki nao ni fasta fasta matokeo yake ni nini?
   
 9. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wangu hata mie hiyo makala nimeiona, ukweli inasikitisha sana kuona sasa Judicial system kwisha habari yake, na hiyo ni kutokana na hawa jamaa(majaji) kuwa presidential appointees, lazima wafanye kazi kwanza wakihakikisha wanalinda maslahi ya aliye wateua, na mwisho ndipo wewe na mimi tushughulikiwe na si kupewa haki. Jambo hili halina dawa kwa sasa mpaka tutakapo kuwa tumepata katiba mpya ambayo itatoa mwongozo wa kuwapata majaji. Tunashukuru hukumu ya kesi ya Lema ambayo imefumbua macho wengi japo watu walikuwa wakihoji kimya kimya weledi wa majaji wetu. Yaani inatia hasira kiasi ikitokea ukawa raisi unaweza kuwapiga chini majaji wote iwapo sheria ingeruhusu na kuajili upya kwa interview kali wao pia wakipewa fursa ya kuomba ajira hiyo na kampuni maarufu zinazo jali credibility kufanya kazi hiyo ndipo bunge liridhie. Watu wengine ambao wanapaswa kupigwa chini kama alivyo fanya raisi mpya wa Malawi ni kupiga chini IGP, RCs,DCs, na hata mkuu wa majeshi sababu amewafanya wanajeshi wetu wamekuwa mbumbumbu pasipo kuona maslahi ya taifa yanaporwa wao wako kimya tu! au kwa sababu wanauziwa bia na bidhaa nyingine kwa bei ya chini! Waangalie mfano wa nchi ya Mali na kwingineko. Nadhani imefika wakati wa askari wa vyeo vya chini kuchukua hatua kwa sababu wao ndio wamewahi kushinikiza mabadiliko haswa katika nchi nyingine. Wakikaa kusubiri tu amri hata za kishenzi ndipo tunazidi kuwaona hamnazo. Wasidhani hata siku moja IGP,mkuu wa majeshi na wenzake watakuwa upande wa wanyonge kwa sababu wao ndio wanafaidi inchi na mafisadi, inabidi ifike wakati waasi na wakatae amri za kishenzi, inakuwaje mtu anakataza watu wasiandamane na wewe unaye pewa amri ukawadhibiti unajua kuwa ni haki yao kikatiba na sheria inasema hivyo? hseria gani hiyo wanayo simamia? ya magamba au? oneni wenzenu Misri na Tunisia walicho fanya na mjifunze. Ipo siku mtafanya maafa na hao wanao watumeni watawaruka kwenye mkono wa sheria. Mfano huo umetokea Rwanda, askari wengi wamejikuta na kesi za kuhusika katika mauaji ya kimbari pasi kutetewa na walio watuma wakati walikuwa wanatimiza amri wanazodai ni halali. Lazima muwe na uwezo wa kuangalia kuwa je, ninacho amriwa kufanya ni kwa mujibu wa sheria? Mie wakati mwingine nashawishika kufikiria kuwa labda ni kutokana na uwezo mdogo wa kufikiria na kuchambua mambo wa askari wetu ambacho nadhani kinachangiwa zaidi na elimu ndogo sababu wengi ni Darasa la saba na walio feli kidato cha nne. Kwa hiyo wanaona iwapo watashindwa kutii amri watafukuzwa kazi na hawana uwezo wa kupata kazi mahali pengine. Unganeni na jeshi la umma la ukombozi tukomboe nchi yetu kwa kukataa kutii amri ambazo hazina tija kwa taifa, kwani kazi ni kuwa polisi au mwanajeshi tu? uiacha au ukafukuzwa utakufa? mnatutia aibu kwa mawazo mgando.
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Ndio hivyo mkuu tunashuhudia hukumu za hovyo hovyo tu. Tizama performance ya wanaoitwa wanasheria wakuu - AG's (ambao wana sifa za kuwa Jaji kwa mujibu wa katiba) - Chenge, Mwanyika na sasa Jaji Werema (msikilize akiongea bungeni!)...yaani ni aibu tupu!
   
 11. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya inatakiwa kuwakana mahakimu na majaji wote ili tuanze upya kuwapata majaji kwa mujibu wa weledi. Hii aibu iliyopo mahakamani ikichagizwa na Mwanasheria mkuu aliyewekwa kiswahiba itakuja kuliingiza taifa katika machafuko makubwa. We fikiria wale majaji walioogopa kutoa hukumu kesi ya mgombea binafsi na kuirudisha bungeni utasema wana weledi kweli?
   
 12. E

  ESAM JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mkuu Kimbunga kama jaji anaitwa vodafasta maana yake aliteuliwa kuwa jaji bila kuwa na uzoefu wakutosha pamoja na sifa nyinginezo ingawa vigezo anaweza kuwa navyo. Hii yote inasababishwa na kuwa na mfumo mbovu wa uteuzi wao uliopo unaingiliwa sana na wanasiasa ili kulinda maslahi yao
   
 13. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  guys where are we going, we need to find the chanjo as soon as possible. By the way kuna namna yoyote ya kuweza kutangua u-jaji wwa mtu iwapo nanashambuliwa na ugonjwa wa siasa?
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu hao majaji ndio wamepewa jukumu la kusimamia katiba mpya! Hapa ni kweli inatakiwa tufanye kama Kenya manake wao waliamua kuanza upya kwenye judiciary wakapiga chini kuanzia Chief Justice hadi majaji wa mahakama kuu. Watu wakaomba na kuhojiwa hadharani na kama ulihukumu kakkesi kako huko nyuma kwa magumashi inakuwa hapo ndipo unapigwa chini mwanzoooni!
   
 15. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo makala nimeiona, ukweli inasikitisha sana kuona sasa Judicial system kwisha habari yake, na hiyo ni kutokana na hawa jamaa(majaji) kuwa presidential appointees, lazima wafanye kazi kwanza wakihakikisha wanalinda maslahi ya aliye wateua, na mwisho ndipo wewe na mimi tushughulikiwe na si kupewa haki kama suala lina maslahi ya kisiasa. Nakumbuka kuna jamaa yangu Advocate aliniambia siku za nyuma kuwa sheria ina nguvu, lakini siasa ikiingilia kati sheria haina nguvu tena. Kesi ya Lema imedhihirisha hilo. Jambo hili halina dawa kwa sasa mpaka tutakapo kuwa tumepata katiba mpya ambayo itatoa mwongozo wa kuwapata majaji. Tunashukuru hukumu ya kesi ya Lema ambayo imefumbua macho wengi japo watu walikuwa wakihoji kimya kimya weledi wa majaji wetu. Yaani inatia hasira kiasi ikitokea ukawa raisi unaweza kuwapiga chini majaji wote iwapo sheria ingeruhusu na kuajili upya kwa interview kali wao pia wakipewa fursa ya kuomba ajira hiyo na kampuni maarufu zinazo jali credibility kufanya kazi hiyo ndipo bunge liridhie. Watu wengine ambao wanapaswa kupigwa chini kama alivyo fanya raisi mpya wa Malawi kwa IGP wao ni kuwapiga chini IGP, RCs,DCs,RPCs,OCDs, bila kumsahau mkuu wa Jeshi la ulinzi kwa sababu amewafanya wanajeshi wetu wamekuwa mbumbumbu pasipo kuona maslahi ya taifa yanaporwa wao wako kimya tu! au kwa sababu wanauziwa bia na bidhaa nyingine kwa bei ya chini makambini! Waangalie mfano wa nchi ya Mali na kwingineko. Nadhani imefika wakati wa askari wa vyeo vya chini kuchukua hatua kwa sababu wao ndio wenye dhiki kama sisi na kuna mifano ambapo wamewahi kushinikiza mabadiliko katika nchi nyingine haswa Afrika magharibi. Wakikaa kusubiri tu amri hata za kishenzi ndipo tunazidi kuwaona hamnazo. Wasidhani hata siku moja IGP,mkuu wa majeshi na wenzake watakuwa upande wa wanyonge kwa sababu wao ndio wanafaidi inchi na mafisadi, inabidi ifike wakati waasi na wakatae amri za kishenzi, inakuwaje mtu anakataza watu wasiandamane na wewe unaye pewa amri ukawadhibiti unajua kuwa ni haki yao kikatiba na sheria inasema hivyo? sheria gani hizo mnazo simamia? za magamba au? oneni wenzenu Misri na Tunisia walicho fanya wakati wa vugu vugu la mabadiliko kwenye nchi zao na mjifunze. Ipo siku mtafanya maafa na hao wanao watumieni watawaruka kwenye mkono wa sheria. Mfano huo umetokea Rwanda, askari wengi wamejikuta na kesi za kuhusika katika mauaji ya kimbari pasi kutetewa na walio watuma wakati walikuwa wanatimiza amri wanazodai ni halali. Lazima muwe na uwezo wa kuangalia kuwa je, ninacho amriwa kufanya ni kwa mujibu wa sheria? Mie wakati mwingine nashawishika kufikiria kuwa labda ni kutokana na uwezo mdogo wa kufikiria na kuchambua mambo wa askari wetu ambacho nadhani kinachangiwa zaidi na elimu ndogo sababu wengi ni darasa la saba na walio feli kidato cha nne. Kwa hiyo wanaona iwapo watashindwa kutii amri watafukuzwa kazi na hawana uwezo wa kupata kazi mahali pengine. Unganeni na jeshi la umma la ukombozi tukomboe nchi yetu kwa kukataa kutii amri ambazo hazina tija kwa taifa, kwani kazi ni kuwa polisi au mwanajeshi tu? ukiacha au ukafukuzwa utakufa? mnatutia aibu kwa mawazo mgando.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Duh mkuu una hasira! Huoni Sanogo kakimbia? Tuwasubiri tu kwenye sanduku la kura. Miaka mitatu si mingi.
   
 17. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,313
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Serikali ya kifisadi itatoa majaji wa kifisadi. Period.

  Mie nawaita majaji "yebo yebo"
   
 18. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Nivgumu majaji wetu kuepuka michezomichafu yakisiasa kwakuwa anayewateua kuwa majaji nimwanasiasa,nivyema kikaundwa kitengo maalumu kwaajiri yakuwateua majaji na si vngnevyo.mm simjuzi wamambo yakisheria lkn najiulza maswli mwenye nakosa majbu.kuna jopo lolote linalotambulika kisheria kwaajiri yakuhakiki uelewa wao washeria?kwann majaji wasiteuliwe na majaji wenzao?kuna siku tunaweza tukampata rais mtata akamteua mke wake kuwa jaji mkuu nk.Nivema katiba mpya iwe wazi juu yajambo ili.
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Voda fasta na sasa yebo yebo. Tumeshuhudia shule za kata na hata kuna vyuo vikuu vinaitwa vya kata labda na kwenye judiciary na kwenyewe kuna wa kata.
   
 20. b

  busar JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hapana tunao bado Kama marehemu Rugakingira
   
Loading...