Ni kweli Majaji wetu wamefikia kuitana Majina Haya?

(4) RCs & DCs

  • RC wa Arucia
  • DC wa Igunga TABORA
  • ...
Kwa hali hiyo nchi itazama[/QUOTE]


Kwenye bold ndiyo wapi Mkuu? Of all DC's.... Mnari (aliyewaramba bakora walimu) was the best.
 
Samaki anaoza kwa kuanzia kichwani. Vivyo hivyo uongozi wa dola unaharibika kuanzia kichwani. Tafakari chukua hatua.
 
Tutajie japo Jaji mmoja ambaye viwango vyake japo vinakaribia vya Judge Lugakingira.

Marekebisho ni Marehemu Judge Rugakingira na siyo Judge Lugakingira kama nilivyoandika hapo juu.
 
Tutajie japo Jaji mmoja ambaye viwango vyake japo vinakaribia vya Judge Lugakingira.

Hakuna hata mmoja, wangekuwepo wasingetoa hukumu za hovyo kama zifuatazo;

1. Babu Seya
2. Dowans
3. Mgombea Binafsi
4. Ditto (kabla Mungu hajaamua kumhukumu)
5. Lema
6. makongoro Mahanga (haijatoka ila upepo unaonekana labda waone aibu)
7. Chenge alivyoachiwa huru baada ya kuua makusudi (alipigwa faini)
8. EPA

Jamani nchi hii kuna wanasheria wasiojua sheria. Hiyo ni mifano tu kuna kesi nyingi majaji wanahukumu mpaka layman anabaki mdomo wazi
 
Isije ikawa makala imeandikwa na mtu mwenye hasira na system ya judicial Tanzania, pengine alifanya makosa akala kibano!

All in all I hope hayo yanayosemwa si ya kweli
 
Hakuna hata mmoja, wangekuwepo wasingetoa hukumu za hovyo kama zifuatazo;

1. Babu Seya
2. Dowans
3. Mgombea Binafsi
4. Ditto (kabla Mungu hajaamua kumhukumu)
5. Lema
6. makongoro Mahanga (haijatoka ila upepo unaonekana labda waone aibu)
7. Chenge alivyoachiwa huru baada ya kuua makusudi (alipigwa faini)
8. EPA

Jamani nchi hii kuna wanasheria wasiojua sheria. Hiyo ni mifano tu kuna kesi nyingi majaji wanahukumu mpaka layman anabaki mdomo wazi

Ndugu naona unaropoka hujui unachosema.

Dowans, ni katika mojawapo ya kesi ambazo hukumu zake hazina utata. Nenda ukawalaumu viongozi wako wako wa kisiasa kwa kuingilia mambo ya kitaalam.

Chenge: Ni kosa la barabarani sasa sijui ulitaka anyongwe

Babu Seya: Ameharibu watoto wa watu
 
Tutajie japo Jaji mmoja ambaye viwango vyake japo vinakaribia vya Judge Lugakingira.

Mkuu wakati huo ni wakati huo sijui kama utarudi! Pamoja na hang over ya chama kimoja kushika hatamu lakini Jaji Luga alikuwa firm. Sasa hivi ambapo tunasema tuna demokrasia na uhuru mpana ndio unakuta judiciary inashutumiwa kwa uegemezi!
 
(4) RCs & DCs

  • RC wa Arucia
  • DC wa Igunga TABORA
  • ...
Kwa hali hiyo nchi itazama.


Kwenye bold ndiyo wapi Mkuu? Of all DC's.... Mnari (aliyewaramba bakora walimu) was the best.

Utapajuwa tu ukisoma kama unavyosoma jina la "Malecela" wa Dom.
Huyo Mnari is a typical sample of the DCs na RCs tulionao hivi sasa. Mimi binafsi simpendi kiongozi anayeweza kufikia uamuzi (nje ya sheria) wa kudhalilisha kwa kuchalaza viboko wanaume/wanawake wazima mbele ya wanafunzi wa shule kama alivyofanya huyo DC wa Bukoba. 1. Hafuati sheria yoyote (sawa na yule mama DC wa Igunga) 2. Maamuzi ya kibabe na yasiyokuwa namasirahi kwa umma 3. Hana training yoyote ya uongozi (kama Nape)
 
Mkuu wangu kinachonitisha ni haya majina wanayoitana. Unajua kama waalimu wanaoitwa Vodafasta tunajua kuwa wamepelekwa wakasoma fasta fasta na matokeo yake tunayaona. Sasa kama watoa haki nao ni fasta fasta matokeo yake ni nini?

Hukumu ya Lema na Zombe!!!:A S kiss:
 
Wangu hata mie hiyo makala nimeiona, ukweli inasikitisha sana kuona sasa Judicial system kwisha habari yake, na hiyo ni kutokana na hawa jamaa(majaji) kuwa presidential appointees, lazima wafanye kazi kwanza wakihakikisha wanalinda maslahi ya aliye wateua, na mwisho ndipo wewe na mimi tushughulikiwe na si kupewa haki. Jambo hili halina dawa kwa sasa mpaka tutakapo kuwa tumepata katiba mpya ambayo itatoa mwongozo wa kuwapata majaji. Tunashukuru hukumu ya kesi ya Lema ambayo imefumbua macho wengi japo watu walikuwa wakihoji kimya kimya weledi wa majaji wetu. Yaani inatia hasira kiasi ikitokea ukawa raisi unaweza kuwapiga chini majaji wote iwapo sheria ingeruhusu na kuajili upya kwa interview kali wao pia wakipewa fursa ya kuomba ajira hiyo na kampuni maarufu zinazo jali credibility kufanya kazi hiyo ndipo bunge liridhie. Watu wengine ambao wanapaswa kupigwa chini kama alivyo fanya raisi mpya wa Malawi ni kupiga chini IGP, RCs,DCs, na hata mkuu wa majeshi sababu amewafanya wanajeshi wetu wamekuwa mbumbumbu pasipo kuona maslahi ya taifa yanaporwa wao wako kimya tu! au kwa sababu wanauziwa bia na bidhaa nyingine kwa bei ya chini! Waangalie mfano wa nchi ya Mali na kwingineko. Nadhani imefika wakati wa askari wa vyeo vya chini kuchukua hatua kwa sababu wao ndio wamewahi kushinikiza mabadiliko haswa katika nchi nyingine. Wakikaa kusubiri tu amri hata za kishenzi ndipo tunazidi kuwaona hamnazo. Wasidhani hata siku moja IGP,mkuu wa majeshi na wenzake watakuwa upande wa wanyonge kwa sababu wao ndio wanafaidi inchi na mafisadi, inabidi ifike wakati waasi na wakatae amri za kishenzi, inakuwaje mtu anakataza watu wasiandamane na wewe unaye pewa amri ukawadhibiti unajua kuwa ni haki yao kikatiba na sheria inasema hivyo? hseria gani hiyo wanayo simamia? ya magamba au? oneni wenzenu Misri na Tunisia walicho fanya na mjifunze. Ipo siku mtafanya maafa na hao wanao watumeni watawaruka kwenye mkono wa sheria. Mfano huo umetokea Rwanda, askari wengi wamejikuta na kesi za kuhusika katika mauaji ya kimbari pasi kutetewa na walio watuma wakati walikuwa wanatimiza amri wanazodai ni halali. Lazima muwe na uwezo wa kuangalia kuwa je, ninacho amriwa kufanya ni kwa mujibu wa sheria? Mie wakati mwingine nashawishika kufikiria kuwa labda ni kutokana na uwezo mdogo wa kufikiria na kuchambua mambo wa askari wetu ambacho nadhani kinachangiwa zaidi na elimu ndogo sababu wengi ni Darasa la saba na walio feli kidato cha nne. Kwa hiyo wanaona iwapo watashindwa kutii amri watafukuzwa kazi na hawana uwezo wa kupata kazi mahali pengine. Unganeni na jeshi la umma la ukombozi tukomboe nchi yetu kwa kukataa kutii amri ambazo hazina tija kwa taifa, kwani kazi ni kuwa polisi au mwanajeshi tu? uiacha au ukafukuzwa utakufa? mnatutia aibu kwa mawazo mgando.
Ngoja nikupe Kifupi nimekulia na kuishi kambini mpk juzi tu nimeanza kujitegemea na bado natembelea coz ndugu zangu wapo humo kwny MAkambi ya Jeshi, ktk sehemu ambazo ccm haikubaliki ni Jeshini, ila na hata 2010 ccm walipata kura chache kuliko maelezo ktk makambi ya Jeshi nao wanajua tatizo wale jamaa nidhamu kwa sana but ukikaa nao hadi wazee wanapinga ccm live vijana ndio hawataki kuickia cdma inakubalika kuliko hama chochote na kuhusu elimu ur wrong ckuhizi hakuna std 7 anayechukuliwa na wengi wamejiendeleza, again maduka yasiyolipiwa kodi yanauza bidhaa feki tena bei juu na ni vichaka vya wahindi kuingiza bidhaa bila kodi then kidogo tu ndio hupelekwa ktk maduka hayo. Cku hizi huko majeshini full ufisadi c mlisikia jamaa anamiliki fungu la kutisha Kwa Madib?
 
Mkuu wangu kinachonitisha ni haya majina wanayoitana. Unajua kama waalimu wanaoitwa Vodafasta tunajua kuwa wamepelekwa wakasoma fasta fasta na matokeo yake tunayaona. Sasa kama watoa haki nao ni fasta fasta matokeo yake ni nini?
Nionavyo, tunaopaswa kuwalaumu wala si majaji. Hawa ni matokeo ya mfumo mbovu. Na ukichunguza kwa kina utabaini kuwa tatizo hili halipo miongoni maw majaji tu. Hay a ni matokeO ya mfumo mbovu ambao unazalisha wanataalamanwa majina tu na wall taalama Yao haioneKani katika weledi wao
 
Nionavyo, tunaopaswa kuwalaumu wala si majaji. Hawa ni matokeo ya mfumo mbovu. Na ukichunguza kwa kina utabaini kuwa tatizo hili halipo miongoni maw majaji tu. Hay a ni matokeO ya mfumo mbovu ambao unazalisha wanataalamanwa majina tu na wall taalama Yao haioneKani katika weledi wao

Mkuu basi nchi imefika pabaya. Kwa maana hiyo unasema kila mtaalam wa nchi hii hatendi kitaalamu? Hivi kweli kabisa nchi haina watu weredi?

Kwa hiyo kupata haki Tanzania ni bahati na sibu?
 
Nchi ya tatu kwa umasikini duniani, sasa tunajiongeze matatizo namna hii. Maana maskini haki yake anaitegemea mahakamani. Au kwa sababu Tanganyika haipo. Mungu tusaidie.
 
Nchi ya tatu kwa umasikini duniani, sasa tunajiongeze matatizo namna hii. Maana maskini haki yake anaitegemea mahakamani. Au kwa sababu Tanganyika haipo. Mungu tusaidie.

Mkuu hili suala si la masikhara hata kidogo. Hapa tunaongelea watu kutolewa uhai kwa Jaji kusema tu kwamba huyu ana hatia ya mauaji! Umasikini wetu hadi kwenye haki!
 
Binafsi sioni tatizo la Judge kuteuliwa na rais, ila tatizo ni pale rais anapokuwa na final say kwenye teuzi. Kwa mfumo wa jumuiya ya madola ni kwamba rais ana uwezo wa kuteua Judge ila hana uwezo wa kumfukuza kazi. Kitu kibaya zaidi walichokifanya CCM kumuongezea rais madaraka ni pale wateule wa rais (RCs and DCs) wanapokuwa katika ethical committees za majaji na mahakimu. Hii inamrudishia rais power of hire and fire(indirectly by ordering his apointees) a judge.

Wale wanaojiita learned brother wanasheria walikuwa kimya na kumwacha Tundu Lissu akiwapigania bungeni juu ya upuuzi huu.

Kama Judge atateuliwa na rais na kisha kuwa vetted na Public kwa kamati ya bunge ya sheria kutangaza publicly mwenye habari yoyote inayomdisqualify mteule aile na kisha kufanyika on Camera hearing na kamati kumpigia kura akipita jina linapelewa Bungeni kwa approval ya wabunge wote na akiishakuwa approved kazi yake inakuwa ni life tenure (ili asifikirie kuwa akistaafu atahangaika na hivyo kuridhisha wanasiasa) mpaka atakapoamua kujiuzulu mwenyewe. Hii itafanya mahakama kuwa huru zaidi.

Hii inawezekana pia kwa bunge kuwa full time lisilo na posho za vikao. Bunge linafanyiwa recess tu kwa vipindi fulani ila linakuwa active for the rest of 5 years. Hii inawezekana pia kwa kuwaondoa mawaziri kuwa sehemu ya bunge, mawaziri wangekuwa wanaitwa na kamati za bunge kwa ajili ya hearing za mambo yanayohusu maeneo yao na kuwaacha wabunge wakiendelea na kazi yao. Mswada si lazima uletwe na mwansheria mkuu, mbunge yeyote yule anweza ku-sponsor a bill na kuileta bungeni kama ikipita basi anapelekwa rais ambaye anakuwa hiyari ya kuisaini ama la, ila pia bunge liwe na power ya ku-overturn presidents veto kwa kutaka at least 70% ya wabunge wote kuupigia kura mswada pale anapoukataa.

Ila mfumo huu wa kuchukua majaji wastaafu na kuwapatia kazi baada ya kustaafu kama unyeviti wa tume mbalimbali ni njia mojawapo kuu ya kuua uhuru wa mahakama. Majaji wengi wanafanyakazi kuwapendezesha wateule ili wanapostaafu wafikiriwe badala ya kusahauliwa. Hapo ndipo ugonjwa wa siasa unapowapata.

Nakumbuka Judge Bomani alipokuwa anagombea urais mwaka 1995: Nyerere alimuuliza kuwa aliona wapi judge kugombea nafasi ya urais?. Nyerere aliona mbali sana, kuwa kama wataruhusu upuuzi ule basi siasa zitahamia mahakamani na ndiyo kitu kinachofanyika leo baada ya majaji wastaafu kuteuliwa kwenye nafasi za kisiasa.

Tunao majaji wengi sana ambao baadae waligeuka kuwa wanasiasa kama vile Joseph Sinde Warioba, Masilingi ambao kwa nyakati tofauti wameshikilia nafasi katika mihimili yote yaani mtatu yaani serikali, bunge na judiciary. Tukiwa-burn majaji kushika nafasi za executives tutakuwa tumepiga hatua kubwa towards uhuru wa mahakama. Lakini vilevile tuwahakikishie maisha bora kwa uhai wao wote otherwise wataendelea kula rushwa na kupindisha haki.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Msisahau Jaji Augustine Shangwa ambaye ni kihiyo wa kawaida aliyeibuliwa na Mkapa ili kumshghulikia Mrema. Nchi yetu iko pabaya hasa kutona na utawala usio makini katika kufanya uteuzi. Kama tuna mawaziri vihiyo na wa hovyo tutashindwa kuwa na majaji hata madaktari? Tunawaandaa vipi kitaaluma?
 
guys where are we going, we need to find the chanjo as soon as possible. By the way kuna namna yoyote ya kuweza kutangua u-jaji wwa mtu iwapo nanashambuliwa na ugonjwa wa siasa?

After writing a new constitution the whole of the judiciary will have to be overhauled . We shall have to have a new chief Justice, Attorney General and High court judges who will be appointed on the basis of their integrity and merit using a transparent and credible vetting system which will be well detailed in the constitution. If our northern neighbours in Kenya have done it, we surely can and will do it too!
 
Mkuu Kimbunga. Idara ya Mahakama imekua inalalamikiwa sana kwa vitendo vya rushwa na kupindisha haki. Vinara wa matendo haya walikua mahakimu na makarani wa mahakama. Ni katika awamu hii ya nne rushwa na matendo mengine maovu tunaanza yasikia kwa wingi ktk ngazi ya majaji. Inadaiwa kuna watu wamepewa ujaji kwa vigezo vya ukada,urafiki,ngono na mtandao!! Eti kuna baadhi ya majaji wameshindwa hata kuamua kesi moja toka wateuliwe! Kuna haja ktk Katiba Mpya kuweka vigezo vya wazi jinsi ya kupata mahakimu na majaji wa mahakama zetu. Kwasasa ni aibu. Mimi nikimsikiliza Werema akijibu hoja Bungeni huwa najiuliza aliteuliwa vipi kuwa jaji na baadaye mwanasheria mkuu wa serikali!!!
 
Mkuu hao majaji ndio wamepewa jukumu la kusimamia katiba mpya! Hapa ni kweli inatakiwa tufanye kama Kenya manake wao waliamua kuanza upya kwenye judiciary wakapiga chini kuanzia Chief Justice hadi majaji wa mahakama kuu. Watu wakaomba na kuhojiwa hadharani na kama ulihukumu kakkesi kako huko nyuma kwa magumashi inakuwa hapo ndipo unapigwa chini mwanzoooni!

Rafiki zangu wapendwa, kama katiba mpya haitamuondolea rais mamlaka ya uteuzi wa majaji,mwanasheria mkuu, wakuu wa mikoa na wengine kadhaa basi nadiriki kusema kwamba haitakuwa na maana yoyote!
Matatizo yote(kwa sehemu kubwa) chanzo ni mamlaka makubwa aliyonayo rais, mtu mmoja tu tena binadamu kama mimi na wewe halafu eti yeye ndo final!
 
Back
Top Bottom