Inategemeana ni maendeleo yapi yanayoongelewa, lakini Shinyanga ni kubwa sana na imeendelea kuliko Kahama. Kahama imeendelea kibiashara na mzunguko mkubwa wa pesa, pia watu wengi.Shinyanga ni mji mkubwa kieneo imesambaa sehemu kubwa. Pili Shinyanga Miundombinu ni mingi kuanzia barabara ni nyingi sana za lami pia ambazo sio za lami zimechongwa vizuri nakuwekwa molamu mpaka pembezoni, ina madaraja mengi na ya kisasa ya watembea kwa miguu na ya kawaida,masoko makubwa mengi(kambarage,nguzo nane, soko kuu,lubaga,ngokolo,ibinzamata nk).Mpangilio wa mji pia ni mzuri ukiwa na bustani za wazi za kutosha(mataa,karogho,ndembezi,mazingira center, balina, Ashi, jambo zoo, fresho nk, na maeneo ya michezo(kamabrage,fresho,risasi(basket).Stendi nzuri zaidi ya tano(stend ya zamani, manyoni, soko kuu, kambarage, lubaga sokoni na mpya inayojengwa katunda. Hospital kubwa Shinyanga zipo Tatu(hospital ya manispaa,hospital ya rufaa mwawaza, hospital ya kolandoto(bingwa kwa huduma za macho, ukoma, kifua nk kwa ukanda wa ziwa). Pia Shinyanga ina viwanda vikubwa baada ya mwanza vingi vimeamia Shinyanga, unapata bidhaa zinazofika ndani na nje ya nchi,.Uwanja wa ndege mkubwa wa kisasa ambao pia unatumika kama uwanja wa dharura kwa viwanja vingine vya ndege inapotokea dharura. Maji ya bomba yamesambazwa mpaka pembezoni na karibia kila familia ina bomba la maji, umeme pia mpaka pembezoni umefika, tambua pia umeme wote unaotumika kanda ya ziwa unasambazwa toka Shinyanga hivyo kuna umeme wa uhakika.Pia tambua Shinyanga ni mji wa kiutawala na Kahama ni mji wa kibiashara.