SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,244
- 4,258
Jamaa ana mpenzi wake, demu mmoja wa uswazi.
Ananieleza kwamba demu huyo ana mazoea ya kumtumia meseji mbili au tatu kwa siku akimsalimia au blah blah za kawaida za hawa mabinti, mara bebi naomba salio, mara naenda saluni naomba uniongezee hazitoshi.........nk.
Sasa jamaa ananieleza kuwa wiki iliyopita siku nzima hakupata meseji yoyote kutoka kwa bebi wake, ulipofika saa mbili usiku akampelekea demu huyo meseji kumsalimu na kumwuliza mbona kimya sana siku hiyo.
Haraka akajibiwa: Leo niko bize sana kwa bibi namsaidia kupalilia na nikimaliza naenda kwa mjomba nasikia yu mgonjwa.
Jamaa akashangaa kusikia hivyo kwani alitarajia vyote hivyo demu angemweleza badala ya kukaa kimya. Kwa hiyo jamaa akarudisha majibu:
Bebi mbona umekaa kimya hujanieleza yote hayo?
Demu akajibu: Hiyo nimekufanyia sapraiz bebi.
Jamaa amekuja kwangu analalamika ile mbaya.
Ananiuliza: Eti bro, sapraiz kwa mtu ndio inafanywago hivyo? Nami mambo ya kumfanyia mtu sapraiz sijui namna yake naomba jibu kwenu nikamweleweshe.