Hii ndagu ya kaburi wazi ni kweli au?

Number ni 26

JF-Expert Member
Apr 3, 2019
1,478
2,836
Heshima kwenu wakuu.

Niende kwenye mada. Leo nilikuwa na jamaa yangu wa kitambo toka wadogo tunabadilishana mawazo kidogo, sasa katika story za kuhusu maisha tukafikia kwenye mambo ya mafanikio "utajiri" aliniambia vitu vya kushangaza na kutisha, nikasema nije niwaulize je ni kweli? Hii kitu ipo huko?

Jamaa akaniambia kuwa kuna aina za utajiri zinapatikana maeneo karibu na mpakani mwa Malawi ambapo ukifanikiwa kuupata unakuwa "rich one" kweli ukwasi wa kutosha


1. Kaburi wazi
Huu unaitwa kaburi wazi, kwenye utajiri huu jamaa anasema mnatoka wewe na babu "mganga" mpaka ziwani mnapanda mtumbwi mpaka kilindini "kwenye kina kirefu" then babu anakwambia shuka kanyaga maji ufanye kama unapiga hatua vile ghafla utajikuta umetokea kwa wenye utajiri wao. Sasa hapo itabidi uwaeleze shida iliyokupeleka na wao watakubali ombi lako vizuri tu ila sharti lao utajiri wao unadumu kwa miaka 3 tu baada ya hapo utakufa utarudi kuwatumikia. Utakaa uko siku 3 then utaibuka kwenye maji pale pale mlipokuwa na babu na utamkuta anakusubiri, mtarudi kilingeni uoge dawa then usepe ukaishi zako miaka 3 ya utajiri wa kutosha. Huu hauna kutoa kafara, hapa kafara ni wewe mwenyewe

2. Kuishi na jini
Huu masharti yake ni kwamba unaenda kwa babu anakupa kwanza mtihani wa kuishi na mwanamke mzuri sana ambae ni jini kwa muda wa mwezi 1 bila kusex then ukimaliza huo mwezi unarudi kwake anakufungisha ndoa ndo anakuwa mkeo moja kwa moja. Sasa hilo jini anakupaje?, yeye babu atakwambia rudi na njia uliyokuja nayo mpaka kwako (ghetto) jifungie ndani baada ya muda fulani utasikia hodi sauti ya kike amka fungua mlango aingie then funga, usiongee nae chochote hata kama akikusemesha kausha kimya endelea na mambo yako. Humo ndani itabidi muishi kama mume na mke ila usimsemeshe kitu atakuwa anaongea yeye tu we kazi yako kumsikiliza anataka nini umletee kwa muda wa mwezi 1 na hakuna mtu atamuona wala kusikia sauti yake zaidi yako wewe, atakuwa anafanya majukumu yake yote kama kupika, kufua, kudeki, kuosha vyombo nk.

3. Kunywa maji ya ziwani
Huu anasema unaenda kwa babu anakupa ndele ya utajiri na sharti la kutokunywa maji haya tunayotumia sisi wengine mfano ya dukani, bomba, kisima nk... Wewe maji yako ya kunywa yatakuwa ya ziwani tu! Sasa utaona mwenyewe upo karibu na ziwa gani uwe unaenda kujaza ndoo yako unachill nayo mjengoni ila hayatakiwi kukaa zaidi ya siku 7, hapo utajua mwenyewe kama utaweza kufata maji ziwani kila week Mwanza to Dar .

4. Kukusanya maji waliotumia watu kwenye misiba au sherehe.

Kwenye huu utajiri masharti yake ni kwamba unakuwa kila baada ya muda fulani unafanya event iwe kwako au kusaidia watu jambo lao lakini cha muhimu watu wale chakula, sasa yale maji wanayonawa ndo utajiri wako huo.

Hayo ndo aliyonieleza jamaa yangu kwamba hizo ndele zipo huko karibu na mpakani mwa Malawi.

Sasa nikasema ngoja nije kuuliza wenyeji wa maeneo hayo je ni kweli?

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom