Ni Kweli Hii ni Sapraiz?

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,257
Jamaa ana mpenzi wake, demu mmoja wa uswazi.
Ananieleza kwamba demu huyo ana mazoea ya kumtumia meseji mbili au tatu kwa siku akimsalimia au blah blah za kawaida za hawa mabinti, mara bebi naomba salio, mara naenda saluni naomba uniongezee hazitoshi.........nk.

Sasa jamaa ananieleza kuwa wiki iliyopita siku nzima hakupata meseji yoyote kutoka kwa bebi wake, ulipofika saa mbili usiku akampelekea demu huyo meseji kumsalimu na kumwuliza mbona kimya sana siku hiyo.
Haraka akajibiwa: Leo niko bize sana kwa bibi namsaidia kupalilia na nikimaliza naenda kwa mjomba nasikia yu mgonjwa.

Jamaa akashangaa kusikia hivyo kwani alitarajia vyote hivyo demu angemweleza badala ya kukaa kimya. Kwa hiyo jamaa akarudisha majibu:
Bebi mbona umekaa kimya hujanieleza yote hayo?
Demu akajibu: Hiyo nimekufanyia sapraiz bebi.

Jamaa amekuja kwangu analalamika ile mbaya.
Ananiuliza: Eti bro, sapraiz kwa mtu ndio inafanywago hivyo? Nami mambo ya kumfanyia mtu sapraiz sijui namna yake naomba jibu kwenu nikamweleweshe.
 
sio mwambie yaan wewe na yeye ni ndege mnao fanana kwa hiyo someni kwa bidii mkikua mtajua wenyew bila kuuliza uliza vitu kama hivyo visivyokuwa na maana.
 
Saa 2 usiku anamsaidia bibi kupalilia ???? Embu punguzeni kutulisha chai mchana
 
Huyo dem hadi anapalilia duuh ananikumbusha dem wangu mmoja Manchali uko alikua analima balaa ila ndo mikono akikuahika dushe kulichezea natoka na maumivu kama nimepigwa msasa
 
Mnatufuturisha mchana jamani na chai zenu.. Mods ebu angalieni hili pia
 
sio mwambie yaan wewe na yeye ni ndege mnao fanana kwa hiyo someni kwa bidii mkikua mtajua wenyew bila kuuliza uliza vitu kama hivyo visivyokuwa na maana.
Mkuu, huwa hiyo picha yako inanikwazaga sana basi tu... Yani ni kama unafurahia hali ya huyo mtoto mwenye viraka. Siku si nyingi nitakublock...
 
Saa 2 usiku anamsaidia bibi kupalilia ???? Embu punguzeni kutulisha chai mchana
Mkuu, soma thread vizuri uielewe! Demu alipokuwa anamjibu jamaa, demu hakuwa shambani muda huo ila alimweleza aliyoyafanya na anayopanga kufanya kwa bibi yake.
 
Anajua maana ya sapraiz???
Aliyoyafanya demu,(kukaa kimya hiyo siku) demu anaona ni sapraiz kwa jamaa yake ila jamaa anaona hiyo si sapraiz, anakuja kwangu nimthibitishie hiyo siyo sapraiz.Nami nakuja kwenu mnieleze kama ni sapraiz kweli au sio.
 
Hivi kwa miaka hii tuliyo nayo ya utandawazi na mwendo wa smart phone kila sehemu bado kuna asiyejua maana ya surprise.

Duuh
 
Jamaa hampeni huyo demu kila siku aanzwe yeye tu kusalimiwa! hapo alikuwa anategwa aone kama na yeye atamkumbuka kwa siku hiyo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom