Ni kweli chadema inafadhiliwa na ujerumani kugomea muswaada wa katiba mpya na kuleta vurugu?

Kaduguda

JF-Expert Member
Aug 1, 2008
724
641
Wadau kuna mbunge wa Mtera kupitia CCM naona anafoka hapa bungeni na kutoa povu kwamba CHADEMA wanafadhiliwa na Ujerumani ili kupinga muswaada wa katiba mpya na kusababisha machafuko katika nchi hii. Naona huu kama uzushi usio kifani ambao una namna ya udaku fulani hivi! Na kama ni kweli basi kuna tatizo hapa! Vinginevyo hapa kuna umuhimu wa kuiomba serikali ya Ujerumani ilitolee ufafanuzi suala hili au huyu mbunge afute kauli yake.
 
Crap ! Mods toa upupu huu.
How comes this issue is crap King2? Hayo yamenenwa na mbunge wa Mtera ktk harakati zake za kuizodoa CHADEMA, ni vema tuwe wakweli ktk hili. Naona kama huyu jamaa kapitiliza na kaleta uzushi suio kuwa na kifani ambao pia ni hatari hata kwa Taifa letu. Kwangu haileti mantiki kwa nchi kama Ujerumani kuifadhili CHADEMA ili ichochee vurugu kwenye nchi kama yetu. Kwa minajiri ipi na ifaidike nini kukitokea vurugu Tanzania? Kwangu huu ni uzushi ambao sitaki kukubali, labda utolewe uthibitisho, vinginevyo Mh. Lusinde ameleta upotoshaji wa makusudi!
 
Tushasikia mengi na tutaendelea kusikia mengi. Kila aliye kwenye system anasema lolote analojisikia na kupongezwa. Wananchi tusipochukua hatua ya kuwakataa we're done.
 
mi nawashauri wabunge wa chadema wasililize kwa makini sana kauli na shutuma zinazotolewa na wabunge wa ccm then warudi kwa wananch kutufafanulia, NAJUA UONGO MWINGI UNAONGELEWA NA WABUNGE WA CCM ILI CHADEMA WAONEKANE WABAYA, CHADEMA WAJITAHIDI SANA KUWA WAKWELI KWA WANANCHI ILI KUWAUMBUA CCM.
 
ndo yale yale ya kuingiza makomandoo kwny uchaguzi wa Igunga knachotakiwa kufanyika waamng'ang'anie athibitishe au afute kauli yake
 
CCM acheni kutapatapa! Mtatoa kila sababu, mara makomandoo, mara nini mwisho mtasema na alshabab
 
We subiri tu utaona sasa hivi atafuta kauli yake na kuomba msamaha. Ngoja wajerumani waipate official uone atavyoogopa huyo magamba anyebwabwaja bila breki.
 
We subiri tu utaona sasa hivi atafuta kauli yake na kuomba msamaha. Ngoja wajerumani waipate official uone atavyoogopa huyo magamba anyebwabwaja bila breki.

Kwa jinsi alivyoongea pumba naona afadhali ya Mzee Malecela alipokuwa akiongoza hilo jimbo la Mtera kuliko huyu kilaza! Nawapa pole sana wananchi wa Mtera kwa kuwa na mbunge wa aina hii, hasara tupu!
 
Kweli siku ya kufa nyani ,nyani mwenyewe huteleza na cyo miti huteleza.
Kwan kila washikapo ccm sasa hiv wanateleza.
 
Hivi kwa suala kama hili tutegemee nini kutoka kwa vyombo vyetu vya usalama??
Hivi kweli huyo Lusinde atawekwa kitimoto ili aelezee kwa undani hayo madai yake ikibidi atoe vidhibitisho??
CHADEMA hapa inabidi wachukue hatua gani?? kwani sidhani taarifa kama hizi wanapaswa kuziacha zipite tu na kwa vile ni chama makini najua watachukua hatua!
Hivi huyo spika wa bunge Kihiyo alizitolea tamko gani hizo taarifa?? mi sikuwa nikifatilia bunge tafadhari!
 
Ni kweli hata mimi nimeona na kusikia kubwabwaja kwa mbunge huyo. Masikitiko yangu ni namna Spika Makinda atakavyofukia suala hili bila kumbana mbunge huyo kuthibitisha kauli zake kwa lengo la kulindana. Hakika angekuwa Mbunge wa CHADEMA amesema hivyo dhidi ya CCM ungeona spika huyo kushupalia kuwa ni kutarisha mahusiano ya nchi na hivyo mbunge afute au athibitishe kauli yake. Kweli nchi yetu inaenda kubaya chini ya utawala wa CCM. Katiba mpya ndio suruhisho la wanyonge.
 
Back
Top Bottom