Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 874
Tunafurahia kupata hostel mpya za kulala wanafunzi pale Udsm. Ni sawa. Tumefahamishwa kuwa kuna flat 20 zenye floor 4 kila moja.
Mimi sio mtaalamu wa majengo. Lakini wataalamu wa majengo wanaweza kweli kututhibitishia kuwa hizi bilioni kumi ndio halisia? Ukiangalia kwa ukaribu unapata shaka. Naamini kuna hela imezidi Ila kwa vile mkuu alishatamka hicho kiasi basi TBA wamelazimika kuendelea kukariri bilioni kumi.
Jé wasimamizi wa mradi huo walikuwa hawalipwi? Bodi ya ukadiriaji majenzi ina standard zake katika kujenga Jengo lolote. Nina amini ipo siku tutapata uhalisia wa gharama hizo.
Kuna athari kubwa ya kutokuwa wakweli katika mradi huo. Athari yake ni kuwa kila jengo litakalojengwa nchini kama litapita gharama hizo basi wataambiwa wameweka chá juu. Tuliona hili kule Simiyu. Rais alikataa Jengo lenye kukadiriwa hela nyingi. Akatoa mfano wa bilioni kumi katika mradi huu wa mabweni ya udsm. Wataalamu watakuwa na woga kuleta gharama halisi zá majengo kwa hofu ya kuambiwa wameweka chá juu.
Tunahitaji kupata majengo haya kwa gharama nafuu lakini isiwe chini ya nafuu. Natoa wito wakadiriaji majenzi waje hapa kutupa standard zao zikoje kwa majengo kama haya. Wasiogope kusema ukweli.
Flat 20 ina maana kila flat iligharimu shilingi milioni 500. Jé flat moja lenye floor 4 gharama yake ni milioni 500? Na hapo hapo wakajenga na uzio. Sitaki kufurahia tu kupata majengo haya lakini lazima gharama halisi zionekane.