Ni kweli Anna Makinda ni 'Mbabe'?

Joka kuu nina hasira sana na huyu mama kiukweli lakini imebidi nicheke tu kwamba akiulizwa kuhusu vigogo atasema ni vipande vya miti .. huu umetoa mfano mzuri sana maana nilikuwa nikijaribu kufikiria niandike kitu gani kieleweke kwa urahisi but thanx that u made it clear.

Fisadi ni mwinzi wa wake za watu!!!

Hili ni jibu la kutaka kuzingua tu watu ndiyo majibu ya kisanii hayo.

Anajua fika kabisa nini maana ya neno fisadi katka Tanzania ya leo.

kwa maana nyingine hilo ni jibu la mipasho zaidi.
 
Wa kuwashangaa ni wale wanaomshangaa huyu spika wetu mpya. Actually, hii ndio sababu iliyomfanya achaguliwe. Msije mkashangaa neno ufisadi likapigwa marufuku kutumika bungeni.
 
- You know what, tutalipeleka pabaya sana hili taifa kama tutadai kujua the meaning ya neno ufisadi as we want ndio should be our litimus test ya nani kiongozi anayefaa na asiyefaa, wananchi tufike mahali tukubali kwamba somebody had to be a new Speaker baada ya Mh. Sitta,

- Na ilikuwa ni lazima atoke kwenye chama chenye majority bungeni in this case CCM, sasa tumpe nafasi Spika mpya afanye kazi yake mpya kwanza ndio tumuhukumu!

William.

Mkuu William huhitaji kujenga fikra kwa mtindo wa vipande vipande. Hapa hajadiliwi Anne Makinda wa 2010 tu, sisi wengine tunamfahamu tangu akianza ubunge 1975 (Sijui ulikuwa wapi?). Tabia mbaya za Makinda si suala la kusubiri, wanaomfahamu wanamfahamu, bahati mbaya wengine mnaanza kumwona Makinda kwenye uspika na ndiyo maana mnasema tumwache afanye kazi ndo tumhukumu. Hivi William hujui hata kuwa Makinda alikuwa naibu spika? Au unadhani mtu akishakuwa spika anakuwa mwingine tofauti na alivyokuwa naibu? Fungua macho mkuu.
 
Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.

namkumbuka sana mwalimu wangu wa kiswahili pale azania sec.....kuna lugha maalu kwa semu fulani, kwa mfano hotelini....wali ng'ombe, na muhudu anaelewa nini kinachozungumziwa kwa ufasaha kabisa.
sasa huyu mama alikuwa anajua ufisadi ambao waandishi wa habari waliokuwa wanauulizaa sema kwa makusudi tu akalikimbia swali, sina la kusema hii ndio Tz na hawa ndio viongozi wetu.
 
Fisadi ni mwinzi wa wake za watu!!!

Hili ni jibu la kutaka kuzingua tu watu ndiyo majibu ya kisanii hayo.

Anajua fika kabisa nini maana ya neno fisadi katka Tanzania ya leo.

kwa maana nyingine hilo ni jibu la mipasho zaidi.

Unfortunately, neno fisadi lilikuwepo toka zamani sana, japo limekuwa likitumika sasa miongoni waTanzania na Wakenya kumaanisha walarushwa na wabadhirifu. Hata hivyo, bado kamusi ya kiswahili inaonyesha kuwa maana ya ufisadi ni utongozaji, uzinzi na mambo yanayoendana na hayo. Ukiangalia kwa makini, kwenye maana, na kwa kufuata kiswahili sahihi, neno fisadi tunalitumia visivyo.
 
Huyu speaker anafanya utani kwenye mambo ya msingi!Ina maana jinsi neno FISADI linavyotumika kisiasa hajui hadi aulize ati maana ya fisadi nini?
huyu ni mwongo tena ni hatari,kila mtu anajua FISADI ni wezi wa mali ya umma(Manyangau yenye njaa na tamaa ya walipa kodi)!
Uki niambia Maasai wa MONDULI kwa EL hajui maana ya fisadi naweza kukuelewa kidogo kwa maana wao EL alivyo jiuzulu walishangilia na kusema EL amepewa cheo kipya kikubwa sana kinaitwa FISADI na pinda anarepoti kwake,wakamlaki kwa zulia jekundu kama mfalme!!

Lakini kwa makinda kujitoa akili na kusema hajui neno fisadi nini zaidi ya alivyo tafsri ni uongo.
 
Asante Jokakuu kwa mfano mzuri unaojitosheleza sana.. Kukwepa swali lenye mantiki kwa kuangalia ufasaha wa lugha au uasili wa msamiati uliotumika ni njia iliyopitwa na wakati katika ulimwengu huu. Ingekuwa vigumu kuendesha vikao vya kimataifa kwa staili ya huyu mama(kuwa mtaalam wa lugha badala ya kujibu point iliyopo) kwa kuwa lugha hutofautiana sana pamoja na kuwa na wakalimani kwa kuwa baadhi ya misamiati katika lugha fulani inaweza isiwepo kabisa katika lugha nyingine.Mtanzania wa leo akidai hawajui mafisadi kwa kuwa maana ya asili ya neno ni mwizi wa wake za watu kweli tutegemee wanaokwapua fedha za umma/au kujihusisha na rushwa watafutiwe jina jipya ili aelewe tunamaanisha nini? Sasa hii vita dhidi ya ufisadi inazimwa kwa "utaalamu wa lugha" na siasa nyepesi.
 
Sijaipata, huyu mama kasemaje tena? I hate her, inabidi 2015 tukaweke kambi jimboni kwake mpaka ang'oke

Hii ilikuwa ni 7th July 2008

Makinda ashangaa mafisadi kusafishwa

na Godfrey God, Iringa
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda amewakoromea baadhi ya wabunge na watu wanaofanya kazi ya kuwasafisha mafisadi kuacha mara moja kwa madai kuwa hawawatendei haki Watanzania wenzao.

Makinda ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Kusini, alitoa kauli hiyo nzito jana wakati akiwasalimia wapiga kura wake katika Kata ya Njombe Mjini kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru.

Ametoa kauli hiyo kipindi ambacho Bunge limegawanyika makundi mawili, moja likiwatetea mafisadi, lingine likiwapinga huku likiishinikiza serikali kuchukua hatua.
 
- You know what, tutalipeleka pabaya sana hili taifa kama tutadai kujua the meaning ya neno ufisadi as we want ndio should be our litimus test ya nani kiongozi anayefaa na asiyefaa, wananchi tufike mahali tukubali kwamba somebody had to be a new Speaker baada ya Mh. Sitta,

- Na ilikuwa ni lazima atoke kwenye chama chenye majority bungeni in this case CCM, sasa tumpe nafasi Spika mpya afanye kazi yake mpya kwanza ndio tumuhukumu!

William.

sawa kabisa willium.

watu wamelewa na uchadema humu JF. kila kitu slaa, slaa!!! hivi hawa hata tukiweka ng'ombe atuongoze kwa dakika tano, hata huyo ng'ombe aking'olewa madarakani wataendelea kuimba ng'ombeee, ng'ombeee sijui mpaka lini? katika kiswahili fasaha, neno fisadi ni kama alivyofafanua mama makinda na si vinginevyo! hicho ni kiswahili na sio makinda, sasa hoja za kumshambulia mama wa watu zinatoka wapi na yeye ametumia kiswahili kama watu wengine? alaumiwe aliyeiba mke wa mtu kama yupo na si aliyefafanua maana ya neno fisadi kuwa lina maana ya mtu anayeiba mke wa mwenzie. ebo!!
 
Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.

Mkuu pasco duh fikiri kidogo mtu wangu..CCM walimsakama sana dr Slaa...na huyo mama itakuwa ni mjinga kama hakujua maana ya FISADI katika Tanzania ya leo....Hilo ni jembe kwa Dr. Slaa na samweli Sitta...Tz Kwishineri kama huyu mama ni Speaker....
 
Pasco,

..Mama Makinda ameulizwa kuhusu mafisadi kulingana na tafsiri ya neno hilo ktk siasa za leo za Tanzania.

..hivi ina maana akiulizwa kuhusu "vigogo" atasema ni vipande vya miti?

..hilo lilikuwa swali la mtego na kutokana na majibu yake amekwepa mtego mmoja na kutumbukia kwenye mtego mwingine.

..huyu ndiye anayedai kwamba amekuwa mbunge "maisha yake yote" halafu anashindwa kujibu maswali mapesi kama aliyoulizwa.

..so far naona kitakachomharibia Mama Makinda ni hii tabia ya kujibu maswali kwa jazba.

NB:

..Mama Makinda hakuwa kwenye timu ya kampeni ya uraisi ya Edward Lowassa mwaka 1995??

Wapi nagonga FIVE au Thanks mzee...maana huyo NG kachemsha....eti maana ya FISADI kwa tanzania ya leo ni mwizi wa wake za watu mbona maana ya mwizi wa mke wa watu tunajua toka long?
 
Wajameni, nilikuwepo kwenye hiyo press conference yake, aliposema mafisadi ni wezi wa wake za watu, hakumaanisha Dr. Slaa. Alikuwa akikanusha kutumwa na mafisadi na kusema kwanza hawajui hao mafisadi ni kina nani na kuuliza kwanza neno fisadi ni nini?. Ndipo akatoa tafsiri ya kamusi. Unachotakiwa wewe kufanya ni
kutafuta kamusi, soma neno fisadi ndipo ubishe alichokitamka mama Makinda.

Makinda ni mkorofi kama unabisha ,subiri tu utajaona mbele ya safari.hakuna haja ya kuandikia mate ,time will tell.mimi ntakukumbusha ukorofi wa makinda,na ipomifano mingi sana,ila kwavile hatuwezi kumuhukumu kwa makosa ya zamani ,na alikuwa hajawa speaker ,sasa ngoja utaona tu jinsi atakavyowahaibisha wanaomshabikia.
 
- You know what, tutalipeleka pabaya sana hili taifa kama tutadai kujua the meaning ya neno ufisadi as we want ndio should be our litimus test ya nani kiongozi anayefaa na asiyefaa, wananchi tufike mahali tukubali kwamba somebody had to be a new Speaker baada ya Mh. Sitta,

- Na ilikuwa ni lazima atoke kwenye chama chenye majority bungeni in this case CCM, sasa tumpe nafasi Spika mpya afanye kazi yake mpya kwanza ndio tumuhukumu!

William.

Ndio kaka, lakini sitta has been removed kwahila tu and thats the only trueth,maana mimi na wewe tunajua utendajikazi wake na hata wabunge wa vyama vya ccm na upinzani walipenda uongozi wake.lengo hapa siokumuondoa tu ,lakini kwa manufaa ya nani.ccm hawampendi mtu anaye stand for the benefit of majority,wanampenda mtu anayetetea uchafu na kuficha makosa.hakuna kisichokuwa na mwisho kaka ,hataukiangalia historia ya siasa za dunia hii,hakuna kisicho kuwa na mwisho .weekend njema kakaangu.
 
Babu yangu hajui maana ya neno KAMUSI, atasaidiwaje? Mh. Speaker hapaswi kuchukulia kuwa wote wanaomsikiliza wana kamusi au hata wanafahamu neno kamusi.

Neno fisadi ni zaidi ya MWIZI, ni zaidi ya JAMBAZI, ni zaidi ya MLAFI, ni zaidi ya mfanyabiashara ya madawa ya kulevya. Ukitaka kuelewa maana ya neno fisadi, fumba macho, fikiria ubaya wowote unaweza kusababisha maafa yasiyoelezeka. Ukishaipata hiyo hali, basi fumbua macho, huo ndo ufisadi. Fisadi ndo huyo mtu aliyenyuma yao. Speaker hapaswi kupata kigugumizi kuhusu neno FISADI.

Ukweli utawaweka HURU.
 
Kwa Kuunga mkono kauli za Sprka Anna Makinda na William Malecela,mwana JF Mtu Mmoja aliandika hivi;

"alaumiwe aliyeiba mke wa mtu kama yupo na si aliyefafanua maana ya neno fisadi kuwa lina maana ya mtu anayeiba mke wa mwenzie!!"

Mama Makinda muda mchache baada ya kushinda Uspika alisema hivi kuhusu maana nzima ya neno fisadi "Nijuavyo mimi neno fisadi ni wanaume wanaochukua wake za watu"

Lkn mwana JF Ndibalema kututhibitishia ugeu geu wa wa Spika Makinda katuletea kauli zake mwenyewe kuhusisha ufisadi na mtu yeyote anayetafuna maliasili za TZ kwa faida zao wenyewe na familia zao kama alivyosema hivi "Hii ilikuwa ni

7th July 2008 kwenye Gazeti la Tanzania Daima;

Makinda ashangaa mafisadi kusafishwa.

na Godfrey God, Iringa
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

"NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda amewakoromea baadhi ya wabunge na watu wanaofanya kazi ya kuwasafisha mafisadi kuacha mara moja kwa madai kuwa hawawatendei haki Watanzania wenzao.

Makinda ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Kusini, alitoa kauli hiyo nzito jana wakati akiwasalimia wapiga kura wake katika Kata ya Njombe Mjini kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru"

Hitimisho:

alishangaa MAFISADI kusafishwa?Ina maana alikuwa anashangaa wanaume wachukua wake za watu kusafishwa?Wanaume wachukua wake za watu waliwahi kujaribiwa kusafishwa na nani ktk TZ yetu?

Ndibalema you make my day,habari kama hizi zinaletwa na watu makini kama akina Ndibalema zenye shahidi juu ndiyo zinaipa heshima JF yetu!
 
- You know what, tutalipeleka pabaya sana hili taifa kama tutadai kujua the meaning ya neno ufisadi as we want ndio should be our litimus test ya nani kiongozi anayefaa na asiyefaa, wananchi tufike mahali tukubali kwamba somebody had to be a new Speaker baada ya Mh. Sitta,

- Na ilikuwa ni lazima atoke kwenye chama chenye majority bungeni in this case CCM, sasa tumpe nafasi Spika mpya afanye kazi yake mpya kwanza ndio tumuhukumu!

William.

Jamani nisaidieni, Malecela anaongea kama mtoto unayejifunza kuongea. Unaandika vitu visivyo na substance kabisa, yaani nakosa neno la kusema. Kama ni kiwandani ningesema ni makapi.
 
Mkuu William huhitaji kujenga fikra kwa mtindo wa vipande vipande. Hapa hajadiliwi Anne Makinda wa 2010 tu, sisi wengine tunamfahamu tangu akianza ubunge 1975 (Sijui ulikuwa wapi?). Tabia mbaya za Makinda si suala la kusubiri, wanaomfahamu wanamfahamu, bahati mbaya wengine mnaanza kumwona Makinda kwenye uspika na ndiyo maana mnasema tumwache afanye kazi ndo tumhukumu. Hivi William hujui hata kuwa Makinda alikuwa naibu spika? Au unadhani mtu akishakuwa spika anakuwa mwingine tofauti na alivyokuwa naibu? Fungua macho mkuu.

- Mkuu naomba nikubali kwamba tunaongelea Mama Makinda wawili tofauti, maana ninayemjua mimi toka akiwa Waziri wa ofisi ya Waziri mkuu hafanani na unayemsema, umeleweka sana. Yaaani kwa sababu amesema tafsiri ya fisadi kama anavyoijua basi hafai kuwa Spika,

- well ukishangaa ya Musa utaona mengine meng ya ajabu sana!

William.
 
Ndio kaka, lakini sitta has been removed kwahila tu and thats the only trueth,maana mimi na wewe tunajua utendajikazi wake na hata wabunge wa vyama vya ccm na upinzani walipenda uongozi wake.lengo hapa siokumuondoa tu ,lakini kwa manufaa ya nani.ccm hawampendi mtu anaye stand for the benefit of majority,wanampenda mtu anayetetea uchafu na kuficha makosa.hakuna kisichokuwa na mwisho kaka ,hataukiangalia historia ya siasa za dunia hii,hakuna kisicho kuwa na mwisho .weekend njema kakaangu.

- Mh. Sitta, amejaribu kugombea tena kiti chake ameshindwa ndio Demokrasia inavyosema, kushindwa ni kushinda tu sio anything-else, mawazo ya namna hii ndio yanasbabisha wanaoshindwa kuleta matatizo badala ya kukubali na kuruhusu Demokrasia ichukue mkondo wake!

William.
 
Back
Top Bottom