Hii ni hali inayoonekana kwa mfano wazi kwenye majiji mfano Dar es Salaam, ambapo wenyeji wengi, licha ya kuwa wamezaliwa na kukulia hapa, bado wanakutana na changamoto kubwa katika kufikia mafanikio.
Zaidi ya hayo, siku hizi hatuwezi kusema kuwa wenyeji wa Dar ni Wazaramo pekee kama ilivyokuwa zamani. Kwa sasa, jiji linajivunia wenyeji kutoka makabila mbalimbali, hasa wale waliozaliwa kuanzia miaka ya 70 na kuendelea.
Kwa upande mwingine, wageni wanaotoka mikoani, wameonyesha kasi kubwa ya mafanikio. Ingawa wameingia katika miji mipya, wanashangaza kwa namna wanavyoweza kuanzisha biashara, kujenga mali, na kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya kipindi kifupi. Kwa mfano, mtu mmoja aliyehamia jiji, kwa muda wa miaka 10-15, anaweza kuwa ameanzisha biashara inayostawi, kujenga nyumba, kumiliki magari, na kuwa na mtaji wa kutosha.