Ni kwanini viongozi wa upinzani wakiadhibiwa na chama wanakaidi ila wa CCM wakiadhibiwa na chama chao wanatii?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
753
1,000
Kuna swali nimejaribu kujiuliza kuhusiana na siasa zetu za Tanzania, mara nyingi vyama vimechukua hatua tofauti tofauti kwa wanachama wao.

Lengo kuu la hatua hizo ni kudumisha nidhamu ya chama na kuhakikisha kuwa chama kinabaki kwenye misingi yake.

Hata hivyo kwa kumbukumbu nyingi nilizonazo ni viongozi wachache sana kutokea upinzani ambao baada ya kuadhibiwa na chama walijirekebisha na kurejea kua wanachama watiifu badala yake wengi wao wameachana kabisa na siasa za upinzani.

Hali hiyo ni tofauti kabisa kwa wana-CCM ambao wakipewa adhabu aghalabu huitumikia na kurejea kuwa wanachama watiifu.

Hapa ndipo najiuliza kwani tatizo ni nini hasa?

Ni adhabu za maonezi zitolewazo na viongozi wa upinzani?
Ni kuhadaiwa na uongozi wa CCM?
Ni woga wa kuendesha maisha nje ya mfumo dola?
Ni kukosa uthabiti na umadhubuti wa kisiasa?
Au siasa ni ulaji tu hivyo tuache kuwashabikia wanasiasa kiuhalisia?

Naombeni mnisaidie kuwaza.
 

Ryaro ryaro

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
326
1,000
Maswali yote ya kwako ndio Majibu, hasa hasa mstari wa pili from your suggested answers. Mfano ni hao Wanamama -19 walioko bungeni Kimagumashi, however, wewe unajua kabisa CCM, chini ya Utawala wa Mwendazake walivyokuwa waoga wa siasa za ushindani"cowards leadership'. Pia naona umesahau kuongongeza sababu ya Njaa inayowakabili Wapinzani Uchwara inayoperekea kuuza utu wao kwa Wenye Mamlaka waoga.
 

Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,717
2,000
CCM huwa wanatii kwasababu:
M/kiti CCM ndio kwenye dola hivyo kama hujipendi USITII.Kuna kitu pale Lumumba kinaitwa maadili.

KAMA HUTAKI MUULIZE MBUNGE JESCA IRINGA kilichompata au wanairinga wakuhadithie.TII MAMLAKA Mnyonge wewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom