G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Huku kukiwa na lundo la tuhuma kuwa utawala wa awamu ya tano umegubikwa na ubaguzi wa kikanda hatimaye Rais John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika. Sherehe hizo kwa mara ya kwanza zinafanyika nje ya makao makuu ya nchi ukiachilia mbali serikali ilipohamia Dodoma.
Swali la msingi ni kwanini sherehe hizo ziende jijini Mwaanza eneo ambalo limetawaliwa na kabila atokalo Rais Magufuli? Ni hoja gani hasa iliyotumika kuzipeleka jijini humo?
Ni jambo la ajabu kuona serikali ikikumbatia waziwazi upendeleo wa ukanda! Haya yanayofanywa yanatupa sisi ari ya kujiridhisha kuwa tumetawaliwa na upendeleo wa waziwazi wa kikabila awamu hii ya uongozi.
Kwa maana hiyo sasa jeshi, viongozi wote wa juu pamoja na wageni wanapelekwa Mwanza ili kuhudhuria sherehe za uhuru.
Siwezi kusema mengine yaliyotokea huko nyuma katika utawala huu yakionyesha mwenendo mbaya wa kikabila ila kiukweli jambo hili halileti picha nzuri hata kidogo.
Hii ni Tanzania imejengwa ila kiobomoa ni kazi rahisi sana.