Ni kwanini 'Best IT Professionals in Africa' wanatokea Nigeria, Kenya na Senegal?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,683
Katika pitapita zangu nilikutana na huu mjadala mitandaoni ya kwamba katika bara la Africa, nchi zinazoongoza kuwa na best IT Professionals ni Kenya, Nigeria na Senegal ndio wanaotisha katika issues za IT.

Je, ni kwanini wenzetu wako vizuri katika maswala ya IT wakati sisi Tanzania tuna vyuo sio chini ya 500 wanavyofundisha course za IT kuanzia ngazi ya diploma, degree, masters lakini hata majirani Kenya wanatuzidi?

Je, ni kwanini Kenya, Nigeria na Senegal ndio wanaotisha katika maswala ya IT?
 
Elimu, na siyo ya kukariri, sio ya vyeti feki, ya kutafakari, kusoma na kuwa mbunifu...period
Kwa kuongezea tuu hapo mkuu ni kwamba vijana wengi walio ma vyuoni wanasoma ili wafaulu mitihani wapate vyeti ila wanashidwa kujiongezaa.
 
Wanasoma ili wapate kazi na sio kuwa wataalam wa hiyo fani.......Pia mazingira ya kufundisha hiyo course au iyo proffesiona l ni ya ujanja ujanja tu........Nenda DIT,UDOM pale Informatics utajua nini kinafanyika
 
Hivi DIT si ndio chuo kinachosifika KWA IT
 
Kenya ni more industrialized kuliko sisi na wazungu wanaitazama kwa jicho la kipekee sana.. Wanataka nayo iwe moja kati ya silicon valley za Africa kama wanavyofanya south africa. Nigeria wana wasomi wa IT kwa Miaka mingi sana, yani hata ajira za IT hamna tena na hata wizi wa mitandao africa Nigeria ndo wanashika kilele. Mtu ana masters ya IT anajiajiri tu anafuga farasi kazi hamna wakati kwetu sekta hii ndo inakua.
 
Kwenye hili pia kwa kiasi fulani aina ya wakufunzi wanaotumika kuandaa wanafunzi ni tatizo, aghalabu unakuta ni wale waliokuwa na G.P.A ya juu ndiyo wanabaki kufundisha chuoni hawajahi fanya kazi kwa vitendo kwenye sekta husika wakaona mambo gani yanayofanyika katika ulimwengu halisi, wanabaki kufundisha vitu ambavyo hata wenyewe hawavifahamu kiundani, walau wale ambao wanakuwa wamechukuliwa baada ya kufanya kazi kidogo wanakuwa na uelewa wa maeneo wanayoyafundisha sababu kuna tofauti kati ya kozi tunazosoma vyuoni na mambo yanavyofanyika katika uhalisia.
 
Naunga hoja asilimia miaa mkuu hapo
 
Back
Top Bottom