WanaJF!
Hivi karibuni Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa ulioenda kwa jina '2013 GLOBAL SMART PARTNERSHIP' ambao uliongozwa na rais Jakaya Kikwete uliofanyika hapa Dar es salaam. Mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali wakiwemo marais, mawaziri, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa na watu mashuhuri.
Ni mkutano ulioipa Tanzania heshima ya kipekee sana katika historia ya nchi yetu, hasa ukizingatia ujumbe wa mkutano huo na ajenda mbalimbali zilizo jadiliwa zenye kulenga kuiwezesha nchi yetu kufanya mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Jambo lililo nishangaza kwenye mkutano huo ni kukosekana kwa uwakilishi wa vyama vya siasa hasa vya upinzania, ukizingati mambo mengi yaliyo jadiliwa yana athiri taifa letu hasa kwenye nyanja ya teknolojia. Kwa vyama vingine sitaweza kuvijadili kwa kuwa ina semekana ni CCM-B, lakini ilikuwaje CHADEMA hakikushiriki?
Kama itakumbukwa, April 8, 2013, Dr Slaa alishiriki kwenye mkutano wa CEO Round Table, na nilimpa pongezi sana kwa kushiriki kwake kwenye mkutano huo, kwani ajenda ilikuwa inazungumzia 'PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP', ambayo ni ajenda nzuri na yenye tija kwa taifa. Lakini iweje hii ya GLOBAL SMART PARTNERSHIP asishiriki? ni kwamba serikali imemtosa au yeye hakupenda kujihusisha na mambo ya serikali?