Ni kwamba Dr Slaa katoswa au?

Ni kwamba Dr Slaa katoswa au?

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,830
WanaJF!

Hivi karibuni Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa ulioenda kwa jina '2013 GLOBAL SMART PARTNERSHIP' ambao uliongozwa na rais Jakaya Kikwete uliofanyika hapa Dar es salaam. Mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali wakiwemo marais, mawaziri, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa na watu mashuhuri.

Ni mkutano ulioipa Tanzania heshima ya kipekee sana katika historia ya nchi yetu, hasa ukizingatia ujumbe wa mkutano huo na ajenda mbalimbali zilizo jadiliwa zenye kulenga kuiwezesha nchi yetu kufanya mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Jambo lililo nishangaza kwenye mkutano huo ni kukosekana kwa uwakilishi wa vyama vya siasa hasa vya upinzania, ukizingati mambo mengi yaliyo jadiliwa yana athiri taifa letu hasa kwenye nyanja ya teknolojia. Kwa vyama vingine sitaweza kuvijadili kwa kuwa ina semekana ni CCM-B, lakini ilikuwaje CHADEMA hakikushiriki?

Kama itakumbukwa, April 8, 2013, Dr Slaa alishiriki kwenye mkutano wa CEO Round Table, na nilimpa pongezi sana kwa kushiriki kwake kwenye mkutano huo, kwani ajenda ilikuwa inazungumzia 'PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP', ambayo ni ajenda nzuri na yenye tija kwa taifa. Lakini iweje hii ya GLOBAL SMART PARTNERSHIP asishiriki? ni kwamba serikali imemtosa au yeye hakupenda kujihusisha na mambo ya serikali?
 
Uchoyo na Ulafi wa CCM utawakufuru... Huyu Rais Mwenyewe hana zaidi ya Miaka 2; na Unajua walikuwa ni Marais Mbalimbali lakini wa Kenya hakutokea; wa Rwanda zii; wa Malawi kapotea; kwahiyo Usifurahie kisichosimama...

Unafiki ndio KOSA
 
Mwulize mwenyeji wa mkutano. Yule profesa wa uchumi alialikwa?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Mkuu, si ndio hao mnawaita CCM-B? kama ndiohivyo hawakuwa na haja ya kushiriki kwani mawaziri wa serikali ya CCM walijaa kwa niaba yao watu wa CUF.
 
Uchoyo na Ulafi wa CCM utawakufuru... Huyu Rais Mwenyewe hana zaidi ya Miaka 2; na Unajua walikuwa ni Marais Mbalimbali lakini wa Kenya hakutokea; wa Rwanda zii; wa Malawi kapotea; kwahiyo Usifurahie kisichosimama...

Unafiki ndio KOSA
nngu007,

Sitaki kuamini kama Rwanda awakupata mwaliko ama Malawi, sina uhakika kama ni wanachama, ila Kenya dharura yake ilitangazwa. Sidhani kama serikali imefanya ulafi wa aina yoyote kwenye huu mkutano, ukizingatia watu mashuhuri wa hapa hapa nyumbani walikuwa wengi. Jambo la kushtua ni kwamba ilikuwaje watu wa muhimu na wenye ushawishi kwenye jamii kama Dr Slaa wasihudhurie?
 
Last edited by a moderator:
documents za kikao zipo kwenye dust bin pale airport VIP, zote ziliachwa wakati washiriki wakipaa mkutano huu ulikuwa ni INTERNATIONAL BUFFET IN TANZANIA kama ilivyo mikutano yote inayoandaliwa bongo, sema tu wakubwa wanakula zaidi ya buffet kwa kuongeza pesa za matumizi na kuunda kampuni za kuhudumia mkutano.

Phd kazakhstan , June 30th, 2013
 
Inaonekana wewe hujafatilia ajenda za kikao kile ndio maana unasema haya!

Kuna mambo mbalimbali yenye maslahi kwa taifa yaliyo jadiliwa, nikupe tu mfano;

Kuna teknolojia imetambulishwa nchi, inaitwa Tele Piercing, kama sijakosea, ila namna inavyofanya kazi ni kama ifuatavyo;

Teknolojia hii ni mahususi katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu nchini, kwani kifaa hicho kitafungwa kwenye mashule yapatayo 150 kote nchini, hasa zile zenye upungufu mkubwa wa walimu. Lengo hapa ni kuwezesha mwalimu mmoja, labda aliepo Dar, kuweza kufundisha watoto wote kwa wakati mmoja kwenye mashule yote 150 ambayo yamefungwa kifaa hicho.

Hivyo, kufanyika kwa mkutano huu kumeleta tija kubwa kwa taifa, na sio vyema kupotosha mkuu.
 
nngu007,

Sitaki kuamini kama Rwanda awakupata mwaliko ama Malawi, sina uhakika kama ni wanachama, ila Kenya dharura yake ilitangazwa. Sidhani kama serikali imefanya ulafi wa aina yoyote kwenye huu mkutano, ukizingatia watu mashuhuri wa hapa hapa nyumbani walikuwa wengi. Jambo la kushtua ni kwamba ilikuwaje watu wa muhimu na wenye ushawishi kwenye jamii kama Dr Slaa wasihudhurie?

HAMY-D Unajuaje? Wageni ni SIRI for SECURITY REASONS...
 
HAMY-D

Unaandika kitu ambacho hukijui lakini unajifanya unajua mwisho unaomba kujulishwa?

Shame of u!
 
Talking kuhusu kujifanya well informed, si ni wewe ndiye unajifanya unamjua Nyerere eti ni mzazi wako? na ukataka kupotosha watu humu waamini hivyo, ila baada ya kubanwa sawasawa ukaleta utetezi wako dhaifu ila bado ulikuwa na chembechembe za kutaka kukuhalalisha wewe kuwa mtoto wa Mwalimu, mkuu kwanini ulidanganya watu?

Mimi siwezi kujifanya najua wakati najua kuwa sijui, ndio maana kichwa cha huu uzi kina alama ya kuuliza! kama hujui maana yake hiyo alama, kiukweli siwezi kukusaidia.

ILA MKUU PUNGUZA UJUAJI, BINADAMU HATUKO HIVYO!
 
Unashangaza, hivi unaamini kuna kitu pale au ni sanaa? Dr wa ukweli hazundumzii mambo ya kufikirika sana. Wewe kila kitu ni Dr Slaa tuu,kwa taarifa yako mambo ya kisanii huwa hajihusishi. Haya huyo Mkulu wako ambaye hajui kwa nini nchi yake ni masikini ameongea nini? Mijadala yenye tija subiri after 2016 utaiona.
 
Talking kuhusu kujifanya well informed, si ni wewe ndiye unajifanya unamjua Nyerere eti ni mzazi wako? na ukataka kupotosha watu humu waamini hivyo, ila baada ya kubanwa sawasawa ukaleta utetezi wako dhaifu ila bado ulikuwa na chembechembe za kutaka kukuhalalisha wewe kuwa mtoto wa Mwalimu, mkuu kwanini ulidanganya watu?

Mimi siwezi kujifanya najua wakati najua kuwa sijui, ndio maana kichwa cha huu uzi kina alama ya kuuliza! kama hujui maana yake hiyo alama, kiukweli siwezi kukusaidia.

ILA MKUU PUNGUZA UJUAJI, BINADAMU HATUKO HIVYO!
Sawa kabisa wala hujakosea :clap2::clap2::clap2:
 
DR Slaa anajua ufisadi tu hamna kingine anachojua sasa kwenye mkutano wa kuongea teknohama angeongea nini? Labda angemwambia Josephine amuandalie desa , si nasikia mama Josephina ni mtaalam wa mifumo ya computer huwa anawatengenezea software Chadema makao makuu?
 
  • Thanks
Reactions: Ome
WanaJF!

Hivi karibuni Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa ulioenda kwa jina '2013 GLOBAL SMART PARTNERSHIP' ambao uliongozwa na rais Jakaya Kikwete uliofanyika hapa Dar es salaam. Mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali wakiwemo marais, mawaziri, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa na watu mashuhuri.

Ni mkutano ulioipa Tanzania heshima ya kipekee sana katika historia ya nchi yetu, hasa ukizingatia ujumbe wa mkutano huo na ajenda mbalimbali zilizo jadiliwa zenye kulenga kuiwezesha nchi yetu kufanya mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Jambo lililo nishangaza kwenye mkutano huo ni kukosekana kwa uwakilishi wa vyama vya siasa hasa vya upinzania, ukizingati mambo mengi yaliyo jadiliwa yana athiri taifa letu hasa kwenye nyanja ya teknolojia. Kwa vyama vingine sitaweza kuvijadili kwa kuwa ina semekana ni CCM-B, lakini ilikuwaje CHADEMA hakikushiriki?

Kama itakumbukwa, April 8, 2013, Dr Slaa alishiriki kwenye mkutano wa CEO Round Table, na nilimpa pongezi sana kwa kushiriki kwake kwenye mkutano huo, kwani ajenda ilikuwa inazungumzia 'PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP', ambayo ni ajenda nzuri na yenye tija kwa taifa. Lakini iweje hii ya GLOBAL SMART PARTNERSHIP asishiriki? ni kwamba serikali imemtosa au yeye hakupenda kujihusisha na mambo ya serikali?

Nakubaliana na hoja yako murua.
 
Ila ki-ukweli hapa HAMY-D ana hoja ya msingi. Inakuwaje vyama ambavyo vinapingania kuingia IKULU havishikriki katika shighuli nyeti kama hizi??? Inawezekana

(1) Ni uchoyo wa kijinga wa CCM au
(2) Ni upuuzi wa kijinga wa vyama vya upinzani kukataa kushiriki

Jibu ni lipi???
 
Uchoyo na Ulafi wa CCM utawakufuru... Huyu Rais Mwenyewe hana zaidi ya Miaka 2; na Unajua walikuwa ni Marais Mbalimbali lakini wa Kenya hakutokea; wa Rwanda zii; wa Malawi kapotea; kwahiyo Usifurahie kisichosimama...

Unafiki ndio KOSA

kwani hao uliowataja walikuwa na ulazima? Kwasababu mkutatano ulikwenda vizuri sana waliohudhuria walichangia ipasavyo sasa nyie haters mnaweza kupotea mkitaka hamieni Malawi; Kenya au Malawi.
 
Back
Top Bottom