Ni kwamba Dr Slaa katoswa au?

Ni kwamba Dr Slaa katoswa au?

Apo ni maendeleo au msiba wa taaluma?..mwalimu dar afu mwanafunzi tunduma?ee Mwenyez epushia mbali..

aepushie mbali maana baada ya watoto kusoma wataanza ku shangaa hizo screen
na hadi waje wazizoee itachukua mda sans......
sio jambo la kuchekelea hata kidogo kama afanyavyo HAMY-D
 
Last edited by a moderator:
WanaJF!

Hivi karibuni Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa ulioenda kwa jina '2013 GLOBAL SMART PARTNERSHIP' ambao uliongozwa na rais Jakaya Kikwete uliofanyika hapa Dar es salaam. Mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali wakiwemo marais, mawaziri, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa na watu mashuhuri.

Ni mkutano ulioipa Tanzania heshima ya kipekee sana katika historia ya nchi yetu, hasa ukizingatia ujumbe wa mkutano huo na ajenda mbalimbali zilizo jadiliwa zenye kulenga kuiwezesha nchi yetu kufanya mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Jambo lililo nishangaza kwenye mkutano huo ni kukosekana kwa uwakilishi wa vyama vya siasa hasa vya upinzania, ukizingati mambo mengi yaliyo jadiliwa yana athiri taifa letu hasa kwenye nyanja ya teknolojia. Kwa vyama vingine sitaweza kuvijadili kwa kuwa ina semekana ni CCM-B, lakini ilikuwaje CHADEMA hakikushiriki?

Kama itakumbukwa, April 8, 2013, Dr Slaa alishiriki kwenye mkutano wa CEO Round Table, na nilimpa pongezi sana kwa kushiriki kwake kwenye mkutano huo, kwani ajenda ilikuwa inazungumzia 'PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP', ambayo ni ajenda nzuri na yenye tija kwa taifa. Lakini iweje hii ya GLOBAL SMART PARTNERSHIP asishiriki? ni kwamba serikali imemtosa au yeye hakupenda kujihusisha na mambo ya serikali?

Duh upo mzee naona huachi kupost comments zako thidi ya CHADEMA inaonyesha kuwa ukilala huwa unaomba kukuche utoke na thread mpya, nakutakia kila lakheri kaka
 
NI MIKUTANO YA KIPUUZI AMBAYO MATOKEO YAKE HAYAJAWAHI KUONEKANA KATIKA MAISHA YA MTANZANIA, ZAIDI YA KUPEANA DEAL ZA KUGAWANA NATURAL RESOURCES ZETU, mkutano uliokuwa unazungumzia teknolojia huku ikiwa imejaa matatizo mengi ya ufundi, SHAME UPON JK( JINGA KUBWA)
 
Sasa si mngeulizana Lumumba hayo mambo kwani nyie si ndiyo watoa mialiko?
 
WanaJF!

Hivi karibuni Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa ulioenda kwa jina '2013 GLOBAL SMART PARTNERSHIP' ambao uliongozwa na rais Jakaya Kikwete uliofanyika hapa Dar es salaam. Mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali wakiwemo marais, mawaziri, wafanyabiashara wakubwa, wanasiasa na watu mashuhuri.

Ni mkutano ulioipa Tanzania heshima ya kipekee sana katika historia ya nchi yetu, hasa ukizingatia ujumbe wa mkutano huo na ajenda mbalimbali zilizo jadiliwa zenye kulenga kuiwezesha nchi yetu kufanya mapinduzi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Jambo lililo nishangaza kwenye mkutano huo ni kukosekana kwa uwakilishi wa vyama vya siasa hasa vya upinzania, ukizingati mambo mengi yaliyo jadiliwa yana athiri taifa letu hasa kwenye nyanja ya teknolojia. Kwa vyama vingine sitaweza kuvijadili kwa kuwa ina semekana ni CCM-B, lakini ilikuwaje CHADEMA hakikushiriki?

Kama itakumbukwa, April 8, 2013, Dr Slaa alishiriki kwenye mkutano wa CEO Round Table, na nilimpa pongezi sana kwa kushiriki kwake kwenye mkutano huo, kwani ajenda ilikuwa inazungumzia 'PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP', ambayo ni ajenda nzuri na yenye tija kwa taifa. Lakini iweje hii ya GLOBAL SMART PARTNERSHIP asishiriki? ni kwamba serikali imemtosa au yeye hakupenda kujihusisha na mambo ya serikali?
Mkuu ulishawahi kusikia Dr Slaa akiongelea masuala ya maendeleo na mawazo yake mbadala?

Kwenye upeo wake maendeleo haya exist, kwake yeye ni skandali tu, as if yeye hanazo.

Kwa suala la kualikwa tunamwombe Mh JK amlete Dalai Lama watakuwa na mengi ya kuongea na Slaa
 
Jamani, Pasco wa JF yuko wapi? ... Rais Kikwete alisema za mbayuwayu changanya na za kwako.

Hii ni kazi maalum
 
nngu007,

Sitaki kuamini kama Rwanda awakupata mwaliko ama Malawi, sina uhakika kama ni wanachama, ila Kenya dharura yake ilitangazwa. Sidhani kama serikali imefanya ulafi wa aina yoyote kwenye huu mkutano, ukizingatia watu mashuhuri wa hapa hapa nyumbani walikuwa wengi. Jambo la kushtua ni kwamba ilikuwaje watu wa muhimu na wenye ushawishi kwenye jamii kama Dr Slaa wasihudhurie?
Hili ni jambo la msingi sana. Hata majuzi kule Entebe, uhuru alikwenda kumtembelea Museven, lakini Museven akamualika rafiki yake Kagame ahudhurie mazungumzo yale.
Museven hakuialika Dar wala Bujumbura kwenye mkutano ule. Tunaweza kumuuliza Museven kwanini hakuialika Dar?

Kwenye swala hili kabla ya kurusha swali, ni lazima tujue washiriki walialikwa kwa mtindo gani? kulikuwa na mialiko? au ayejisikia alikwenda tu?
kama kulikuwa na mualiko, je vyama vya Upinzania vilialikwa? vingapi? wangapi walikwenda?
Pili, kwakuwa Dr. Slaa ndio Katibu mkuu wa CHADEMA, haimaanishi kwamba ni lazima yeye ahudhurie kwenye vikao vyote unavyotaka wewe. kama ilivyo kwa CUF, sio kila mkutano ahudhurie Prof. Lipumba.
 
JK anaofia slaha ataeleza jinsi serkali inavyong'oa watu kucha na meno

Hapo umepotea mkuu. Dr slaa hata kama angekuwepo kwenye huo mkutano angekuwa amehudhuria tu na si mshiriki. Hivyo asingepata hata sekunde ya kuongea
 
Inaonekana wewe hujafatilia ajenda za kikao kile ndio maana unasema haya!

Kuna mambo mbalimbali yenye maslahi kwa taifa yaliyo jadiliwa, nikupe tu mfano;

Kuna teknolojia imetambulishwa nchi, inaitwa Tele Piercing, kama sijakosea, ila namna inavyofanya kazi ni kama ifuatavyo;

Teknolojia hii ni mahususi katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu nchini, kwani kifaa hicho kitafungwa kwenye mashule yapatayo 150 kote nchini, hasa zile zenye upungufu mkubwa wa walimu. Lengo hapa ni kuwezesha mwalimu mmoja, labda aliepo Dar, kuweza kufundisha watoto wote kwa wakati mmoja kwenye mashule yote 150 ambayo yamefungwa kifaa hicho.

Hivyo, kufanyika kwa mkutano huu kumeleta tija kubwa kwa taifa, na sio vyema kupotosha mkuu.

hadi kijijini kwetu isole kitafika na kufanya kazi kweli? na kama kitafanya kazi kitakuwa na ufanisi kweli?
 
nngu007,

Sitaki kuamini kama Rwanda awakupata mwaliko ama Malawi, sina uhakika kama ni wanachama, ila Kenya dharura yake ilitangazwa. Sidhani kama serikali imefanya ulafi wa aina yoyote kwenye huu mkutano, ukizingatia watu mashuhuri wa hapa hapa nyumbani walikuwa wengi. Jambo la kushtua ni kwamba ilikuwaje watu wa muhimu na wenye ushawishi kwenye jamii kama Dr Slaa wasihudhurie?

Nimependa kwenye red
 
Inaonekana wewe hujafatilia ajenda za kikao kile ndio maana unasema haya!

Kuna mambo mbalimbali yenye maslahi kwa taifa yaliyo jadiliwa, nikupe tu mfano;

Kuna teknolojia imetambulishwa nchi, inaitwa Tele Piercing, kama sijakosea, ila namna inavyofanya kazi ni kama ifuatavyo;

Teknolojia hii ni mahususi katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu nchini, kwani kifaa hicho kitafungwa kwenye mashule yapatayo 150 kote nchini, hasa zile zenye upungufu mkubwa wa walimu. Lengo hapa ni kuwezesha mwalimu mmoja, labda aliepo Dar, kuweza kufundisha watoto wote kwa wakati mmoja kwenye mashule yote 150 ambayo yamefungwa kifaa hicho.

Hivyo, kufanyika kwa mkutano huu kumeleta tija kubwa kwa taifa, na sio vyema kupotosha mkuu.

Wewe ni mwalimu au unasema kufurahisha wana JF? Hiyo technology ya Tele Piercing haiwezi kutumika kwa shule zetu hata ukienda shule za hapo Dar ni vigumu kwa sababu zifuatazo:

1. Kiingereza kwa watoto wetu wote hadi waliopo vyuo vikuu ni tatizo kubwa na hivyo kama unajua vema walimu wengi wanafundisha kwa kiswahili na kuandika notice kwa kiingereza.
2. Mradi wa 'big results' haujaanza maana unafahamu teknolojia hiyo inahitaji umeme. Kwa sasa nchi yetu ina 19% ndo wanaopata umeme na umeme wenyewe hata ukiwa na saloon ya kunyolea nywele usipokuwa na standby generator utaliwa tu maana huwa hakuna ratiba maalum ya kukatika umeme. TANESCO wao wanayo ratiba lakini haifuatwi na kila mara utasikia kuna technical fault ilitokea mtuwie radhi.
3. Mtindo wa kufundisha kwa sasa ni students centred learning na teknolojia hiyo ni zaidi lecture method ambayo itafanya mambo yaende nyuma badala ya kwenda mbele.
4. Teknolojia hiyo inapendekeza wanafunzi wasome kwanza vitabu mbali mbali kabla ya kuingia kwenye darasa...unajua ukitaka kumficha kitu mtanzania unakiweka kwenye maandishi licha ya kwamba vitabu vyenyewe havipo.
5. Nahisi utasema wanatumia pia solar energy kuendesha mitambo hiyo, nenda katika zahanati zetu vijijini uone solar panel moja tu ilivyoshindwa kuhudumia walau spot light ya kijijumba cha zahanati maana utunzaji ulikuwa karibu na zero na sehemu nyingine wajanja walihamishia kwao, sembuse kwenye shule zetu zenye walinzi wa sungusungu?
6. Watanzania tunapenda vitu dhahania na huu nao ni mradi dhahania, watoto wetu hawajui hata kutumia simu na nilimsikia JK akiongelea iPod n.k kana kwamba mtu aliyeko NYANSULUBI na kule kwetu Mabondekwinama atakuwa tu na uwezo huo
7. Mitandao yetu hadi benki na TRA utaambiwa leo mtandao uko chini (hadi kwenye ATM) na TTCL na mkonga wa taifa waliosema ni suluhisho la kudumu na hub iko University of Dar es Salaam na wame-subscribe Mbps nyingi nadhani zaidi ya 12 lakini kaangalie mtandao ulivyo hadi wamelazimika kuomba kuunganishwa na TERNET badala ya mkonga wa taifa ili mambo yaende vema.

Hivyo tusijifanye kama vile tupo na miradi ya kuwaletea tu ulaji watu wa kuuza hizo mashine za namna hiyo wakati hazitazaa matunda. Elimu yetu haijaharibika maana mtindo wa elimu iliyotolewa Tz kuanzia miaka ya 77 hadi leo ni ule ule isipokuwa kitu kimoja tu nacho ni 'alternative to practical' vingine vyote vimebaki ukiacha mabadiliko ya Mungai yaliyodumu kwa muda mfupi. Naye kama hukujua alipewa na kichaa mmoja wa Liege Ubelgiji aliyekuwa na ubia wa kuendesha shule zake kule Iringa kumbe kaingizwa mkenge!Miaka yote hiyo mfumo umefanya kazi vizuri hadi kwenye miaka ya kuanzia late 90's ni vema kujiuliza kwa nini kuliko kutafuta mfumo mbadala maana mfumo ulifanya kazi vema na watu walifaulu na vijana walisifika kote walikoenda kusoma. Hatukuwa na watanzania wasiojua kiingereza wala wa kubabaisha na kuanza kuwa VIHIYO. Unajua wa kwanza kuwa KIHIYO ni mbunge kwa hiyo waliopelekea mambo haya kufika hapa tulipo tuanze na WANASIASA tutapata suluhisho.
Najua unaipenda nchi yako Tz kama ninavyoipenda lakini umeghubikwa na kutetea chama zaidi kuliko nchi...nadhani Tz ni wazo pana zaidi kuliko CUF, CDM, CCM etc
 
Inaonekana wewe hujafatilia ajenda za kikao kile ndio maana unasema haya!

Kuna mambo mbalimbali yenye maslahi kwa taifa yaliyo jadiliwa, nikupe tu mfano;

Kuna teknolojia imetambulishwa nchi, inaitwa Tele Piercing, kama sijakosea, ila namna inavyofanya kazi ni kama ifuatavyo;

Teknolojia hii ni mahususi katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu nchini, kwani kifaa hicho kitafungwa kwenye mashule yapatayo 150 kote nchini, hasa zile zenye upungufu mkubwa wa walimu. Lengo hapa ni kuwezesha mwalimu mmoja, labda aliepo Dar, kuweza kufundisha watoto wote kwa wakati mmoja kwenye mashule yote 150 ambayo yamefungwa kifaa hicho.

Hivyo, kufanyika kwa mkutano huu kumeleta tija kubwa kwa taifa, na sio vyema kupotosha mkuu.

Hivi tatizo la upungufu wa walimu hapa kwetu linasababishwa na nini hasa? kuna tafiti zinaonesha kwamba kuna idadi kubwa sana ya wahitimu katika vyuo vyetu vya ualimu ambao wanaachana na kada hiyo na kujiunga na kada nyingine. kwa hiyo UPUNGUFU WA WALIMU ni matokeo ya tatizo jingine. tuseme upungufu wa waalimu ni sawa na mtu anayeharisha kutokana na kuwa na ugonjwa wa malaria. chanzo cha kuhara huko ni malaria. tiba kamili siyo hasa kutibu kuharisha, bali kutibu malaria. kwa hiyo swali ni kwamba kwa nini watu wanakimbia ualimu? hapo sidhani kama ufumbuzi ni TEKINOLOJIA. hapo ufumbuzi ni suala la utashi wa kisiasa, sera madhubuti, usimamizi makini, kutenga fedha ya kutosha na kusimamia utekelezaji wake. hivyo kuzungumzia tekinolojia hiyo uliyosema, haina tofauti na daktari anayeng'ang'ania kumpa dawa za kuharisha mgonjwa ambaye tatizo lake hasa ni malaria.

Katika tekinolojia za aina hii, nguvu kubwa sana inatoka kwa watengenezaji na wawekezaji. hawa wapo kuuza tekinolojia tu. kwa watu wasio makini, utajikuta unagharimia vitu ambavyo havina msingi na havisaidii kuinua maisha ya watanzania na kuwawezesha kutatua matatizo na kero zao. TEKINOLOJIA peke yake haiwezi kuleta mchango mkubwa kama mchanganuo (analysis)haujafanyika kujua tatizo hasa ni nini na linatatuliwaje, sera (policies) makini hazijawekwa kujua tunaanzia wapi tunaishia wapi, nani anafanya nini, uongozi bora na usimamizi makini. ni kwa sababu hii miradi mingi ya tekinolojia imekwama na kuingiza hasara kubwa kwa wahusika. na hapo sijazungumzia matatizo ya miundombinu kama umeme, madawati nk., walimu waliopoteza ari ya kufundisha, matatizo ya mitaala, nk.

Lakini kama viongozi wetu wanachojali sio mafanikio ya projekti fulani, bali umaarufu watakaopata, kabla ya kesho yake kuanzisha projekti nyingine, na wala sio wao watakaowajibika kulipa madeni hayo moja kwa moja, basi wataendelea kufanya tu ujinga huo na baadhi yetu wataendelea kuwasifia, kana kwamba wanafanya jambo la maana kwa taifa letu, na kumbe wanazidi kutuingiza katika mkenge mmoja baada ya mwingine.
 
nngu007,

Sitaki kuamini kama Rwanda awakupata mwaliko ama Malawi, sina uhakika kama ni wanachama, ila Kenya dharura yake ilitangazwa. Sidhani kama serikali imefanya ulafi wa aina yoyote kwenye huu mkutano, ukizingatia watu mashuhuri wa hapa hapa nyumbani walikuwa wengi. Jambo la kushtua ni kwamba ilikuwaje watu wa muhimu na wenye ushawishi kwenye jamii kama Dr Slaa wasihudhurie?

Simple answer: Mwulize mwenyeji wa mkutano kama kamtosa au Dr kajitosa mwenyewe.
 
Hoja zako hazina mashiko na hatuwezi kuzijadili ziko below kiwango. Nadhani uwahi tu wakupe hizo buku 5 ukale kwani naona hata njaa inachangia. Itabidi JF ichuje watoa na wachangiaji mada ili kuokoa muda. Ni ----- tu huo kwani wapinzani hawawezi kujialika katika mikutano ambayo serkali ni mwenyeji. Samahani hatuna jinsi zaidi ya kukuambia uchukue muda kidogo kuona ni kitu gani unakilleta humu ndani. Kwaheri.
 
Hapo umepotea mkuu. Dr slaa hata kama angekuwepo kwenye huo mkutano angekuwa amehudhuria tu na si mshiriki. Hivyo asingepata hata sekunde ya kuongea

Kumbe mkutano wenyewe haukuwa 'participatory'? Ni vema kama Dr Slaa hakualikwa maana anaamini katika kuwashirikisha watanzania wote mambo yanayowahusu ikiwemo mikataba itakayotokana na mkutano huo kwa nchi yetu.
 
Kuna watu wanamuona Dk Slaa kama Mungu wao vile
Kuna mambo kama wanaona Dk Slaa ana fit anaalikwa na kuna mambo anapotezewa tu
 
Nina mashaka na hiyo AVATAR yako hammy d. Maana naona uwezi maliza siku bila kumtaja Dr Slaa unamfeel sana nini? Ntakutumia no yake umtafute Faragha!
 
Back
Top Bottom