Ni kwamba Bongofleva ya zamani ilikuwa bora au?

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Mimi kila nikitaka kusikiliza nyimbo za zamani za bongofleva nasikiliza kile kizazi kilichotamba miaka ya 2000 hadi 2003 hivi, kwa upande wangu ndo naamini kulikuwa na ngoma kali sana, sijui nipo sahihi au ndo ule msemo wa old is gold, na sijui kama miaka 15 ijayo hizi nyimbo zinazohit sahivi ntaziona nzuri kama nazoziona za enzi zile. Ila nadhan nyimbo za zamani zilikuwa nzuri zaidi na wasanii walikuwa siriaz ingawa wasanii wa enzi hizo walipishana na hela, wasanii wa zamani walikuwa wanaumiza vichwa tofauti na sahivi ambapo wanafocus kutengeneza nyimbo za kuchezeka tu ili wapige show, na ni wasanii wa kuangalia upepo wa mashabiki ndio maana tunaona wakifanya mara kwaito mara za kinaija, enewei tuwaache wafanye hivyo maana wanatafuta hela na kuwaangalia watz wanataka nini. Ila kwangu Mimi hiki kizazi cha kina Profesa Jay, Nature, Daz Nundaz,Jide, Gangwe Mobb, SoloThang, JayMoe, MwanaFa, GK, AY, Afande Sele, Mike T, Dully, TID,Mr Paul, etc kilikuwa kizazi bora kupata kutokea bongo, unakuta ngoma kali kibao zinahit kwa wakati mmoja (Bongo Daslam,Ndiyo mzee,Kamanda, Kigetogeto,Jinsi Kijana,Kama Unataka dem,Bishoo,Machozi,Mtoto wa geti kali,Mambo ya pwani,huyu Na yule,nyaluland,mayowe,mabinti,ni raha tu,hii leo,etc). Hakika hiki ni kizazi cha dhahabu....
 
Wimbo mzuri unabaki kuwa mzuri tu. Haijalishi ni old au new skul
 
Back
Top Bottom