Kwanini Hip hop Bongo inakufa?

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,818
11,542
Zamani hip hop ndiyo ilidominate charts maredioni mpaka mitaani...enzi za kina prof j, Afande sele, Ngwea nk.

Leo hii amapiano, Bongofleva (copy za kinaijeria) na singeli ndio zinadominate kupigwa maredioni mpaka mitaani.

Sikuhizi hakuna wasanii wa hip-hop wanaoshikilia soko kwa kuuza nyimbo au kutoa hit kama zamani.

Karibia wote wamepoa, wametulia hata wakitoa ngoma inabuma au unakuwa chini ya kiwango.

Tatizo nini? Je ni ukosefu wa Ubunifu kwa wasanii au nini? Au hip-hop kama genre imeshakuwa zilipendwa sikuhizi vijana wanataka mziki wa kucheza tu?

Msanii gani wa hip-hop saivi anatrend au anafanya vizuri ambaye watu wanasubiria kazi zake kwa hamu?
Young killer? Young lunya? Rapcha? Darasa? Stamina?

Mbona hao wote hawamfikii hata Dulla makabila?

Tatizo nini?
 
Hip Hop; Reggae zinaendana na Mapinduzi, Utetezi na kuondokana na marginalization (Nyimbo za Hisia, Kupinga Status Quo)....

Sasa hizi zama za Uchawa, Flip Floppers na watu wa kujali matumbo yao - Nadhani walicholishwa ndio kinachowafaa; anyway bora tu tuendelee na nyimbo za mapenzi (language of all Nations)
 
madee aliwaambia miaka mingi tu,

hip hop haiuzi, hip hop halipi,
hip hop kibongobongo bora uuze pipi,
 
Hip Hop; Reggae zinaendana na Mapinduzi, Utetezi na kuondokana na marginalization (Nyimbo za Hisia, Kupinga Status Quo)....

Sasa hizi zama za Uchawa, Flip Floppers na watu wa kujali matumbo yao - Nadhani walicholishwa ndio kinachowafaa; anyway bora tu tuendelee na nyimbo za mapenzi (language of all Nations)
Kwan kina Afande sele na professa jay walikuwa na mapinduzi gani?
 
Wasanii tu siku hizi wa hip hop hakuna..
Ngoma zao wanabwaja bwabwaja tu.

Muziki wa hip hop unahitaji flow nzuri, mashairi matamu na bado kibwagizo kizuri.. Ukitimiza hivyo vitatu ngoma tamu bila shaka.

Muziki huo mwingine muhimu ni iwe tamu sikioni aidha kwa mdundo ama uimbaji(niite tone sijui kitu gani)
Sasa hapa ndipo kina diamond wanapiga bao, hata wakiimba mashairi utumbo lakini ngoma ni tamu masikioni basi wanaishi mjini.
 
Sio Tu hip-hop iliyokufa Bali ni Aina nyingi Tu ya muziki kama vile R&b, zukhu, Dancehall, nyimbo za asili pia .. Ila kwakua umeuliza hip-hop nirudi kwenye mada...
Hip-hop imekufa Kwa sababu kuu mbili nazoziona..

Kwanza uandishi mistari mbovu ambao content zake haziigusi jamii... Umemtaja professor Jay angalia Ngoma zake kama Nikusaidieje au ndiyo Mzee.. au Afande sele Mtazamo unagundua ni Ngoma zilizokua na impact kubwa Sana. Lakini Leo hii Msanii Bora wa hip-hop ni bilinass ukiuliza anaimba nini? Hakuna majibu.

Pili wasanii wengi wa hip-hop wameshindwa kuendana na dunia ya leo... Wengi hawana njia Bora ya kujibrand na kufanya promo ( nyimbo zao sio rahisi kupatikana YouTube au kwenye site kama hizo ) ili washindane na wabana pua ambao nao wanaimba Tu matusi nowadays...

Mengine wadau wataongezea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom