RUBY baada ya kumdisi MAJIZZO aachia Wimbo mkali akiwa na MBOSSO

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,664
4,876
Siku za Juzi kati msanii wa Bongofleva mwenye Sauti yake hapa Mjini Daresalade alimchamba Majizzo na kumtuhumu kumuomba Rushwa ya Ngono na mambo mengine kadha wa kadha. Kitu ambacho kiliibua maswali mengi kuhusu ukaribu wa Rubby na Majizzo. Hata hivyo msanii wa Muziki wa kizazi kipya ameachiwa Album kwa Mujibu wa maelezo yake ambayo pia kwenye video ya kichambo tuliona amesema kwamba majizo alikataa kutoa Sapoti. Lakini mpaka sasa kule YouTube kuna nyimbo mbili tu alizoziachia ndani ya siku hizi mbili baada ya kumchamba majizzo.

Kitu kilichovutia ni namna alivyoamua kumshirikisha mkali wa hizi kazi bwana MBOSSO KHAN kwenye moja ya nyimbo alizoachia. Nyimbo inafahamika kama "Uridhike". Ni nyimbo kali sana.


View: https://youtu.be/M7FaYo86Us8?si=ek4ekdIR1ohtuq7a

RUBY ni msanii mkali sana japo nae ana mapungufu yake. Na kama mwanadamu, hukosi mapungufu yoyote, hata wewe unaesoma hapa una mapungufu mengi tukiamua tuyaelezee mapungufu yako Jamiiforum itafungiwa. Hivyo basi ili tufike kule MTV, BET na kwingineko basi tuhakikishe tunawashika na hawa wasanii wazuri mikono sisi kama mashabiki kwa kusikiliza nyimbo zao. Siamini kwamba dakika Tatu ni nyingi sana kumsapoti kijana wetu kwa kusikiliza nyimbo zake. Tuwe kama wanaijeria, maana wanaijeria wao wanasikiliza na kusapoti nyimbo zao tu kwa asilimia kubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom