Salaam.
Nina mambo Mengi mno ya kueleza lakini kwa sababu sipendi kuwachosheni itabidi nifupishe.
Baada ya kuamishwa kikazi kuja mwanza nilipata binti( mama wa mtoto mmoja) sharti alilonipatia ni kumpangia nyumba, Nami nikakubaliana nae sasa baada ya kupanga anaanza kunitajia vitu kibao anataka sofa, flat screen, kitanda cha chuma, subwoofer, red carpet, vyombo vipya nk.
Ukiangalia mirija yote ya kupata pesa ya ziada siku hızı hakuna mtu unategemea mshahara tu nao ni laki Saba tu kwa mwezi. Pili sijaona faida kabisa ya kuwa na mchepuko usawa huu ni vikwazo vikubwa vya maendeleo. Hivyo niamua kupiga chini kwa sababu input ni kubwa mno kuliko output.
Labla anayejua faida ya kuwa na mademu wa staili hii anijuze.