Ni kosa la kiufundi au ni makusudi??

Ni kosa la kiufundi au ni makusudi??

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,589
Reaction score
28,755
29365531_1783085288409224_8774057099790385152_n.jpg


Unamchukua Mohamed Dewji na Bakhresa unawaweka pamoja, halafu unawapa maji ya kunywa ya Kilimanjaro mshindani wao mkubwa katika biashara ya maji.

Kumbuka Bakhresa anamiliki brand yake ya maji na Mo anayo pia.

Wenzetu kwenye nchi zilizoendelea kwenye mikutano mikubwa kama hii inayokutanisha mahasimu wa kibiashara huwa wanatumia maji yasiyo na brand au wanatumia maji ya kwenye jagi kabisa au ya kwenye water dispenser.

Hili lilikuwa ni kosa la kiufundi au ni makusudi??
 
Hayo maji sio lazima wayanywe pia hapo hawakuwa kibiashara.
 
Kwahiyo ulitaka mengi anywe yake bakhresa anywe uhai,mo anywe maisha,oilcom wanywe yakwao?
 
Mi nahisi ni bora wangewekewa maji ya mito au ya bahari[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji377] [emoji377] [emoji377] [emoji124] [emoji125] [emoji125]
 
Sasa mwenyekiti wao si ni mengi, ambaye tena alikaa meza juu na magufuli so no problem acheni tu hayo maji yakae hapo
 
Kwa Tz itachukua miaka mingi kuja kuwa na brand ya maji yenye hadhi zaidi ya Kilimanjaro, dhifa au sherehe zote 'kubwa' hautokuta kitu tofauti na Kilimanjaro. Si suala la ubora tu bali hata ku establish label(brand) huchukua muda,maarifa pamoja na nguvu(juhudi) kubwa.
 
Vipi majumbani kwao wanakunywa hayo maji wanayowauzia?!
 
Hiyo picha nimejaribu kwa haraka haraka kuhesabu wafanyabiasha weusi, si wengi sana
 
Halafu mbaya zaidi mwenye hayo maji, alikua kakaa high table, bora hata angekua kakaa huko back bench au nje ya ukumbi kabisa.
 
Back
Top Bottom