Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Kaka bati nimenunua mwenyewe za kupima kihusu kuibiwa never mana mi alipima nikaagiza kiwandani fundi hakuusika kwa namna yoyote mzee
Ok labda sababu nimeangalia upande mmoja tu
Au yawezekana upana bati ni chini ya 90cm
 
Mchwa dawa yake ni kumuondoa malkia lakini hayo mambo ya madawa ni kudanganyana kuna watu wenye utaalam wa kuwaondosha mchwa.
Yule malkia sehemu anapoishi pamejengwa na kuimarishwa kiasi kwamba vitu kama moto au kemikali haviwezi kumdhuru. Na kama kwenye kichuguu hujamuondosha malkia basi hujafanya kitu
Hapo ni kuchimba shimo na kupiga baruti lipua kichuguu kizima
 
Kwa structure yoyote inayohusu ulinzi
Tumia square pipe, nondo au iron sheet (za mageti)

Wako mafundi wazuri wa kuku design-ia kitu kikawa kizuri cha kuvutia.

Flat bar hapana kwa kweli.
Hizi Tumia kwa structure zinazohitaji urembo na sio ulinzi.

#YNWA
Ila mpaka leo wizi wa majumbani ni kweli Tanzania bado maskini sasa majumbani utaiba nini zaidi ya TV na simu
 
Changamoto Ni Nini?? Na Kuisha Kwa Nyumba Inategemea Ni Stage Ipi?? Je Ww Ulihamia Bila Kuweka Madirisha Au Bila Kuweka Paving Maana Zote Hapa NI NYUMBA Ambazo Hazijaisha Inategemea Na Mlengo La Mtu Na Mtu.
Mi nahisi utachelewa kuimaliza maana utaona haina shida utaanza zoea gofu
 
Sana Mkuu, alafu hajui mali ya wizi hata huwezi kuifanyia jambo la manufaa.

Hao mafundi wameniibia lakini hakuna cha ziada wamefanya zaidi ya kwenda kulewea hela zangu pamoja na kuhongea mademu.

Saivi nikitaka kujenga ni vyema niweke kambi hapo hapo hadi Ujenzi uishe kwa hatua niliyopanga
Nilisimamia ujenzi wa nyumba ya familia nikajifunza baadhi ya kanuni!!

1. Kugawanya ujenzi kwa phases, ambapo phase ya kwanza msingi, ya pili kupandisha na ya tatu kupaua hapo unakuja kwenye finishing hiyo ni phase ya nne yenye vipengele vidogo vidogo kama plambing, mabomba ya umeme, plasta, madirisha (grill) na n.k.

2. Kugawanya phases na kujengea mfukoni, unakwenda site na ramani yako unafanya makadirio na fundi ya gharama, nguvukazi na materials kwa phase ya kwanza. Unachofanya kadirio la fundi unaongeza na wewe kidogo (mafundi hawajui kukadiria). Unakusanya ile pesa.

3. Ukishakusanya pesa ya phase, unatafuta wiki au siku kumi za kazi ya phase 1. Mfano; ushaongea na fundi msingi utatumia siku nne, saa kumi na mbili upo site halafu wa mwisho kuondoka. Angalau utapunguza kupigwa na fundi na phase ya pili hivyo hivyo

4. Unapogawanya ujenzi kwa phase maumivu ni madogo sana. Mfano foundation m1.7 unatafuta m2 unasimamia show ukimaliza unaondoka na mahesabu ya kupandisha labda m4 unakwenda kuitafuta. Baada ya miezi ukirudi nyumba inapanda wiki tu mpaka inaisha japo ulisimama kwa miezi sita. Ukiondoka hapo na hesabu za kupaua na n.k.

NB: Ujenzi hakikisha unachorewa ramani tena mchoraji anafika site kuangalia eneo atakushauri vizuri sana
 
Shukrani kushare Kiongozi, watu hujifunza kutokana na makosa.

Kupitia andiko lako na mengine walioshare wenzetu hapa, wengi watajifunza.
 
Pole sana Mkuu, mafundi wengi wamekuwa sio waaminifu.

Kuna mmoja nilipoona ananiibia nikiwa mbali, nikafanya maamuzi ya kumpeleka Wife kusimamia.

Alichokifanya ilikuwa nikilipia kwa Supplier tofali 1000 basi yeye anamwambia Supplier apeleke tofali 750 badala ya 1000.

Hiyo siku nikatimba Site bila taarifa na nikaanza kuhesabu mwenyewe hizo tofali, mbona nilimtimua siku hiyo hiyo na huyo Supplier naye nikavunja mkataba naye pia.

Mafundi wanatuumiza sana Wajenzi, ujenzi wa Milioni 100 unaweza kuta unatumia milioni 120 usipokuwa makini
Sasa hapo kilaza ni fundi au supplier?
 
KUANZA KUJENGA NA FUNDI ASIE JUA KUFANYA SETTING YA MSINGI!!!!!!! MSINGI HAUKUWA SQUARE NA ILIONGEZA GHARAMA KWANGU , LAZIMA UNAPOAANZA KUJENGA TAFUTA MTAALAMU UMLIPE, MALIPO INATEGEMEA NA AINA YA NYUMBA THEN NDIYO UENDELEE NA MAFUNDI WA KAWAIDA KAWAIDA. NAOMBA SANA MZIGATIE HILI NDG ZANGU MAANA NAJUA HUMU WAJUAJI WENGI :D

Pia kuna kosa kubwa la kutokuwa na walewa mdogo wa plumber au maksudi kutaka urahisi Kwanza kwenye Bathroom kufanya setting choo, sehemu ya kuogea na wash basin vikae vipi? sasa unakuta fundi sehemu ya kuongea inakuwa ya kwanza ukifungua mlango tu then inafuata wash basin mwisho kwenye ukuta na juu kidirisha ndiyo sasa kinakaa choo , sasa ebu fikiria unavyooga maji ya shower yanaruka mpka mlangoni ndiyo sasa yanaelekea upande wa choo ndiyo yanatoka, ukimuuliza fundi anakwambia kutakuwa na slope kali haina shida!!!!! kimsingi kwenye set up unaanza na wash basin au choo then mwishoni unaweka sehemu ya kuogea (shower) kosa lingine ni plumber kuweka heater ndani ya bathroom badala ya kuiweka nje tena unakuta kila bathroom ina heater yake wakati inawezekana kuweka moja ikatumika hata bathroom tatu. AKSANTENI.
 
Nimejenga uelekeo wa jua linapochomoza na jua linapozama yaani ilo joto lake full shangwe mchana hakukaliki jua linapiga sebuleni na chumbani kwangu usiku napo hakulaliki.mafundi vimeo sana wanashindwa hata kutoa ushauri
Piga ukuta mrefu + Mapazia mazito

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Dah
"Sasa mwanzoni nilipanga yule wa kiume ndio atakuwa analala kwenye hiyo underground lakini ameniambia baba fanya ufanyavyo ila mimi sitalala huku bondeni kwenye banda la kuku akimaanisha ile underground."

....
Siku nyingine ukitaka kujenga,
Jipe muda kwanza wa kuitafakari ramani..
Heri upoteze muda kabla haujajenga,kuliko kujenga haraka ramani ambayo haujaridhika nayo.
Mkuu soma tena andiko langu, kwa kifupi hata ramani sikuwa nayo nilicholewa na Fundi mchundo tu harakaharaka alipofika site. Nilikataa gharama za mchora ramani 350K kumbe ndio naingia kwenye gharama kubwa zaidi.
 
Nyumba yako inafanana na nyumba Fulani huku mtaani ninakoishi
Au ndio hiyo?

Mwenye nyumba naye saa hii atakuwa anajutia.
Yeye hicho kichumba kiduchu Cha chini ameweka mpangaji,sijui anaishije mule maana ni kidogo,kimlango kiduchuu ila ni mwembamba anapita.
Hapana sio hiyo, nyumba yangu bado haijaisha.
 
Back
Top Bottom