Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Mkuu soma tena andiko langu, kwa kifupi hata ramani sikuwa nayo nilicholewa na Fundi mchundo tu harakaharaka alipofika site. Nilikataa gharama za mchora ramani 350K kumbe ndio naingia kwenye gharama kubwa zaidi.
Aisee
Pole Mkuu
 


Wewe ulitoa mpya bila Raman tena
Halafu akaanza tu ghafla
Yaani hela anayo mkononi,kila kitu anacho
Anataka kujenga na ramani hana

Hakuwahi hata tamani ya mtu akapaste,akamuachia mwamba achorechore
Na ujenzi fasta ukaanza

Kujenga bila plan ni kazi jamani,
Kuna ndugu yangu Kila mwaka anafanya marekebisho
Ukienda kesho utakuta amebadili mlango ameweka huku
Ukienda Tena mara amebadili sebule
Mara amekata vyumba
Yaani hekaheka kama zote.
 
Kampuni wanachokifanya ni kutafuta mafundi wazuri tu, kwanini usitafute mafundi wazuri wewe mwenyewe badala ya kulipa kampuni kukutafutia fundi.
Kampuni wanatumia mafundi hawa hawa, wao wanasimamia standards tu.

Ujue hata wajenzi huchangia, mtu anatumia kokoto kubwa sana, hatumii vibrator ili aggregates zikae vizuri.

Mafundi wazuri wapo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Dirisha la jikoni kuwekwa baada ya kozi mbili ,matokeo yake wakati wa plumbing imekua ngumu kuweka sehemu ya sink, nimeingia hasara ya kutoa grill likakatwe na kupandisha kozi mbili tena ili kupatikane mahali pa kuweka sink la vyombo,sikutaka libanane kwenye kona

Fundi kutotoboa msingi ili nyumba ipumue,hapa nafikiria kutoboa hata kama nyumba imeshapanda.

Kujenga mashimo mawili ya choo badala ya moja,hii najutia mpaka kesho ,kila mtu site naona anajenga moja

Kupandisha kozi 11 badala ya 10 baada ya msingi,matokeo yake nyumba imekua ndefu sana
Nyumba ikiwa ndefu si ndo vizuri au?
 
Kuamini mtu (msimamizi) wa karibu aliyekuwa anasimamia nyumba ilinigharimu wakati wa kutaka kuhamia .kumbe nyumba ilikuwa inavuja kama kuku aliyekatwa kichwa .Hakuwahi kunieleza mapema mbaya zaidi fundi amerekebisha mpaka kaamua kuniblock
 

Attachments

  • IMG_20230323_035144_884.jpg
    IMG_20230323_035144_884.jpg
    327.1 KB · Views: 76
  • IMG_20230323_035039_806.jpg
    IMG_20230323_035039_806.jpg
    223.7 KB · Views: 78
Ulitumia mashine ya umeme yenye mixer na vibrator au ile shindilia ya mkono (bambam)? Ulinunua au ulikodi?

Kuna gharama ya kununua mchanga, cement, vibao, maji ya kumwagilia, gharama ya kuwalipa wafyatua tofali, vibao vya tofali na gharama ya umeme kama utatumia vibrator na mixer


Ili utoe tofali 3000 kwa ratio ya 40 utahitaji cement mifuko 75 (cement 1@16,500)
●Mifuko 75@16,500= 1,237,500

Mchanga wa tofali 3000
●Mchanga mnene trip 2@400,000= 800,000 (FAW ton 20)
●Mchanga mlaini; Bagamoyo/Kibaha trip 1@350,000 (SCANIA mende)

Gharama za wapiga tofali (Mfuko 1@4000)
●Mifuko 75@4000=300,000

Kibao 1@1700
●Vibao 1000@1700=1,700,000


HADI HAPO TAYARI 4,387,500
SIJAHESABIA GHARAMA ZA KUKODI/KUNUNUA MASHINE, MAJI NA UMEME

UKINUNUA TOFALI 3000@1100 NI 3,300,000

NB: GHARAMA INATEGEMEA NA ENEO HUSIKA HIYO HESABU NI KWA MKOA WA DAR
Umempa hesabu nzuri sana, ukijumlisha na muda unakuwa umepotea mazima, sasa ivi tofari ya mashine ya umeme ni elf moja mpaka kwako na unachagua kila mpigaji kwa ubora unaotaka, kupiga mwenyewe ni hasara
 
Back
Top Bottom