Ni kitu gani kinachoifanya ndege ipae...

Ni kitu gani kinachoifanya ndege ipae...

Mimi napendelea sana mambo ya ndege (aeroplanes), na mara nyingi huwa youtubes huwa nacheki ndege jinsi inavyopaa, kutua, sauti zake, aina mbali mbali za ndege, jinsi pilot anavyosukuma pipa ndani ya cockpit wakati wa take off (kupaa) na approach and landing (kushuka na kutua).

Nimegundua wakati wa kupaa pilot hana kazi sana kulinganisha na wakati wa kutua (landing) pale pilot naona anapata shida kidogo maana umakini unakuwa mkubwa kuliko kwa jinsi nilivyoona kupitia youtube. kweli ndege ina raha yake.

Ila kitu kinachonisumbua mimi ni kwamba ni nini inaifanya ndege ipaeee?

MabawA yake
 
Mimi huwa napenda kuangalia ndege zinazocrush........jinsi watu wanahangaika humo ndani....kichwa kinavyokatika na kuacha mkia.....jinsi inavyoangukia pua.......vile ikianguka majini inavyopiga mbizi.......au zikigongana moja ikiingia ubavuni mwa mwezie......napenda sana........[/ Duh!!
 
Takeoff part hapa ndege inatakiwa iwe spidi takeoff ni kuanzia 280kph hapa ndege itaweza nyanyuka na kupaa kitu cha pili tunasema high angle of attack ili ndege ipae lazma eneo la bawa liongezeke kuna vitu vinaitwa slap and flaps huwa vinachomoza kwa chini vinatengeneza downward shape husaidia kuongeza presha na mkandamizo chini hvo ndege inapaaa na bila kusahau eleveta ipo nyuma mkian wakati wa kupaa huwa inanyanyukw juu hvo husaidia kichwa cha ndege kunyanyuka.
 
Thrust force inavozid kuwa kubwa ndo ndege inazidi kupaaa,, airplane physics ni noma, wataalam walikaa na walituliza akili sio mchezo
 
kupaa na kutua kwa ndege kunategemea na shape ya mabawa kwa wakati husika.

Jaribu hili
ukiwa kwenye gari inayoenda kasi, jaribu kutoa kiganja chako nje huku vidole vyote vikiwa vimenyooka na kikiwa kinaangalia chini, na wakati gari iko kwenye mwendo kazi jaribu polepole kubadilisha shape ya kiganja chako jaribu kuzungusha kiganja kuelekea gari linapoenda (yaani vidole viangalie upepo unapotokea) na utashangaaa mkono unavyonyanyuka na pia jaribu kugeuza tena kiganja ili mgongo wa kiganja uwe unaangalia upepo unapotokea na utashangaa mkono unavyopelekwa chini
ahsante mwalimu mfano rahisi sana kuuelewa
 
Back
Top Bottom