Ni Kisa kingine cha kusikitisha.................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Kisa kingine cha kusikitisha..................

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Masikini_Jeuri, Aug 17, 2010.

 1. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mama mmoja mkazi wa Nkuhungu hapa mjini Dodoma, jana amelia kwa masikitiko makubwa na kutoamini baada ya kumkuta mpwawe wa umri wa miaka 4 akiwa kaumizwa vibaya kwa kupigwa na kuchomwa na pasi mgongoni na shangazi yake mdogo (Binamu yake huyu mama). Shangazi mkubwa aligundua hilo baada ya kupita siku 3 tangu mpwa atendewe ukatili huo! (Tunalo la kujifunza hapa wazazi na walezi)!

  Mtoto huyo amabaye amefiwa na Baba (Kaka yake na huyu mama) alichukuliwa kuletwa kutunzwa na shangazi yake hapa Dodoma na wakati huo huo huyu Mama alikuwa anaishai na binamu yake (Shangazi mdogo) amabaye ndiye amekuwa akiwasaidia kazi za pale nyumbani kama dada wa kazi.

  Kwa mujibu wa maelezo ya mtoto ni kwamba amekuwa akifanyiwa vitendo vingi sana vya kunyanyaswa na kuteswa na tukio hili ni baada ya kujinyea! Shangazi mdogo kwa hasira alimshushia kipigo mtotto huyo na hiyo haikutosha alimwamuru avue nguo na kisha alimchoma na pasi ya umeme mgongoni ! Ili kuficha maovu haya alimtishia kuwa atamwadhibu zaidi akija kumsema kwa shangazi mkubwa na pili alimvisha pull over kila wakati shangazi mkubwa akiwepo; Piga picha ya mateso aliyovumilia mtoto huyo kwa siku 3!

  Kilichosababisha kugundulika jana ni baada ya shangazi mkubwa kuchelewa kuelekea mihangaikoni alipitia chumbani kwa mpwawe na kugundua kuwa amekojoa kitandani. ndipo alipomwamsha na kumkuta akiwa na nguo nzito mwilini na zikiwa zimelowana. Hivyoa limvua nguo zote na ndipo alipokutana na jambo la kusikitisha........!

  Alichokifanya shangazi mubwa ni kumsafirisha huyo binamu yake arudi kwao! Nampa pongezi kwa moyo wake wa kusamehe lakini pia sidhani kama ni hatua sahihi! Anasema anahisi kuwa endapo angechukua hatua ya kisheria ni wazi huyu binamuye angefungwa na hilo huenda lingepelekea kugombana nandugu zake ambao ni wazazi wa huyu Binti (Binamu). na pili kwa ukatili huo anaogopa kuwa baada ya kutoka huyu mtu anaweza kuja kumdhuru hata kwa kumuua.

  Wana JF hasa sie wazazi na walezi naomba kwa pamoja kwa nafasi zetu tuwaombee wanetu! Tuombe ulizi wa Mungu kwa wanetu! Pili tuwaombee hawa wanaotusaidia kulea wanetu!

  Mungu aingilie kati!:amen:
   
 2. Mnene 1

  Mnene 1 Senior Member

  #2
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du! huyo mwanamke ana roho ya kikatili sana.
   
 3. Braniac

  Braniac Senior Member

  #3
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh no comment
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Na Mungu wetu aliye hai na amfanya huyo shangazi mdogo TASA!! Asizae hata mjusi wa kupandikizwa! Ana pepo la mauaji huyo.
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Visa kama hivi ni kuvipeleka mbele ya sheria sijui angekuta amemuua huyo mtoto ingekuwaje kuna watu wana roho za kikatili sijui wanapokuwa wanafanya matendo kama hayo hasa kwa mtoto mwenye umri huo anakuwa anajisikiaje au laiti kama huyo anayefanya kitendo hicho angekuta mwanawe anafanyiwa hivyo angejisikiaje au angechukua hatua gani kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana.

  Hapo kwenye nyekundu najaribu kufikiri ila sipati jibu :confused2: sijui kama mtu mwingine akute mtoto wake amefanyiwa hivyo anaweza akasamehe kwa kuogopa kugombana na ndugu zake.
   
 6. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :pray: aisee inasikitisha saaana.
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  eeeiii...lakini jamani kuna watu wakatili ana jamani.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ee bwana sasa ile movie vipi?
   
 9. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Afu wewe unapendaga kweli kwenda off topic, movie nPM nkupe maelekezo, hivo hii story umeisoma kweli weye???
   
 10. m

  mramba Member

  #10
  Aug 17, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ash!
  Huyu shangazi mdogo ana moyo au jiwe la mtoni!!.
  Na huyu shangazi mkubwa leo kachelea asigombane na nduguze je, ingekuwa ni mwanaye kafanyiwa hivyo pia angechelea au ni kwa sababu siyo wake?
  Na kama kaogopa hao nduguze watakaomsema vibaya na huyo mama wa mtoto huyo asiye na baba haogopwi ataumia roho na kusema vibaya? AU KISA MTOTO WA MJANE??
  Shangazi mkubwa hajatenda haki hata chembe na simpongezi balli namlaumu.Angepeleka mbele na mambo yendelee kihaki ili kila mmoja alipwe ujira wa kazi yake!
  sasa leo umeogopa ya ndugu zako na ya Mungu wako utaogopa lini shangazi mkubwa?
   
 11. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha.. Bora uishi na mnyama kuliko ukutana na binadamu kama huyo.
   
 12. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ndugu zanguni;

  Mimi niliposikia milisismkwa! Kwani nilipiga picha ya kuwa jr ndo mtoto anayefanyiwa haya yote...............! Oooh Mungu atusaidie kwa kweli ndio maana nikapongeza moyo huo wa Shangazi..................Binafsi NINGECHUKUA HATUA KALI SANA! Iwe fundisho kwa makatili wengine wote!:mad2::mad2::mad2:
   
 13. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Eee Mungu mpe ahueni huyu mtoto na mpunguzie maumivu! wakati mwingine huwa nashindwa kuamini kabisa kama roho hizi katili pia zinaamini kama kuna moto wa milele. Shangazi mkubwa amekosea kidogo kabla ya kumrudisha kwao angemvizia wakati amelala akamchoma " maeneo" ili asije fikiri siku moja kukutana na mume nae apate mtoto wake, yaani kifupi nagemfanya tasa kiaina.
   
 14. D

  Dick JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo mwanamke ana roho mbaya kuliko shetani. Tumwombe Mungu ampe nafuu huyu malaika (mtoto).
   
 15. ghumpi

  ghumpi Senior Member

  #15
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Shangazi mkubwa pia wa kulaumiwa. she is nt responsible at all!! kwa nini anafcha maovu?
   
 16. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mungu aingilie kati!:amen: Huo ni ushenzi uliopitiliza kituo, what do you expect from a 4 yrs kid? Kaniaribia
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  maskini huyu shangazi ana roho kama mkaanga sumu..hivi kuna watu hawajui uchungu wa Mwana? so sad
   
Loading...