Kambi ya Fisi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,514
- 22,002
Mhuni wa kiume atamzushia kuwa kamla mdada mwenye kujiheshimu ili kuharibu heshima yake.
Hali kadhalika mdada mhuni atazusha vivyo hivyo kwa mkaka mwenye kujiheshimu.
Kuna mhuni atakuzushia kwamba umeiba kwa mwajiri wako ili akuharibie kibarua chako, kuna wahuni watakuzushia kwamba una makundi ya kigaidi na unataka kupindua serikali. Watazusha ili wakugombanishe kisiasa.
Ikiwa watu wanaweza kuzusha uongo katika jina la Mungu, kwa nini huwa unastuka wanaposema uongo kuhusu wewe?
Ikiwa watu walimzushia Yesu kuwa ni mlevi na mwenye pepo, kwa nini upoteze akili unapozushiwa uongo?
Yusufu alizushiwa uongo kwamba alimbaka mke wa bosi wake, Yusufu alitulia japo alipelekwa gerezani lakini Mungu alimthibitisha kwa kumtoa gerezani na kumpa ukuu.
Sio lazima kupigana jino na kucha ili kutakasa jina lako . Tulia, kisasi ni cha Mungu.
Ubarikiwe.