Ni kama vile Spika Ndugai anakaimu na nafasi ya KUB, maana siyo kwa ukosoaji huu anaoufanya bungeni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Binafsi nimeridhishwa sana na utendaji wa Spika Ndugai katika mkutano wa bunge unaofungwa leo.

Ndugai ameweza kuikosoa serikali katika baadhi ya mambo yakiwemo ajira kwa vijana, riba kubwa kwenye mikopo ya elimu ya juu, SUA kuacha majukumu yake ya msingi na kuanza kufundisha walimu wa sekondari na hata kuwakemea " kimtindo" wabunge wanaopiga makofi kama walevi bungeni.

Pamoja na kwamba bunge hili halina KUB japo wabunge wa upinzani wamo kiukweli Ndugai ameziba pengo la KUB.

Maendeleo hayana vyama!
 
Unamfurahia mtu anayejitekenya na kucheka mwenyewe!

Mfano kuhusu hilo suala la riba kubwa ya mikopo ya juu lilipitishwa wapi kutumika kama sheria? Si hapo hapo Bungeni na hao Wabinge wenu wa Ccm huku wakipiga na vigelegele!

Yaani mnatengeneza wenyewe tatizo, halafu mnakuja baadae kujifanya kuwa ni wakombozi! Yale yale ya kikokotoo!! All in all, CCM must go!! Inatuchelewesha sana kuyafikia maendeleo ya kweli.
 
Kwani hiyo sheria ya Bodi ya Mikopo ya kukata asilimia 15 wakati inapitishwa yeye si ndio aliongoza wabunge wa CCM kuipitisha kwa kura ya ndiooooo.

Hata CAG alieshauri hiyo sheria ni mbovu si walimuondoa kwa mizengwe badala ya kufanyia kazi ushauri aliokuwa anawapa juu ya mambo mbalimbali.
 
Ilitakiwa KUB wa wakati ule aipinge!
 
Binafsi nimeridhishwa sana na utendaji wa Spika Ndugai katika mkutano wa bunge unaofungwa leo.

Ndugai ameweza kuikosoa serikali katika baadhi ya mambo yakiwemo ajira kwa vijana, riba kubwa kwenye mikopo ya elimu ya juu, SUA kuacha majukumu yake ya msingi na kuanza kufundisha walimu wa sekondari na hata kuwakemea " kimtindo" wabunge wanaopiga makofi kama walevi bungeni.

Pamoja na kwamba bunge hili halina KUB japo wabunge wa upinzani wamo kiukweli Ndugai ameziba pengo la KUB.

Maendeleo hayana vyama!
Duh..
Hata Sheitwani huwa ana wapambe wake🙄
 
Anajitahidi bonge lionekane linakosoa sirikali kuliko enzi za wapinzani machachari... Sasa limekuwa la malalamiko tuu bila masuluhisho ukizingatia mshikanchi halizingatii anafanya anavyoona yeye basi nikakikundi ka porojo za wavaa suti na kutafuna fedha za umma.
Wenye welewa hawawafuatilii wala hawajui kama wanakutana
 
IMG_20210211_163253.jpg
 
Lakini wewe unafuatilia!
 
Ndungai hana cha kupoteza. Alijipendekeza 2015-2020 ili asikatwe. Na anastaafu 2025 kwahiyo anahakikisha anastaafu vizuri. Ndani ya CCM hakuna anayemwelewa Jiwe. Ngoja ifike 2024 ndiyo atawajua wana CCM
2024 ni mbali, mabadiliko yapo njiani
 
Back
Top Bottom